Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) imebaini wizi wa mita 103 za maji ndani ya kipindi cha miezi mitatu, huku ikionya kuwa vitendo hivyo vinaongeza changamoto katika uendeshaji wa huduma za maji na usafi wa mazingira jijini Dodoma. Mkurugenzi Mtendaji wa DUWASA, Mhandisi Aron Joseph, ameyasema hayo Oktoba 26, 2026, jijini Dodoma, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu changamoto mbalimbali zinazoikabili mamlaka hiyo, zikiwemo wizi wa mita za maji na mifuniko ya chemba za majitaka. Amesema wizi na uharibifu wa miundombinu ya maji na majitaka unaweza kuongeza gharama za uendeshaji wa mamlaka hiyo, pamoja na kuhatarisha usalama wa wananchi na kuathiri utoaji wa huduma kwa jamii. Aidha, Mhandisi Aron amesema takribani asilimia 70 ya wateja wa DUWASA wana mita za maji zilizofungwa ndani ya fensi za makazi yao, hali inayoweza kuleta changamoto katika usomaji wa mita kila mwezi na kurahisisha upatikanaji wa taarifa sahihi za matumizi ya maji. Katika hatua nying...
Marato tv - Sauti ya Jamii