Skip to main content

Posts

Showing posts from February 22, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Nyansaho Foundation Kwa Kushirikiana na Mbunge wa Serengeti Watoa Tabasamu Kwa Wanafunzi 361

TAASISI ya Nyansaho Foundation kwa kushirikiana na ofisi ya mbunge wa jimbo la Serengeti imekabidhi vifaa mbalimbali vya masomo kwa wanafunzi 361 vyenye thamani ya zaidi ya milioni 60. Wanafunzi hao ambao wamenufaika na msaada huo wametoka kata 30 za jimbo la Serengeti ambao walishindwa kuripoti katika shule zao za Sekondari walizopangiwa kwa kukosa mahitaji hayo muhimu. Akikabidhi Mahitaji hayo leo February 22,2026 Mbunge wa Jimbo la Serengeti Bi. Mary Daniel ambaye ni Mgeni Rasmi katika hafla hiyo amekabidhi Msaada huo zikiwemo Shati,Sketi,Suruali,viatu,counter Book, bokei la kalamu, Rimu za kuandikia na kusomea,Rula,Kiwi za viatu, brashi pamoja na Begi. Baada ya kukabidhi Mahitaji hayo Mhe. Mary Daniel amewasisitiza,wazazi, walezi pamoja na Wananchi Kwa ujumla kuwahamasiahana kuhakikisha wanafunzi wote wanaripoti shuleni ili waendelee na Masomo.  "lakini pia niwasisitize wananchi kwamba wasaidieni sana watoto wetu kutimiza ndoto zao kwani kufanya hivi mtawasaidia sana"....

Waziri Mkuu Aweka Jiwe la Msingi Ujenzi wa Hosteli Nelson Mandela

*Asifu maono ya Rais Dkt. Samia kuhimiza sayansi, atoa maagizo sita WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba ametoa wito kwa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Kampasi ya Tengeru ihakikishe inakuwa kitovu cha ubora wa kitaaluma na utafiti bunifu unaolenga kutatua changamoto halisi za dunia ya leo. Ametoa wito huo leo (Jumapili, Februari 22, 2026) wakati akizungumza na viongozi wa mkoa wa Arusha, wanachuo na wakazi wanaoishi jirani na taasisi hiyo waliofika kushuhudia uwekaji wa jiwe la msingi katika hafla iliyofanyika kwenye Kampasi ya Tengeru, wilayani Arumeru, mkoani Arusha.  “Tumeona tumeona chanjo ya samaki, tumeona mbolea inayozalishwa kwa kutumia mwani. Tumeona ndege nyuki ya kupanda mazao shambani, hii itaokoa muda wa unaotumika kupanda mazao. Hizi bunifu zote zinaundwa ili kurahisisha kazi kwani zinatatua mambo mengi kwenye shughuli za kila siku za maisha yetu,” amesema. Aidha, ameitaka taasisi hiyo ihakikishe mafunzo yatakayotolewa, yanazingatia zaidi uju...

Waziri Mkuu Apewa Heshima Kwa Kuvishwa Vazi la Tamaduni za Kimasai

 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Arusha, Thomas Ole Sabaya akimvalisha Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba, vazi la utamaduni wa kimasai ikiwa ni ishara ya kumvika hadhi ya Laigwanan ambaye ni kiongozi wa kimila wa jamii ya kimaasai leo tarehe 22 Februari, 2026 wakati akikaribishwa kwa ziara zake za kikazi zilizoanza rasmi leo mkoani humo.

Dkt. Mwigulu Aweka Jiwe la Msingi Hostel za Wanafunzi Chuo cha Nelson Mandela

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Februari 22, 2026 ameweka jiwe la msingi la  ujenzi wa mabweni ya wanafunzi katika Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela, Kampasi ya Tengeru, Mkoani Arusha. Mradi huo unaofadhiliwa kupitia bajeti ya maendeleo ya Serikali, unalenga kuongeza uwezo wa malazi ya wanafunzi kutoka 600 hadi 1,000.  Mradi huo unatekelezwa kwa awamu tatu, ambapo kila awamu inajumuisha ujenzi wa jengo moja la bweni, ikiwemo vyumba maalum kwa wanafunzi wa kike wenye watoto au mahitaji maalum Awamu ya kwanza ya ujenzi imepangwa kugharimu shilingi bilioni  6.10, hadi sasa fedha zilizotumika ni shilingi bilioni 4.74 na ujenzi umefikia takribani asilimia 80.

Heslb inavyoshirikiana na Wadau Kuwawezesha Wanafunzi Kujitegemea Kiuchumi

  Na: Dk. Reubeni Lumbagala, Tanga Elimu ni haki muhimu ya binadamu. Elimu ni nyenzo muhimu ya kumsaidia binadamu kumudu maisha yake. Kwa kutambua hilo, ndiyo maana wazazi na walezi wanapambana sana kusomesha watoto na vijana wao ili kuwawezesha kupata elimu bora ya kuwasaidia katika maisha yao na kutimiza ndoto zao za kimaendeleo walizonazo. Kazi kubwa na nzuri zimefanyika nchini katika kuboresha sekta ya elimu katika ngazi zote za elimu kuanzia elimu ya awali, msingi, sekondari, vyuo vya kati na vyuo vikuu Ili watoto na vijana wa Kitanzania waweze kupata elimu bora ya kuwasaidia maishani mwao. Mitaala ya ujifunzaji imeboreshwa ili kuwajengea wanafunzi umahiri wa kujitegemea pindi wanapohitimu ngazi mbalimbali za masomo yao. Ikumbukwe kuwa mabadiliko haya mazuri ya mitaala yamekuja kipindi hiki ambacho wahitimu wengi wana changamoto ya kukosa stadi na ujuzi stahiki wa kuwawezesha kuajiriwa au kujiajiri katika sekta mbalimbali. Ndiyo maana wengi tunapongeza mabadiliko haya ya mitaa...

Sido Mara na Ggf Yaja na Teknolijia ya Kuokoa Mitaji Kwa Wakulima wa Mbogamboga na Matunda

Na Mwandishi wetu Jovina Massano Musoma. Shirika la viwanda vidogo vidogo (SIDO) mkoani Mara kwa kushirikiana na shirika la Grain to Grow Foundation (GGF) watoa mbinu ya kutumia Kaushio jua kwa wakulima wa mbogamboga na matunda ili kuokoa mitaji yao. Akiongea na Mwandishi wetu meneja wa SIDO mkoani hapa Bi.Salome Mwasomola ameelezea namna bora ya kuongeza thamani  katika mazao ya mbogamboga na matunda kwa kusindika kupitia teknolojia ya nishati jua kwa kutumia kaushio hilo ambalo linaweza kukausha mazao hayo bila kuathiri viini lishe/ virutubisho vilivyomo. Ameongeza kuwa teknolojia hiyo ni rahisi kutumiwa na wakulima kwa kuwa inatumia jua na inapatikana kwa urahisi  pia inaweza kutumiwa popote hata nyumbani. Ifahamike kuwa utumiaji wa teknolojia hii ni njia mojawapo ya kuongeza thamani ya mazao  kwa wakulima na kuokoa mitaji ukizingatia  hata soko lake ni dogo kwa kuwa hakuna kiwanda cha kusindika mazao hayo mkoani hapa. Amefafanua kuwa lengo utoaji elimu hii kwa wa...