Skip to main content

Posts

Showing posts from September 28, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

PART TWO: KATIBA YASEMA NINI? SERIKALI NI NINI, VYOMBO VYA DOLA NI VYA NANI - WACHAMBUZI WAENDELEA KUMUUNGA MKONO COMRADE CHACHA

  Na Mwandishi Wetu Maalum Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 ndio inaojibu kila kitu kuhusu kauli iliyotolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Idara ya Oganaizesheni, Ndugu Paul Chacha, aliposema hadharani kuwa Chama Cha Mapinduzi ndicho mmiliki halali wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Jeshi la Polisi na Idara ya Usalama wa Taifa, na kuwa viongozi wote wa Serikali wamewekwa na CCM na sio na wananchi kama wengi wanavyodhani. Kauli hiyo imeibua mjadala mkali mitandaoni ambapo wapinzani wamejaribu kuipotosha kama ni kauli ya kichochezi. Lakini uchambuzi wa kina wa Katiba na misingi ya Sayansi ya Siasa unaonyesha kuwa Ndugu Chacha yupo sahihi kwa asilimia mia moja. Katiba yenyewe ndio inathibitisha hilo. Ibara ya 4 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano inasema kwa maneno yasiyopindika kuwa Jamhuri ya Muungano ni nchi ya kidemokrasia na ya kijamaa inayofuata mfumo wa vyama vingi, na kwamba mamlaka yote ya dola yatatumika na kudhibitiwa na vyombo vitatu tu ...

ARTICLE 119 CONNECTION: CCM CHAIRMAN IS COMMANDER-IN-CHIEF BY LAW, ANALYSTS SPEAK FROM CONSTITUTION

 By Our Special Correspondent The Constitution of the United Republic of Tanzania of 1977 and the Constitution of Chama Cha Mapinduzi of 1977 as amended have finally settled the heated debate sparked by Comrade Paul Chacha, Secretary of the National Executive Council for Organization. While opposition activists have been shouting on social media that state organs belong to the people, constitutional analysts have gone back to the books and found that Comrade Chacha is legally correct. The secret lies in the connection between Article 148 of the National Constitution and Article 119 of the CCM Constitution. Article 148 (1) of the Constitution of the United Republic states clearly: "The President shall be the Commander-in-Chief of all the Armed Forces of the United Republic." The question that many do not ask is, who is this President and where does he come from? He does not fall from the sky. The law that creates the President is found in the political party constitutions. CCM...

MAKAMU WA RAIS AAGIZA MILANGO IFUNGULIWE KWA VIJANA 10,000*

 ARUSHA, Agosti 28, 2026 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi ametoa wiki mbili kwa Wizara ya Mipango na Uwekezaji, Fedha na Kilimo kuandaa mpango wa mafunzo kwa Vitendo ambao utaanza kuchukua walau vijana 10,000 kupata uzoefu katika Taasisi, Mashirika ya Umma na Sekta binafsi ili kuandaa vijana watakaokuwa na uzoefu wa kujiajiri na kuajiriwa kama sehemu muhimu ya kutekeleza nguzo ya pili ya Dira ya Taifa 2050 na kusaidia maendeleo ya Nchi. Makamu wa Rais ametoa maelekezo hayo wakati alipomwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan, kwenye ufunguzi wa Kikao Kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Mashirika ya Umma, kinachofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC). Amewataka Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Mashirika ya Umma kubadili namna taasisi hizo zinavyofanya kazi na kuwa injini ya mageuzi ya uchumi kuelekea Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, huku akielekeza kuanzishw...

CHUO CHA UHASIBU ARUSHA(IAA) CHANYAKUA TUZO CEOs FORUM 2026.

 Mwandishi wetu,Arusha Chuo Cha Uhasibu Arusha(IAA) kimejinyakulia tuzo ya mshindi wa kwanza katika kundi la taasisi za umma zisizo za kibiashara zinazofanya vizuri katika usimamizi na matumizi bora ya fedha(Best Financial Management Perfomance -Non-Commercial Entities). Tuzo hiyo imekabidhiwa kwa Mwenyekiti wa Baraza la upngozi IAA,Dkt Mwamini Tulli na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Deogratias Ndejembi katika kikao cha wenyeviti wa bodi na wakuu wa taasisi za umma(CEOs Forum) katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Arusha (AICC) jijini Arusha. Akizungumza na wanahabari mara baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo mkuu wa chuo hicho,Dr Eliaman Sedoyeka amesema kwamba mara baada ya maelekezo ya Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ya kuzitaka taasisi za umma zijipambanie katika makusanyo na matumizi Chuo chao kilianza kufanya jitihada za dhati kuhakikisha wanatimiza azma hiyo na sasa wanajivunia kwa kupiga hatua. Dkt Sedoyeka amesema kwamba wamenza kutekeleza maeleke...

JKCI YAONGOZA HUDUMA BORA, YATWAA TUZO CEO FORUM 2026

 TAASISI ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) imeibuka mshindi wa kwanza katika kundi la taasisi zinazofanya vizuri katika kuboresha huduma na kutoa huduma bora kwa jamii, katika Kikao Kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi, Mashirika ya Umma na Wakala za Serikali (CEO Forum 2026). Ushindi huo umetangazwa leo, Septemba 29, 2026, wakati wa kikao hicho kinachofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC), huku JKCI ikitambuliwa kwa hatua zake katika matumizi ya huduma za kidijitali, kuongeza kiwango cha kuridhika kwa wateja na ukuaji wa idadi ya wateja katika mwaka wa fedha 2024/2025. Tuzo hiyo imetolewa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius John Ndejembi, ikiwa ni sehemu ya kutambua taasisi zilizofanya vizuri katika kuboresha huduma na kuongeza thamani kwa jamii. Akizungumza baada ya kupokea tuzo hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Dkt. Peter Kisenge, amesema ushindi huo ni matokeo ya juhudi za pamoja za watumishi wa taasisi ...

CHACHA SOYA AUNGANA NA NMB KUWAJENGEA UELEWA WAFANYABIASHARA TARIME

MKURUGENZI wa Kampuni ya Soya One Limited, Chacha Soya, ameungana na Benki ya NMB katika kikao maalum kilichowakutanisha wafanyabiashara na wadau mbalimbali wa biashara kutoka Tarime, kwa ajili ya kujadili fursa za kifedha na namna huduma za benki zinavyoweza kuchochea ukuaji wa biashara. Kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa CMG Hotel, Tarime, ambapo washiriki wamepata fursa ya kufahamu bidhaa na huduma mbalimbali za kifedha zinazotolewa na NMB, pamoja na namna ya kuzitumia kwa ufanisi katika kuendesha na kukuza biashara zao. Chacha Soya ameshiriki kikao hicho akiwa ameongozana na Naibu Balozi Mkuu wa Kampuni ya Soya One Limited, Zaka Media, katika tukio lililowapa wafanyabiashara nafasi ya kujifunza, kuuliza maswali na kubadilishana uzoefu kuhusu changamoto na fursa zilizopo katika sekta ya biashara. Maafisa wa NMB wametoa elimu kuhusu matumizi sahihi ya huduma za kifedha, fursa za uwekezaji pamoja na huduma mbalimbali zinazoweza kuwawezesha wafanyabiashara kusimamia fedha zao na ...

TIRA Yang’ara; Yatunukiwa Tuzo ya Mshindi wa Pili kwa Matumizi Bora ya Fedha – Taasisi za Umma

  Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) leo Septemba 28, 2026, imetunukiwa tuzo ya mshindi wa pili katika kundi la Taasisi za Umma zisizo za Kibiashara zinazofanya vizuri katika usimamizi na matumizi bora ya fedha (Best Financial Management Performance – Non-Commercial Entities). Tuzo hiyo imekabidhiwa kwa Kamishna wa Bima, Dkt. Baghayo A. Saqware, na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, katika Kikao cha Wenyeviti wa Bodi na Wakuu wa Taasisi za Umma (CEOs Forum) kinachoendelea katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC), jijini Arusha. Tuzo hizo zimeandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina kwa lengo la kutambua Taasisi za Umma zinazofanya vizuri katika maeneo mbalimbali ya usimamizi na matumizi ya rasilimali za umma. Akieleza kuhusu kundi la Matumizi Bora ya Fedha, Msajili wa Hazina, Bw. Nehemiah Mchechu, amesema tathmini hiyo imezingatia ufanisi katika matumizi na ukusanyaji wa mapato, pamoja na hatua za kupunguza utegemezi ...

KATIBU MKUU WIZARA YA NISHATI NA MADINI ZANZIBAR ATEMBELEA BANDA LA GST KATIKA MAONYESHO YA 9 YA TEKNOLOJIA YA MADINI GEITA

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Zanzibar, Ndugu Joseph Kilangi, ametembelea banda la Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) katika Maonyesho ya 9 ya Kitaifa ya Teknolojia na Uwekezaji katika Sekta ya Madini yanayoendelea katika Viwanja vya Dkt. Samia Suluhu Hassan, Geita. Katika ziara hiyo, Ndugu Kilangi ameongozwa na Kamishna wa Madini nchini, Dkt. Abdulrahman Mwanga, ambaye amemueleza kuhusu majukumu, shughuli na huduma zinazotolewa na GST, hususan katika tafiti za kijiolojia na utafiti wa rasilimali madini nchini. Akiwa katika banda hilo, Ndugu Kilangi amepata fursa ya kuona kwa vitendo teknolojia, vifaa na mbinu mbalimbali zinazotumika katika utafiti na uchunguzi wa madini. Aidha, amefahamishwa kuhusu huduma zinazotolewa na GST kwa wachimbaji, wawekezaji pamoja na wadau wengine wa Sekta ya Madini. Ziara hiyo imefanyika wakati ambapo Maonyesho hayo ya 9 yanaendelea kuwakutanisha wadau mbalimbali wa Sekta ya Madini kutoka maeneo tofauti, kwa lengo la ...

GST YATOA ELIMU YA UCHUNGUZI SAMPULI ZA MADINI KWA WACHIMBAJI GEITA

 Na Wellu Mtaki, Geita Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini (GST) imeendelea kutoa elimu kwa wananchi na wadau wa sekta ya madini kuhusu huduma za uchunguzi wa sampuli za miamba, mawe, udongo na maji, hatua inayolenga kuwawezesha kupata taarifa sahihi za kisayansi kwa ajili ya utafiti na shughuli za uzalishaji wa madini. Akizungumza wakati wa Maonesho ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea mkoani Geita, Fundi Sanifu Mkuu kutoka GST, Gideon Nshange, alisema taasisi hiyo ina uwezo wa kufanya uchunguzi wa aina mbalimbali za sampuli za madini na kimazingira. Nshange alisema maabara ya GST hufanya uchunguzi wa madini mbalimbali, ikiwemo dhahabu, shaba, fedha na madini mengine ya msingi, sambamba na uchunguzi wa miamba, udongo na sampuli za maji zinazohusiana na mazingira. “Tunafanya sampuli za miamba, mawe na udongo, lakini pia tunafanya sampuli za maji kwa maana ya sampuli za kimazingira. Pia tunafanya tafiti za vitu mbalimbali, ikiwemo utafiti unaohusiana na dhahabu,” ...

TPDC YAWASOGEZEA WANANCHI ELIMU YA MAFUTA NA GESI KATIKA MAONESHO YA TEKNOLOJIA YA MADINI GEITA

Na. Wellu Mtaki , Dodoma  Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limeeleza kuwa ushiriki wake katika Maonesho ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika mkoani Geita unalenga kuwawezesha wananchi na wadau mbalimbali kupata elimu na uelewa mpana kuhusu sekta ya mafuta na gesi asilia nchini. Kupitia maonesho hayo, TPDC imeweka msisitizo katika kutoa taarifa sahihi kuhusu shughuli mbalimbali zinazohusiana na utafutaji, uchimbaji, uzalishaji na matumizi ya mafuta na gesi asilia, pamoja na fursa zinazopatikana katika sekta hiyo muhimu kwa maendeleo ya Taifa. Akizungumza katika maonesho hayo, Hassan Temba kutoka TPDC, amesema ushiriki wa shirika hilo ni sehemu ya juhudi za kuifikisha elimu ya mafuta na gesi asilia kwa wananchi kwa njia rahisi na inayoeleweka, huku akisisitiza umuhimu wa jamii kufahamu namna rasilimali hizo zinavyotafutwa, kugunduliwa na kuendelezwa. Amesema Tanzania imepiga hatua katika kugundua na kuendeleza rasilimali ya gesi asilia, hivyo wananchi wanapaswa kuwa n...

ENG. SAMAMBA ATOA MAELEKEZO KWA WAMILIKI WA MIGODI NA MAAFISA MADINI WAKAZI WA MIKOA

 _Katika kukabiliana na mvua kubwa za El Niño_ 🔶Aagiza maboresho ya taratibu za migodi, ukaguzi wa maduara, mabwawa ya tope sumu na maandalizi ya dharura 📍KAHAMA Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Eng. Yahya I. Samamba, amewaelekeza wachimbaji wadogo, wamiliki, mameneja na wakaguzi wa migodi nchini kuchukua hatua za haraka kujiandaa na kukabiliana na mvua kubwa zinazotarajiwa kunyesha kuanzia Oktoba hadi Desemba mwaka huu, ikiwemo kuongeza kasi ya ukaguzi wa maeneo ya uchimbaji (maduara), mabwawa ya kuhifadhia tope sumu na kuimarisha mipango ya dharura. Eng. Samamba ametoa maelekezo hayo leo, Septemba 28, 2026, wilayani Kahama Mkoani Shinyanga wakati akifungua mafunzo kwa wachimbaji wadogo wa madini kuhusu maandalizi ya kukabiliana na athari za mvua hizo, akisema tahadhari hiyo inazingatia taarifa za Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kuhusu uwezekano wa mvua kubwa kuliko wastani katika kipindi hicho. Amesema mvua hizo zinaweza kuathiri shughuli za uchimbaji na kusababisha madh...