Na John Mapepele Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe.Mohamed Mchengerwa amezindua soko la kisasa la nyama choma la Kumbilamoto vingunguti, Ilala jijini Dar es Salaam na kushuhudia utiaji wa mikataba ya miradi 6 ya maendeleo yenye thamani ya shilingi bilioni 7.7 Mara baada ya kuzindua soko hilo ambalo limegharimu takribani shilingi milioni 727 amepongeza uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa kufanikisha mradi huo ambapo amezitaka Halmashauri nyingine kuiga mfano huo. Aidha, amefafanua kuwa soko hilo litakwenda kuwapatia ajira wananchi wengi huku akisisitiza kuendelea kulitunza ili lisiharibike kwenye kipindi kifupi. Mhe. Mchengerwa ameongeza kuwa kukamilika kwa soko hilo ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na kufafanua kuwa Serikali ya awamu ya sita tayari imekamilisha miradi mingi kama iilivyoahidi. Wakati huo huo Waziri Mchengerwa amezitaka Halmasha...
Marato tv - Sauti ya Jamii