Na Mwandishi Wetu BODI ya Huduma za Maktaba Tanzania (TLSB), imeandaa mkutano wa waandishi na wachapishaji wa vitabu kuhusu Sheria ya amana kwenye maktaba mtandao wa taifa na ununuzi wa vitabu kwa ukuzaji wa soko la ndani utakaofanyika kesho. Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya (TLSB), Profesa Rwekaza Mukandara. Mkurugenzi Mkuu wa (TLSB), Dk. Mboni Ruzegea, alisema jana kuwa mkutano huo utafanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa TLSB Maktaba Kuu ya Taifa na kwamba lengo ni kujadili kwa pamoja utekelezaji wa sheria ya amana katika mfumo wa maktaba mtandao wa taifa na ununuzi wa vitabu kutoka kwa waandishi na wachapishaji wa ndani. Alisema TLSB iliyoanzishwa kwa Sheria ya mwaka 1975 inawapa mamlaka ya kuendeleza masuala ya maktaba kwa kuhakikisha nchi inakuwa na vitabu vya kutosha kupitia maktaba. “Mkutano huu wa kesho unalenga tunachofanya kila siku kwa hiyo tunataka kuzungumza na wachapishaji na wazalishaji kuhusu ubora wa wanachozalish...
Marato tv - Sauti ya Jamii