Skip to main content

Posts

Showing posts from November 19, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri Kikwete akutana na Balozi wa Japan nchini

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Kikwete amekutana na kuzungumza na Balozi wa Japan nchini Tanzania. Balozi huyo ambaye pia ni Mwakilishi wa Japan katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Yusushi Misawa pamoja na ujumbe wake amepomtembelea waziri Kikwete katika Ofisi ya NSSF, Jijini Dar es Salaam. Katika kikao hicho, wamejadili mambo mbalimbali ikiwemo kuwezesha vijana wa Kitanzania nafasi za kujifunza kazi na kuimarisha mafunzo pamoja na kuongeza ujuzi.

Zahanati ya Nyasaungu Kuanza Kutoa Huduma za Afya Mwezi December 2024

Fresha Kinasa,  Mara. KIJIJI  cha Nyasaungu  chenye vitongoji vitano (5) kilichopo katika Wilaya ya Musoma Mkoani Mara  kinakamilisha ujenzi wa zahanati yake ambayo inatarajiwa kuanza kutoa Huduma za Afya kwa Wananchi  ifikapo Disemba 2024.   Hayo yamebainishwa kupitia taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo hilo Novemba 18, 2024.  Kikiwa ni  moja ya vijiji vitatu vya Kata ya Ifulifu ambapo  Vijiji vingine ni Kabegi na Kiemba ambavyo kila kimoja kina zahanati yake. Kufuatia hatua hiyo, ifikapo Disemba 2024, kila kijiji ndani ya Kata ya Ifulifu kitakuwa na zahanati yake. Hatua  ambayo imetajwa kuwa kubwa sana ya maendeleo kwenye Kata hiyo.  Zahanati hiyo ujenzi wake ulianza  kwa kutumia michango ya fedha kutoka kwa wanakijiji na Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo. Ambapo aliendesha Harambee mbili za kupata fedha za kuanza ujenzi wa zahanati hiyo na Wanakijiji wanachangia nguvukazi kwenye ujenz...

Waziri Mkuu amesema Serikali itaendelea Kuboresha Mazingira ya Uwekezaji Nchini

*Lengo ni kuwezesha sekta hiyo kuendelea kuongeza mchango katika ukuaji uchumi WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji wakubwa na wadogo kwenye sekta ya madini ili kuhakikisha wanaendesha shughuli zao kwa tija na kusaidia kukuza uchumi wao na wa Taifa kwa ujumla. Amesema lengo ni kuwezesha sekta hiyo inaendelea kuongeza mchango wake katika ukuaji wa uchumi wa nchi kwa kuhakikisha inachangia zaidi ya asilimia 10 katika pato la Taifa ifikapo 2025. “Hii ni pamoja na kuendelea kuboresha miundombinu ya umeme, barabara, reli, bandari na viwanja vya ndege ili kusaidia shughuli za madini kufanyika kwa tija na kwa gharama nafuu.“ Waziri Mkuu ameyasema hayo leo  (Jumanne, Novemba 19, 2024) alipomwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Kimataifa wa Madini na Uwekezaji Tanzania unaofanyika kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere, Dar es Salaam. Amesema lengo la mkutano huo ni pamoja na kuvut...

Balozi Yakubu anaendelea Kuimarisha Diplomasia Nchini Comoro

Balozi wa Tanzania nchini Comoro,Saidi Yakubu amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Umoja wa Visiwa vya Comoro,Mheshimiwa Azali Assoumani. Mheshimiwa Rais Azali amemkabidhi Balozi Yakubu ujumbe maalum kwenda kwa Rais Samia Suluhu Hassan na akielezwa kuridhishwa kwake na ushirikiano wa sekta za biashara na kijamii ulioko baina ya nchi hizo mbili. Rais Azali pia alimueleza Balozi Yakubu kuwa ameshakutana na Marais wa Tanzania Hayati Ali Hassan Mwinyi,Hayati Benjamin Mkapa,Jakaya Kikwete,John Magufuli na sasa Rais Samia Suluhu Hassan na wote wameonesha upendo mkubwa kwa Comoro na anafurahi sasa makampuni ya Tanzania yanakuja kuwekeza Comoro. Kwa upande wake Balozi Yakubu alishukuru kwa ushirikiano anaoupata toka kwa mamlaka mbali mbali za Comoro na kumueleza namna uwekezaji na biashara baina ya Tanzania na Comoro inavyoimarika katika siku za hivi karibuni.

Tarafa ya Mbarika yajivunia ongezeko la ufaulu kidato cha nne na darasa la saba

Tarafa ya Mbarika wilayani Misungwi Mkoani Mwanza imefanikiwa kutokomeza ufaulu wa Daraja sifuri katika Matokeo ya Mitihani ya Taifa ya kidato cha nne. Tarafa hiyo pia inajivunia ongezeko la ufaulu wa wahitimu wa elimu ya msingi kutoka asilimia 48 mwaka mwaka Jana hadi kufikia asilimia 72 mwaka huu. Mafanikio hayo yamefikiwa kufuatia ushirikiano uliopo baina ya wadau mbalimbali wa sekta ya elimu wakiwemo wazazi na walezi,walimu pamoja na viongozi wa ngazi zote pamoja na uwekezaji unaofanywa na serikali kwenye sekta ya elimu. Afisa Tarafa hiyo Cresensia Mwalongo amebainisha hayo wakati ziara ya kuzungumza na wanafunzi wa shule mbalimbali za sekondari zilizopo kwenye Tarafa hiyo ikiwemo Mbarika,Mnyeti,Ilujamate na Lubili. ‘’Tunazunguka kwa ajili ya kuzungumza na wanafunzi kuwatia moyo na kuwaonyesha hali ya Maisha ambayo iko nje ambapo kama wakifanya vibaya watakwenda kuishi namna gani,kwa hiyo tunawatia moyo na kuwahamasisha kuhakikisha wanajikita zaidi katika masomo na kuachana na mamb...