Skip to main content

Posts

Showing posts from February 7, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Prof.Shemdoe, Akutana na Mkurugenzi wa Benki ya Azania Kujadili Maendeleo ya Ushirikiano

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI) Mhe. Prof. Riziki Shemdoe amekutana na Mkurugenzi mtendaji Benki ya Azania Bi. Esther Mangenya na kufanya mazungumzo ya namna bora ya kushirikiana katika kuboresha utoaji wa huduma za afya msingi, elimu msingi na ujenzi wa miundombinu ya barabara pamoja miundombinu ya huduma nyinginezo za kijamii. Prof. Shemdoe alifanya mazungumzo hayo na Mkurugenzi Mtendaji huyo wa Benki ya Azania tarehe 05 Februari 2026 ofisini kwake Jijini Dodoma, alipomtembelea kwa lengo la kujitambulisha ili kujenga mahusiano mazuri ya kiutendaji yatakayowanufaisha wananchi waliopo kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa. Katika kikao kazi hicho, Prof. Shemdoe na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania Bi. Esther Mangenya wamekubaliana kujenga mahusiano mazuri ili wananchi wanufaike na mchango wa Serikali na benki hiyo katika kuboresha miundombinu ya utoaji wa huduma za kijamii. Kwa kutambua mchango wa taasisi za kifedha kwa jamii,...

DC Itunda Ahimiza chakula mashuleni Mbeya

📍 Ammwagia sifa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuboresha miundombinu Na Mwandishi Wetu, Mbeya MABORESHO yanayofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita katika sekta ya elimu yameendelea kuzaa matunda baada ya ufaulu wa wanafunzi kuongezeka kwa kasi nchini.  Akizungumza na wadau wa elimu Jijini hapa, Mkuu wa wilaya ya Mbeya Mhe Solomon Itunda alisema maboresho katika sekta ya elimu yamesaidia kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa ufaulu nchini. Itunda alisema hatua hiyo imetokana na  uamuzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kutoa mabilioni ya fedha kwa ajili ya ujenzi wa madarasa, maabara, na uboreshaji wa mazingira ya kufundishia, jambo ambalo limerejesha hamasa ya kusoma kwa wanafunzi na walimu. Alisema katika kuyaenzi maboresho hayo na kuhakikisha tija inaonekana darasani, Mkuu huyo wa wilaya amewaeleza wadau wa elimu Jijini Mbeya kwamba ni vema kuweka mkakati wa kudumu wa ustawi wa wanafunzi ikiwemo kuhakikisha kila shule watoto wanapata chakula...

Waziri Mkuu Mstaafu Majaliwa Akutana na Tume ya Jaji Chande

DODOMA: TUME ya Uchunguzi wa Matukio ya Uvunjifu wa Amani yaliyojitokeza wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, Leo Februari 6, 2026 imekutana na Waziri Mkuu Mstaafu Kassim Majaliwa. Mkutano huo wa Tume na Majaliwa umefanyika katika ukumbi uliopo katika Jengo la Takwimu lililopo mkoani hapa. Miongoni mwa yaliyojadiliwa katika mkutano huyo ni pamoja na namna matukio hayo yalivyoanza, athari zake kwa watu, mali na miundombinu pia ushauri wa namna ya kuondokana na matukio hayo. Tume inaendelea kukutana na makundi mbalimbali wakiwemo waathirika wa Matukio hayo ambapo kwa Dodoma tume inaendesha shughuli zake katika Ukumbi wa Takwimu, kwa Mkoa wa Iringa Tume ipo Ukumbi wa Siasa ni Kilimo na kwa Shinyanga Tume ipo katika Ukumbi wa Manispaa ya Kahama.

Mzee Pinda Afika Mbele ya Tume ya Jaji Chande

  DODOMA: TUME ya Uchunguzi wa Matukio ya Uvunjifu wa Amani yaliyojitokeza wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, Leo Februari 6, 2026 imekutana na Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda. Mkutano huo wa Tume na Pinda umefanyika katika ukumbi uliopo katika Jengo la Takwimu lililopo mkoani hapa. Miongoni mwa yaliyojadiliwa katika mkutano huyo ni pamoja na namna matukio hayo yalivyoanza, athari zake kwa watu, mali na miundombinu pia ushauri wa namna ya kuondokana na matukio hayo. Tume inaendelea kukutana na makundi mbalimbali wakiwemo waathirika wa Matukio hayo ambapo kwa Dodoma tume inaendesha shughuli zake katika Ukumbi wa Takwimu, kwa Mkoa wa Iringa Tume ipo Ukumbi wa Siasa ni Kilimo na kwa Shinyanga Tume ipo katika Ukumbi wa Manisapaa ya Kahama.

Profesa Hubert Kairuki Atajwa Kama Shujaa Sekta ya Afya

Na Mwandishi Wetu MWANZILISHI Mtandao wa Afya na Elimu Kairuki (KHEN) na Hospitali ya Kairuki, Profesa Hubert Kairuki ametajwa kama mtu alieacha alama isiyofutika kwenye maisha ya watanzania kutokana na maono aliyokuwa nayo wakati wa uhai wake.  Hayo yaliibuliwa na washiriki wa mjadala wa kumbukumbu ya miaka 27 ya kifo cha Profesa Kairuki uliofanyika katika hospitali ya Kairuki Mikocheni jijini Dar es Salaam. Watoa mada kwenye kongamano hilo walieleza namna walivyomfahamu Profesa Kairuki na namna alivyosimamia maono yake ya kuhakikisha anasaidi jitihada za serikali katika kutoa huduma za afya. Mgeni rasmi kwenye kongamano hilo, Dk Egina Makwabe ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Wenye Hospitali Binafsi (APHFTA), alisema Profesa Kairuki atakumbukwa kwa kuwa mstari wa mbele kuanzisha hospitali binafsi ya kwanza. Alisema wakati huo ambapo serikali haikuwa inaruhusu watu binafsi kuwa na hospitali, Profesa Kairuki alisimama kidete kuhakikisha anatimiza ndoto zake na alifanikiwa kuanzisha...