Skip to main content

Posts

Showing posts from October 1, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Jenista Mhagama:Miundombinu sekta ya afya peramiho yazidi kuimarika

Serikali kupitia Wizara ya Afya imetoa shilingi Bilioni 40 kwa mwaka wa fedha2023/24 ili kuendelea kuimarisha miundombinu ya miradi mbalimbali ikiwemo ya Sekta ya Afya kwa kujenga Hospitali pamoja na vituo vya Afya katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma ikiwa pamoja na Jimbo la Peramiho. Waziri wa Afya na Mbunge wa Jimbo la Peramiho Mhe. Jenista Mhagama amesema hayo Septemba 24, 2024 wakati wa ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Jimbo la Peramiho, Songea Mkoani Ruvuma. "Kwa Mwaka wa fedha 2023/24 Serikali imetoa fedha kiasi cha Tsh: Bilioni 40 katika Jimbo la Peramiho ili kutekeleza miradi ya maendeleo katika Sekta mbalimbali ikiwemo Sekta ya Afya kwa kujenga Hospitali pamoja na Vituo vya Afya." Amesema Waziri Mhagama Aidha, Waziri Mhagama amesema Serikali kupitia Wizara ya Afya imeendelea kufanya kazi na Hospitali ya St. Joseph's Mission ya Peramiho kama Hospitali ya Rufaa

Waziri Simbachawene avutiwa na maendeleo yaliyofikiwa katika majimbo ya musoma vijijini na mjini

Na Shomari Binda-Musoma WAZIRi wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti, Utumishi wa Umma na Utawala Bora George Simbachawe amesema ameshuhudia mambo makubwa ya maendeleo kwenye jimbo la Musoma vijijini na mjini. Kauli hiyo ameitoa leo oktoba mosi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Mara sekondari mara baada ya kufanya ziara kwenye majimbo hayo. Amesema serikali imekuwa ikileta fedha nyingi mkoani Mara na zimetumika vizuri na kuwaletea wananchi maendeleo. Waziri huyo amesema vijana wanayo nafasi ya kufahamu shughuli za maendeleo inayotekelezwa na wasidanganywe na watu wanaopotosha. " Waheshimiwa wabunge wote wawili Profesa Sospeter Muhongo wa jimbo la Musoma Vijijini na mheshimiwa Vedastus Mathayo hapa mjini niwashukuru kwa kazi nzuri mnayoifanya ya kusukuma shughuli za maendeleo. " Changamoto nilizosikia ntazifikisha moja kwa moja kwa mheshimiwa Rais na naamini zitafanyiwa kazi",amesema Amesema kikubwa ni kuendelea kumuombea Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ili ...

Waziri Kassim Majaliwa akizungumza na mkuu wa wilaya Temeke Sixtus Mapunda

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Sixtus Mapunda, wakati alipowasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Octoba 01, 2024. Waziri Mkuu alitokea New York nchini Marekani, ambapo alimwakilisha Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa 79 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA79).

Balozi Yakubu na Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya uigizaji mchele comoro wateta

Balozi wa Tanzania nchini Comoro Mhe. Saidi Yakubu amekutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Uagizaji Mchele nchini Comoro, Moussa Hamada ambapo wamezungumzia namna bora ya kuongeza uagizaji wa bidhaa hiyo toka Tanzania. Balozi Yakubu akimkaribisha Ubalozini hapo jijini Moroni alimueleza kuwa Tanzania yafaa iwe ndio chaguo la kwanza kuagiza bidhaa hiyo kwa kuzingatia ukaribu wa kijiografia, ubora wa mchele wa Tanzania, urahisi wa upatikanaji na pia idadi kubwa ya mavuno inayoongezeka kila mwaka nchini humo. Balozi Yakubu alimueleza Mkurugenzi huyo kuwa makongamano ya hivi karibuni yamebaini kuwa kuna uhitaji mkubwa na changamoto za kufanyiwa kazi baina ya Mamlaka yake yenye dhamana ya kuagiza mchele nje ya Comoro na wadau wa nje na kikao hicho kijadili namna bora ya kutatua changamoto tajwa. Kwa upande, Bwana Moussa Hamada alimueleza Balozi Yakubu kuwa ni wakati muafaka kujadili kutokana na umuhimu wa bidhaa hiyo ambayo ndio chakula kikuu cha Comoro na kuarifu kuwa mahitaji ni tak...

Billion Mia tatu kugharamia ujenzi wa kongani ya viwanda vya kuchakata mazao mikoa ya kusini

 Na NIRC,Mtwara SERIKALI imesema iwe jua ama mvua itajenga Kongani ya viwanda vya kuchakata mazao ya mikoa ya kusini kwa gharama ya zaidi ya sh. Bilioni 300. Akizungumza katika mwendelezo wa ziara yake mkoani Mtwara,Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amesema kuwa Kongani ya viwanda vya kuchakata mazao ya mikoa ya kusini itajengwa eneo la Maranje Mjini Nanyamba mkoani Mtwara.  Amesema eneo la mradi lina jumla ya  ekari 1,572,ambapo eneo linaloendelezwa kwa sasa ni ekari 354 na ekari 1,218 zilizobaki zitasafishwa na kuwekewa fensi mwezi  ujao. Waziri Bashe ameeleza kuwa, Kongani hiyo ya viwanda ndio suluhisho la changamoto walizonazo wakulima wa mikoa hiyo. “Wapo watu walisema ni ndoto haitawezekana leo nawaambia Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan ni msikivu na mtendaji, ameamua iwe jua iwe mvua kongani itajengwa hapa na itahusisha viwanda mbali mbali vya kuchakata korosho, ufuta, mbaazi na mengine,”amesema Waziri Bashe Amesema Serikali imeanza hatua za awali za ujenzi wa ...

Serikali yapongeza kasi na usimamizi wa miradi ya maendeleo mkoani mara

Na Shomari Binda-Musoma Serikali imepongeza kasi na usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa mkoani Mara ikiwemo ya elimu,afya,maji na miundombinu. Pongezi hizo zimetolewa leo oktoba mosi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora George Simbachawene katika siku ya kwanza ya ziara yake ya siku 4 mkoani Mara. Akizungumza na watumishi kwenye ukumbi wa uwekezaji uliopo ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mara kabla ya kutembelea miradi iliyopo manispaa ya Musoma na Musoma vijijini amesema amesikia taarifa na kutambu kinachofanyika. Amesema serikali imekuwa ikileta fedha nyingi mkoani Mara kwaajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali na usimamizi mzuri uliopo wa fedha hizo kazi zinafanyika. Simbachawene amesema ipo miradi ya shule mpya ambayo ililetewa fedha na imekamilika na wanafunzi wameingia madarasani na kupata elimu. Amesema sio miradi ya elimu pekee bali kwenye sekta ya afy,maji na miundombinu imeletewa fedha na serikali na imefanyika vizuri. " Nikushukuru sana ...

Waziri Bashe Aitaka Tari Kuongeza Tafiti Mbegu za Asili

Na Elizabeth Cornely  WAZIRI wa Kilimo, Hussein Bashe, ameitaka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) kuongeza zaidi tafiti na uzalishaji wa mbegu za asili ikiwamo  kuwajengea uwezo zaidi watafiti wake kupitia vyuo vya ndani na nje ya nchi.  Bashe ametoa agizo hilo kupitia kwa Mkurugenzi Mkuu wa TARI, Dk. Thomas Bwana wakati wa ziara yake katika Kituo cha Utafiti cha TARI - Naliendele, mkoani Mtwara.  Katika ziara hiyo, Bashe alikagua  na kupata taarifa kutoka kwa watafiti kuhusu tafiti za mbegu za korosho, ufuta, karanga, njugu na mboga mboga. “Naelekeza pia nyaraka za kuanzisha mfuko wa kufanya tafiti za kilimo ‘agricultural research fund’ na kanuni zake ziandaliwe ili kuiwezesha TARI kutunza rasilimali fedha zitakazotokana na makato ya mazao kwa lengo la kuwezesha uendelezaji wa tafiti za kilimo nchini,” amesema Bashe.  Bashe ametolea mfano wa makusanyo yanayotokana na makato kwenye mauzo ya zao la Korosho ambapo kwa Mikoa ya Mtwara na Lindi ni Sh...