Skip to main content

Posts

Showing posts from April 15, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Uongozi Mpya wa ZBC wakutana na TCRA, Zanzibar

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dkt. Jabiri Bakari katika kikao kazi na wajumbe kutoka Tume ya Utangazaji Zanzibar (ZBC) wakiongozwa na Katibu Mtendaji mpya wa Tume hiyo Ndugu Hijji D. Shajak, tarehe 15 Aprili, 2025, katika ofisi za TCRA Zanzibar. Kikao hicho kimelenga kudumisha mashirikiano kati ya taasisi hizo mbili ili kuboresha Sekta ya Utangazaji. Mnamo Septemba 15, 2023, TCRA na ZBC zilisaini mkataba wa maboresho (MoU) ya makubaliano ya kuboresha usikivu wa vituo vya redio vya Zanzibar katika mikoa ya Dar es Salaam na Tanga, na usikivu mzuri wa redio za mikoa  hiyo kwa upande wa Zanzibar. Makubaliano hayo pia yalilenga kuongeza ushirikiano katika matumizi ya rasilimali masafa kwa ufanisi.

Shughuli za Mazishi ya Mhandisi Gissima Nyamo-honga

 Matukio mbalimbali katika shughuli za Mazishi ya aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga. Mazishi hayo yanafanyika nyumbani kwake eneo la Migungani, Bunda Mkoani Mara leo tarehe 16 Aprili, 2025.

Bodi Mpya NEMC Yazinduliwa na Kutakiwa Kuanza na Mifuko ya Plastiki

Na  Mwandishi Wetu, Dodoma WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) ameiagiza Bodi mpya ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kushughulikia changamoto ya ukuaji wa haraka wa miji (urbanization) ili kuwe na mipango bora ya matumizi ya ardhi. Waziri Masauni aliyasema hayo jana jijini Dodoma wakati akizundua bodi ya tisa ya NEMC itakayoongozwa na Mkuu wa Mkoa mstaafu, Mhandisi Mwanasha Tumbo. Alisema miji inakua kwa kasi bila mipango bora ya matumizi ya ardhi  hali inayosababisha msongamano, uchafuzi wa mazingira, ukosefu wa mifumo ya maji safi na taka na uharibifu wa vyanzo vya maji na kingo za mito na bahari. Pia Waziri Masauni aliagiza  bodi hiyo kufanya vikao vyake kama mujibu wa sheria na iweke mikakati madhubuti ya kupata fedha za kujiendesha. “Nawaagiza mshirikiane kwa karibu na menejimenti ya Baraza ili kuleta matokeo yenye tija na msimamie vizuri Baraza ili kudhibiti uchafuzi wa mazingira nchini,” alisema. Aidha, Waziri...

Waziri Mkuu Aelekea Somanga

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa asubuhi Hii Aprili 16, 2025 amewasili eneo la Somanga kukagua Miundombinu ya barabara kuu ya Dar es Salaam-Lindi ambayo imeathiriwa na mvua zinazoendelea kunyesha nchini. Mheshimiwa Waziri Mkuu ameambatana na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Stegomena Tax pamoja na Waziri wa Ujenzi Abdallah Ulega.

Bodi mpya NEMC yazinduliwa na kutakiwa kuanza na.mifuko ya plastiki

Na  Mwandishi Wetu, Dodoma WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) ameiagiza Bodi mpya ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kushughulikia changamoto ya ukuaji wa haraka wa miji (urbanization) ili kuwe na mipango bora ya matumizi ya ardhi. Waziri Masauni aliyasema hayo jana jijini Dodoma wakati akizundua bodi ya tisa ya NEMC itakayoongozwa na Mkuu wa Mkoa mstaafu, Mhandisi Mwanasha Tumbo. Alisema miji inakua kwa kasi bila mipango bora ya matumizi ya ardhi  hali inayosababisha msongamano, uchafuzi wa mazingira, ukosefu wa mifumo ya maji safi na taka na uharibifu wa vyanzo vya maji na kingo za mito na bahari. Pia Waziri Masauni aliagiza  bodi hiyo kufanya vikao vyake kama mujibu wa sheria na iweke mikakati madhubuti ya kupata fedha za kujiendesha. “Nawaagiza mshirikiane kwa karibu na menejimenti ya Baraza ili kuleta matokeo yenye tija na msimamie vizuri Baraza ili kudhibiti uchafuzi wa mazingira nchini,” alisema. Aidha, Waziri...

Mbunge Mathayo Atoa Shukrani Kwa Rais Dkt.Samia Akichangia Bajeti Ofisi ya Waziri Mkuu

Na Shomari Binda-Musoma  MBUNGE wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo ametoa shukrani kwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi. Shukrani hizo amezitoa wakati akichangia Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwenye Kikao cha 5 cha Bunge la 12 Mkutano wa 19. Amesema kama mwakilishi wa wananchi wa jimbo la Musoma mjini anstoa shukrani nyingi kwa namna alivyowatendea mema kwenye kipindi cha uongozi wake Akizungumzia suala la elimu amesema shule mpya 4 zimejengwa huku kila mmoja ikipata fedha zaidi ya milioni 500 na leo watoto wanasoma bila tatizo. Amesema licha ya ujenzi wa shule mpya madara mengi mapya yameongezwa kwenye shule za zamani ambayo yamekuja kupunguza wanafunzi kujazana madarasani. Mbunge huyo amesema changamoto ndogo ni mahala pa wanafunzi kukaa na kwa sasa kwa kutu.ia fedha zake na wadau wa elimu yanatengenezwa madawati zaidi ya 3500 ili kumaliza changamoto hiyo. Kuhusu huduma za maji amesema upatikanaji ni asilimia 100 na ki...

Rais Samia Amwaga Bilioni 45 Kutatua Tatizo la Maji Jiji la Dodoma

▪️Mradi wa visima 10 Nzuguni A kuzalisha lita 20m kwa siku ▪️Visima zaidi kuchimbwa maeneo ya pembezoni ya Jiji kupunguza Mgao ▪️Waziri Aweso aweka kambi Dodoma kushughulikia suala la Maji ▪️Mbunge Mavunde apongeza jitihada za serikali kutatua kero ya maji Waziri wa Maji Mh. Jumaa Aweso amesema Rais Dkt. Samia S. Hassan ameelekeza utekelezaji wa miradi ya maji yenye thamani ya Bilioni 45 kutatua changamoto ya Maji Jijini Dodoma wakati ikisubiriwa utekelezaji wa Miradi ya kuleta maji kupitia Ziwa Victoria na mradi wa Bwawa la Farkwa. Waziri Aweso ameyasema hayo leo wakati akishuhudia utiaji wa saini wa mkataba wa mradi wa kusambaza maji kupitia visima vya maji vya Nzuguni A wenye thamani ya Tsh 5bn unaotarajiwa kuwanufaisha watu 123,095. “Mbunge wenu alileta maombi kwa Mh. Rais Samia juu ya uchimbwaji wa visima virefu wakati wa mkutano wa Mh. Rais pale Mpunguzi na sisi Wizara tukapata maelekezo ambayo tumeyafanyia kazi. Tunamshukuru Mh. Rais Samia kwa kulivalia njuga suala la maji hapa ...

Waziri Mkuu Amesema Wananchi Milioni 24 Wamenufaika na Trilioni 3.5 Kutoka Mifuko ya Uwezeshaji

 BUNGE la jamhuri ya Kuungano wa Tanzania aprili 15 mwaka 2025 limepitisha kwa kishindo makadirio ya bajeti ya ofisi ya waziri mkuu na taasisi zilizo chini yake katika kipindi cha mwaka wa fedha 2025/2026. Akihitimisha majadiliano ya makadirio ya mapato na matumizi ya fedha kwa mwaka 2025/2026,waziri mkuu Kassim Majaliwa amesema shilingi trilioni 3.5 zimetolewa na mifuko ya uwezeshaji wananchi kiuchumi iliyopo nchini kwa wanufaika zaidi ya milioni 24 ambapo kati yao, wanawake ni zaidi ya milioni 11 na wanaume ni milioni 13. “Uanzishwaji wa mifuko na programu za uwezeshaji wananchi unatokana na mahitaji ya kiuchumi kwa maendeleo ya nchi yetu. Mifuko iliyopo imeweza kutoa jumla ya shilingi trilioni 3.5 kwa wanufaika zaidi ya milioni 24,” amesema. Ameyasema hayo leo (Jumanne, Aprili 15, 2025) Bungeni jijini Dodoma, wakati akitoa hoja ya kuhitimisha mjadala wa bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Taasisi zake na Mfuko wa Bunge kwa mwaka 2025/2026.   Akielezea mambo yaliyofanyika ndani...