☑️ Watumika kwenye ujenzi wa miradi mikubwa kama Bandari ya Tanga, Bomba la Mafuta EACOP 📍 Tanga, Tanzania Sekta ya Madini nchini inaendelea kushuhudia mageuzi ya kuongeza thamani madini yakiwemo ya ujenzi kama mchanga na kufungua fursa nyingine mpya kwa wachimbaji wadogo wa mchanga kupitia teknolojia bunifu za usindikaji. Katika mkoa wa Tanga, Kampuni ya Muwa Trading Tanzania Limited imewekeza kwenye Kiwanda cha kuosha na kusafisha mchanga kwa maji ili kuondoa udongo na uchafu mwingine kama mizizi, hatua ambayo imebadilisha kabisa mtazamo wa thamani ya rasilimali hiyo kwa miaka mingi. Kwa mkoa wa Tanga, unaojulikana kwa utajiri wa madini ya viwandani na ujenzi, mchanga safi unaopatikana baada ya kuoshwa sasa ni malighafi yenye thamani kubwa kwa viwanda vya saruji, miradi ya kimkakati ya Serikali ikiwemo Bandari ya Tanga na ujenzi wa Bomba la Mafuta la EACOP katika Kata ya Chongeleani. Teknolojia hiyo pia inaelezwa kutoa fursa kwa wachimbaji wadogo na wawekezaji kuongeza ma...
Marato tv - Sauti ya Jamii