Skip to main content

Posts

Showing posts from June 14, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

DKT.MWINYI: JUNI 17 NI SIKU YA MAPUMZIKO ZANZIBAR

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ametangaza kuwa Jumatano, Juni 17, 2026, itakuwa siku rasmi ya mapumziko Zanzibar kwa ajili ya kuukaribisha Mwaka Mpya wa Kiislamu wa 1448 Hijria. Akitoa tamko hilo leo Ikulu Zanzibar, Rais Dkt. Mwinyi amesema hatua hiyo ni utekelezaji wa uamuzi wa Serikali wa kuutambua Mwaka Mpya wa Kiislamu kama miongoni mwa siku muhimu zinazoadhimishwa Zanzibar. Amesema siku hiyo itawapa wananchi, hususan waumini wa dini ya Kiislamu, fursa ya kuukaribisha mwaka mpya kwa ibada, dua na matendo mema, pamoja na kumuomba Mwenyezi Mungu aendelee kuijaalia Zanzibar na Tanzania kwa ujumla amani, umoja na ustawi. Rais Dkt. Mwinyi amewahimiza wananchi kuutumia mwaka mpya wa Hijria kama kipindi cha kujitafakari, kuimarisha uchamungu, kusaidiana na kudumisha maadili mema yanayochangia kujenga jamii yenye mshikamano na maendeleo. Aidha, amezitaka taasisi za Serikali, taasisi binafsi, waajiri na wananchi wote kuzingatia tan...

SERIKALI YAPOKEA HOJA YA MBUNGE WA BUTIAMA KUHUSU MIKOPO YA ASILIMIA 10 KWA MAJIJI MAKUBWA

 Serikali imepokea na kuahidi kuifanyia kazi hoja ya kutathmini mfumo wa utoaji wa mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya ndani ya halmashauri kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, hususan katika majiji yenye uwezo mkubwa wa ukusanyaji wa mapato. Hoja hiyo iliwasilishwa Bungeni jijini Dodoma na Mbunge wa Jimbo la Butiama, Dkt. Charles Mahera, ambaye alitaka Serikali kutafakari uwezekano wa kufanya marekebisho ya mfumo huo ili kuzingatia tofauti za mapato kati ya majiji makubwa na halmashauri nyingine nchini. Dkt. Mahera amesema kuwa wakati halmashauri zote zinatenga asilimia 10 ya mapato yao ya ndani kwa ajili ya mikopo hiyo, baadhi ya majiji makubwa hukusanya mapato makubwa yanayofanya fedha zinazotengwa kufikia mabilioni ya shilingi.  Ameeleza kuwa hali hiyo inaweza kuibua haja ya kutafuta uwiano utakaowezesha sehemu ya fedha hizo kuelekezwa pia katika miradi ya maendeleo kama ujenzi wa barabara na miundombinu mingine muhimu. Akijibu swali hilo kwa niaba ya Serikali, Naibu...

RAIS DKT. MWINYI AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA UWANJA WA AFCON FUMBA

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ametembelea mradi wa Uwanja wa AFCON Fumba kwa ajili ya kukagua maendeleo ya ujenzi wake. Ziara hiyo ya ukaguzi imefanyika leo, tarehe 14 Juni 2026, ambapo Rais Dkt. Mwinyi ametembelea maeneo mbalimbali ya uwanja huo wa kisasa unaojengwa na Kampuni ya Orkun Group ya Uturuki unaotarajiwa kutumika katika Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2027. Rais Dkt. Mwinyi ameendelea na utaratibu wake wa kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.  Nchi tatu za Afrika Mashariki, Tanzania, Kenya na Uganda, zinatarajiwa kuandaa kwa pamoja Michuano ya AFCON 2027. Uwanja wa AFCON Fumba ni miongoni mwa viwanja vinavyotarajiwa kutumika katika michuano hiyo.