Skip to main content

Posts

Showing posts from November 20, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri Mavunde awakaribisha Wawekezaji wa Madini kutoka Finland Kuwekeza Nchini Tanzania

▪️Ampongeza Rais Samia kwa kuboresha mazingira ya Biashara nchini ▪️Wavutiwa na uwepo wa Rasilimali madini za kutosha ▪️Finland yaiahidi Tanzania ushirikiano kwenye utafiti wa madini 📍 Dar es Salaam Waziri wa Madini Mh. Anthony Mavunde amewakaribisha jumuiya ya wa Wafanyabiashara kutoka Nchini Finland kuwekeza kwenye sekta ya madini kwa kuwa nchi ya Tanzania imejaaliwa kuwa na rasilimali ya kutosha ya madini,mazingira ya uwekezaji rafiki na sera zinazotabirika. Waziri Mavunde ameyasema hayo jana  Masaki Jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa kifungua kinywa ulioandaliwa na Ubalozi wa Finland nchini kwa lengo la kuwakutanisha wafanyabiashara wa Madini kutoka Finland na Wizara ya Madini ili kubaini maeneo ya ushirikiano na fursa za kiuchumi zilizopo sekta ya madini nchini Tanzania. Akizungumza katika hafla hiyo Balozi wa Finland nchini Tanzania Mh. Theresa Zitting amesema Tanzania na Finland ni nchi zenye ushirikiano mkubwa kwenye masuala ya kiuchumi na hivyo ni wakatinmuafaka sa...

Waziri Mkuu Mgeni rasmi Mkutano wa pamoja wa Mawaziri na Viongozi wa WHO

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Novemba 21, 2024 ni mgeni rasmi katika mkutano wa pamoja wa Mawaziri  na Viongozi wa juu wa Shirika la Afya Duniani kuhusu hali ya Utekelezaji wa Afya kwa Wote na Utayari wa Kukabiliana na Dharura nchini. Mkutano huo ambao unafanyika katika Hotel ya Hyatt Jijini Dar es Salaam ni sehemu ya utekelezaji wa Azimio la Mkutano wa 73 wa Afya duniani uliofanyika mwaka 2020 kuhusu kutekelezaji kwa hiari mapitio shirikishi ya hali ya utekelezaji wa afya kwa wote na utayari dhidi ya dharura za kiafya kwa nchi wanachama wa Shirika la Afya Duniani (WHO).

Mhe. Sangu: Watumishi wa Umma Tumieni Mifumo ya Kidijitali Kuwasilisha Changamoto Zenu

Na. Hamida Ramadhan, Katavi  SERIKALI imewataka Watumishi wa Umma nchini kuwasilisha changamoto zao za  kiutumishi wakati wowote na mahali popote ili ziweze kufanyiwa kazi  lengo likiwa ni kumsaidia Mtumishi kutatuliwa changamoto zake pasipo kulazimika kusafiri kwenda jijini Dodoma.  Ametaja mifumo hiyo ya kidijitali  ikiwemo e-Mrejesho, Sema na Waziri wa Utumishi pamoja na njia ya kupiga simu ambapo hadi sasa njia hizo zimesaidia kuleta mageuzi makubwa katika uboreshaji wa utoaji wa  huduma bora kwa Wananchi wakiwemo Watumishi wa Umma.  Mhe. Sangu ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza na Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda, Mkoani Katavi, ikiwa ni muendelezo wa kliniki ya kimkakati ya kusikiliza na kutafuta ufumbuzi wa changamoto mbalimbali zinazowakabili  Watumishi hao. Akifafanua mfumo wa kidijitali wa "Sema na Waziri wa Utumishi" Mhe. Sangu amesema mfumo huo  unamsaidia Mtumishi wa Umma kuwasiliana ana kwa ana na Waz...

Mhe. Sangu Aridhishwa na Usimamizi wa Fedha za TASAF - Rukwa

Na Hamida Ramadhan-Rukwa  NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu ameupongeza Mkoa wa Rukwa kwa usimamizi bora wa fedha za Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kupitia utekelezaji wa Mpango wa Kuzinusuru Kaya Maskini nchini kwa kufuatilia kwa ukaribu utekelezaji wa miradi inayowanufaisha walengwa wa mfuko huo. Mhe. Sangu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kwela Mkoani humo ametoa pongezi hizo leo kwa nyakati tofauti wakati alipotembelea kukagua  baadhi ya miradi inayotekelezwa na TASAF    katika Wilaya Nkasi na Kalambo. Ameitaja miradi hiyo inayotekelezwa na TASAF ikiwemo ujenzi wa kisima cha maji katika wilaya ya Nkasi pamoja na uanzishwaji wa shamba la miti ya mbao wilayani Kalambo.  Akizungumzia suala la ujenzi wa kisima hicho uliogharimu zaidi ya Sh. Milioni tatu (3) hadi kukamilika kwake  kimekuwa msaada mkubwa kwa kuhudumia zaidi ya kaya 200 katika Kijiji cha Kantawa.  Kufuatia hatua hiyo Mhe. Sa...

Chande atoa Maagizo kwa Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini

  Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb) amelitaka Baraza la 13 la Uongozi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini kuwa walinzi wa dira, dhima na mwelekeo wa Chuo. Alitoa rai hiyo jijini Dodoma wakati akizundua Baraza hilo la Uongozi uliofanyika katika Chuo cha Mipango ya Maendeleo vijijini, Kampasi ya Dodoma. Mhe. Chande alisema kuwa kulingana na Sheria ya Chuo, Baraza la Uongozi wa Chuo linapaswa kuhakikisha kuwa dira, dhima, na mwelekeo wa taasisi vinasimamiwa kwa weledi na uwajibikaji mkubwa ili kufikia matokeo chanya ya taasisi kwa manufaa ya wadau wote wa ndani na wa nje. “Kufanya kazi kwa bidii, maarifa na umakini na hali ya juu kunakiwezesha Chuo kutoa huduma bora inayokidhi matakwa ya wadau wetu na hasa katika zama hizi za kidijiti. Mnatakiwa kuwekeza kwenye kujitoa, kujituma, na kutumia muda mwingi kutafuta ufumbuzi wa changamoto zinazowasilishwa kwenu na menejimenti”, alisema Mhe. Chande. Mhe. Chande alilitaka Baraza la uongozi wa Chuo kuishauri Menejimen...

Kizza Besigye afikishwa mahakamani Uganda

 Kizza Besigye amefikishwa katika mahakama ya kijeshi ya Makindye, nchini Uganda. Wanachama wa chama cha Forum for Democratic Change (FDC ) leo walipiga kambi katika Mahakama hiyo, wakisubiri kufikishwa kwake mahakamani, gazeti la Monitor limeripoti. Kiongozi huyo mkongwe wa upinzani aliripotiwa kutoweka mwishoni mwa juma katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi alikokuwa ameenda kwa shughuli binafsi. Siku ya Jumatano, vyanzo vilisema Dk Besigye, mmoja wa wanasiasa waliokamatwa mara nyingi zaidi katika historia ya hivi karibuni ya Uganda, alirejeshwa nchini na alikuwa akishikiliwa katika kambi ya kijeshi ya Makindye na alitakiwa kufikishwa mahakamani. Kutoweka kwa Besigye kulifuatia kukamatwa Julai 23 kwa wanaharakati 36 wa Uganda wanaohusishwa naye huko Kisumu, mji wa kando ya ziwa nchini Kenya karibu na mpaka. Wanaharakati hao wa kisiasa walitekwa nyara na kusafirishwa hadi Uganda ambako walifunguliwa mashtaka ya uhaini na kupelekwa katika Gereza la Kitalya. Wanaharakati hao ambao walia...

Hapi awataka wana Kagera Kutofanya Mzaha na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Na Angela Sebastian; Bukoba  Mjumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)Taifa na katibu mkuu wa jumuiya ya Wazazi Ally Hapi amewataka wanachama wa CCM mkoa wa Kagera kutofanya mzaha katika uchaguzi wa Serikali za mitaa kwani viongozi wa mitaa ndio msingi maendeleo ya Watanzania. Hapi alisema hayo leo Nov 20-2024 wakati wa uzinduzi wa kampeni za chama hicho za kuwatambulisha wagombea wa vijijini 662,mitaa 66 na vitongoji 3664 wa mkoa wa Kagera wanaotarajiwa kushiriki kinyanganyilo cha uchaguzi wa Serikali za mitaa  Novemba 27 mwaka huu. "Hawa ndio watu wa mwanzo kusimamia ulinzi na usalama katika maeneo yetu ya mitaa na vitongoji,hawa ndio wa kwanza kuwapelekea shida zetu,ndio viongozi wakusimamia maendeleo yetu mita hivyo tusifanye mzaha wala ushabiki katika uchaguzi huu tuchague viongozi wenye uwezo wa kuongoza ambao wanatokana CCM"alisema  Hapi  Uchaguzi huu ni muhimi sana ata jikoni hauwezi kupika na figa moja hivyo kuanzia ngazi za tawi...

Dkt. Nchimbi amesema Ccm ina Mtaji wa Imani ya Watanzania

_Azindua kampeni Mwanza akitamba na takwimu za kura za uhakika_ _Awasihi wanaCCM kila mmoja kutafuta kura 10 kwa ajili ya ushindi wa kishindo_ _Ahamasisha kampeni za nyumba kwa nyumba na mtu kwa mtu, isiachwe kura hata moja, wakiwemo wapinzani_ _Awataka washindi kuwatumikia Watanzania kwa kupinga dhuluma na rushwa_ Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, amesema CCM inaingia kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa kikiwa na imani kubwa ya Watanzania kutokana na uimara wa chama na uongozi wa Mwenyekiti wake, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan. Amesema kuwa uimara wa CCM unatokana na wingi na umakini wa wanachama wake, akitoa takwimu jinsi wanachama wapatao milioni 8 wa CCM walivyojitokeza kupiga kura wakati wa mchakato wa ndani ya chama hicho kupata wagombea wa nafasi mbalimbali kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Balozi Nchimbi amesema mtaji wa imani ya Watanzania, utumishi wa CCM kupitia sera zake, na uongozi makini unakipatia chama hicho uhakika wa ushi...