Skip to main content

Posts

Showing posts from November 24, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri wa Viwanda awaahidi neema wenye viwanda

  Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga ameahidi kuendeleza ushirikiano baina ya serikali na wenye viwanda kuhakikisha anatimiza ndoto za Rais Samia Suluhu Hassan za kuongeza idadi ya viwanda nchini. Aliyasema hayo jana wakati akizungumza na wanachama na viongozi wa Shirikisho la Wenye Viwanda nchini (CTI), alipowatembelea kwenye ofisi zao jijini Dar es Salaam kujua changamoto zinazowakabili na kuweka mikakati kuzitatua. Alisema CTI ni wadau wakubwa kwenye maendeleo ya viwanda na ndiyo sababu ameamua kuwatembelea siku za mwanzo baada ya kuingia ofisi akiwa Waziri wa Viwanda.   Alisema ameamua kuanza kutembelea shirikisho hilo kwa kuwa ni muhimu sana kwenye ustawi wa viwanda na linawafikia wadau  18,000  wa sekta hiyo ya viwanda. Waziri Kapinga alisema maono ya serikali ya awamu ya sita ni kuboresha uchumi wa viwanda kukuza ajira na kuendeleza kustawisha biashara na kukuza viwanda vya ndani. “Tumezungumza mengi na wenye viwanda na moja kubwa ...

Yaliyojili wakati wa ziara ya Waziri Mkuu Dkt Mwigulu Nchemba katika mkoa wa Dar-es-Salaam

_Katika ziara hiyo Mheshimiwa Dkt. Mwigulu amekagua miundombinu ya Umma pamoja na mali zilizoathiriwa na vurugu iliyotokea Oktoba 29, 2025._ ▪️Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameelekeza hakutakuwa na maadhimisho ya Sherehe za Uhuru Desemba 09 na badala yake fedha ambazo zilipaswa kutumika katika Sherehe hizo zitumike  katika kurekebisha Miundombinu iliyoharibika kutokana vurugu zilizotokea Oktoba 29, 2025. ▪️Wapatieni kazi wakandarasi wazawa, wanauwezo, hata kazi wanazopewa wageni, wakandarasi wazawa ndio wanafanya hizi kazi. ▪️Maeneo ambayo kazi inaweza kufanywa na mtanzania ifanywe na Mtanzania, hata maeneo ambayo biashara inaweza kufanya na mtanzania ifanywe na mtanzania, Tanzania ni ya Watanzania. ▪️Mfanyakazi yoyote mzembe na mlarushwa msimhamishe, mfukuzeni kazi, vijana wakitanzania ambao wanafanya kazi vizuri wako wengi ▪️Ninaungana na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kutoa pole kwa wote walioathirika na vurugu zilizotokea oktoba 29, 2025 ▪️Tumuunge mkono Rais na wajum...

Waziri mkuu atoa siku 10 miundombinu ya muda irejeshwe

_Asema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amefuta maadhimisho ya 09/12_ _Aagiza fedha zake zitumike kurejesha miundombinu iliyoharibika_ _Rais Samia aagiza Kanisa la Ufufuo na Uzima lifunguliwe_ WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba ametoa siku 10 kwa watendaji wa taasisi zinazohusika na usafiri wa mwendokasi jijini Dar es Salaam wakae na kuainisha maeneo ya kufanyiwa kazi kwa haraka ili kurejesha hali ya mpito wakati Serikali ikitafuta suluhisho la kudumu. “Wizara ya Ujenzi, TANROADS, DART, UDART, OWM-TAMISEMI, TANESCO na wadau wengine, kaeni kuanzia leo, husisheni mabenki rejesheni intaneti, umeme, mageti ya kukatia tiketi ili turejeshe hali ya mpito wakati tukitafuta suluhisho la kudumu,” amesema.   Waziri Mkuu ametoa wito huo leo jioni (Jumatatu, Novemba 24, 2025) wakati akizungumza na wakazi wa Dar es Salaam katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Mbezi, wilayani Ubungo, jijini humo. Alikuwa katika ziara ya siku moja ya kukagua miundombinu iliyoharibiwa na vurugu zilizotoke...

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linawashikilia wahamiaji haramu 14 raia wa Burundi

  Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linawashikilia wahamiaji haramu 14 raia wa Burundi waliokamatwa wakiwa wameingia nchini kinyume na sheria kwa kutumia usafiri wa magari mawili tofauti ya abilia. Taarifa ya kukamatwa kwa wahamiaji haramu hao imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, DCP Wilbrod Mutafungwa, Novemba 23, 2025 wilaya ya Sengerema wakati akizungumza na umma kupitia vyombo vya habari. Kwa mujibu wa Kamanda Mutafungwa, mafanikio ya kukamatwa kwa watuhumiwa hao yametokana na  ufuatiliaji wa mienendo ya kihalifu na uwekaji wa vizuizi barabarani: Katika Kijiji cha Busisi, Tarafa ya Sengerema, jumla ya wahamiaji haramu 13 walikamatwa tarehe 23.11.2025 majira ya 7.30 mchana wakiwa wanasafiri ndani ya gari aina ya Tata yenye usajiri T. 337 DYA, mali ya Chiza Francis Lugubi, mkazi wa Dodoma, linalofanya safari zake kati ya Kabanga (Ngara, Kagera) na Mwanza. Wakati wa kukamatwa, dereva wa gari hilo, aliyetambulika kwa jina la Jonas Richard, alifanikiwa kutoroka eneo la t...

Wanafunzi shule ya Kaizirege na Kemebos waomba vijana kudumisha amani

  Na Angela Sebastian  Bukoba  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari za Kaizirege na Kemebos zilizoko Manispaa ya Bukobamkoani Kagera, wamewaomba Watanzania hususani vijana kudumisha amani na utulivu na kutojihusisha na vurugu ili kuwawezesha wanafunzi kuepukana na wasiwasi na hofu hasa kipindi hiki ambacho wanafanya mitihani ya Taifa na ya kufunga mwaka. Walitoa ushauri huo jana katika risala zao zilizosomwa na Jovan Mwandala darasa la saba na Innocent Madaraka Nyerere wa kidato cha nne katika mahafali ya darasa la saba na kidato cha nne ya shule hizo yaliyofanyika kata ya Ijuganyondo huku wakiaonyesha  kusikitishwa na vitendo vya uvunjifu wa amani ambayo ni tunu ya Taifa letu. "Tunawaomba wazazi wetu,kaka zetu,dada zetu,Watanzania wote  kuendelea kudumisha amani na utulivu hari hiyo inatuondolea wasiwasi sisi na kutuongezea morali ya kusoma hasa wakati huu tunapoendelea na mitihani yetu ya Taifa ili tuweze kufanya vizuri katika mitihani yetu"alieleza Nyere...

Dkt. Mwigulu Akagua Miundombinu na Mali Zilizoharibiwa na Vurugu za Oktoba 29, 2025

Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba leo Novemba 24, 2025 amekagua miundombinu ya usafiri wa mwendo kasi pamoja na mali nyingine ikiwemo nyingine zilivyoharibiwa kutokana na  vurugu zilizotokea Oktoba 29, 2025 jijini Dar es Salaam. Maeneo yaliyokaguliwa ni pamoja na Kituo cha Mafuta cha Puma ilichopo kimara baruti, vituo vya mwendo kasi vya Kimara Korogwe na Kimara Mwisho pamoja na kituo cha Mafuta cha Rupees kilochopo Kimara Stop Over.