Skip to main content

Posts

Showing posts from September 27, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Serikali imesema sera ya elimu ya lazima kwa miaka kumi darasani kutekelezwa mwaka 2027/28

  Na Mwandishi Wetu, Ruvuma Serikali imesema utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Toleo la Mwaka 2023 juu elimu ya lazima kuwa ya miaka 10 utaanza Mwaka 2027/28 ambapo wahitimu wa elimu ya msingi ya miaka 6 watakutana na wahitimu wa mwisho wa elimu ya msingi ya miaka saba na wataanza kidato cha  kwanza kwa pamoja. Hayo yameelezwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda Mkoani Ruvuma  jana  wakati akiwasilisha mada juu ya Sera Mpya ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Toleo 2023 kwa wajumbe wa Baraza Kuu la Umoj wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi, Wenyeviti na Makatibu wa Wilaya  (UWT) ambapo alisisitiza kuwa ifikapo Mwaka 2027/28 Mtoto ambaye hatakaa shuleni kwa miaka 10 hatua za kisheria zitachukuliwa kwa mzazi au mlezi. Waziri Mkenda ameongeza kuwa ili kuhakikisha utekelezaji wa sera mpya unakwenda sawa bila kikwazo chochote, Serikali inaendelea na kufanya mapitio ya Sharia ya Elimu, Sura ya 353 ili iendane na mabadiliko yali...

Kituo Jumuishi Temeke kinabeba dhamira ya Rais katika uboreshaji wa huduma za haki nchini

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Sagini Septemba 26, 2024 alitembelea katika Kituo Jumuishi cha Masuala ya Familia Temeke, ambapo katika ziara hiyo Naibu Waziri amejionea na  kufurahishwa na huduma jumuishi  zitolewazo kituoni hapo.  Akizungumza katika ziara hiyo, Mhe. Sagini amesema kuwa  Sekta ya Mahakama Nchini  imeendelea kupiga hatua kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali katika kuboresha huduma za utoji haki katika Vituo Jumuishi vya Mahakama Nchini.  "Uwepo  wa  Kituo hiki hapa Temeke unaonesha dhamira ya dhati aliyonayo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha jamii inapatiwa ufumbuzi wa matatizo mbalimbali na Haki inatendeka kwa kila mtu na kwa wakati. Niwapongeze pia kwa kuwa katika kipindi cha miaka mitatu tangu kuanzishwa kwa Kituo hiki mmeweza kufanya tathmini na kupata taarifa halisi kuwa malengo ya kuanzishwa kwa Kituo hiki yamefikiwa kwa asilimia mia moja hii ni ha...

Kikwete akagua maandalizi ya kilele cha mbio za mwenge wa uhuru mjini mwanza

-Akutana na makundi mbalimbali kuhamasisha shamra hizo -Awatembelea Vijana wa Halaiki. Waziri wa Kazi,Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Mh. Ridhiwani Kikwete amefanya ziara ya siku mbili mkoani Mwanza ikiwa ni kukagua maandalizi ya Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru zinazotaraji kuhitimishwa mkoani hapo Tarehe 14 Oktoba, 2024 katika uwanja wa CCM kirumba jijini hapo.  Akiwa mjini Mwanza ,Waziri Kikwete amepata nafasi ya kukutana na makundi mbalimbali ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha ushiriki wa kilele hicho na wiki ya Vijana ambayo inataraji kuanza tarehe 8 hadi 13 Oktoba 2024 katika viwanja vya furahisha.  Waziri Kikwete ambaye alikutana na makundi ya Vijana Wasanii katika fani mbalimbali na baadae kukutana na Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na Walimu wa sekondari na vyuo toka wilaya zote za Mkoa huo, alitumia nafasi hiyo kuwahimiza kujitokeza kwa wingi na kuhakikisha kuwa wanaulaki Mwenge kwa shamra nyingi na kushiriki kilele cha wiki ya vijana.  Baada ya mikutano hiyo ya Wadau...

Mbunge Ghati ateta na katibu mkuu wa ccm Taifa

 Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara Mhe.Ghati Zephania Chomete, Leo tarehe 27 Septemba 2024 amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa CCM Taifa Balozi Dkt.Emmanuel John Nchimbi.  Mhe.Ghati ametumia fursa hiyo kumpongeza Balozi Dkt.Nchimbi kwa namna anavyosimamia shughuli za Chama, Jumuiya na Idara zake kama Mtendaji Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi kwa ngazi ya Taifa.  Mhe.Ghati amemhakikishia Dkt.Nchimbi kuwa wanawake na wananchi Mkoani Mara wataendelea kumuunga mkono Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kumpa kura za ndio na za kishindo katika uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika novemba mwaka huu pamoja na uchaguzi mkuu wa mwakani kutokana na Utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo. 

Mkuu wa Majeshi ya ulinzi Tanzania atembelea Msumbiji

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Jenerali Jacob John Mkunda amefanya Ziara ya Kikazi nchini Msumbiji kuanzia tarehe 23 hadi 27 Septemba, 2024. Wakati wa ziara hiyo, pamoja na masuala mengine, Jenerali Mkunda alitembelea Ubalozi wa Tanzania uliopo Jijini Maputo tarehe 24 Septemba, 2024 na tarehe 25 Septemba, 2024 alishiriki kwenye Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi la Msumbiji.  Wakati wa Maadhimisho hayo, Jenerali Mkunda alitunukiwa na Mhe. Filipe Jancito Nyusi, Rais wa Jamhuri ya Msumbiji, Nishani Maalum ya Heshima kwa kutambua na kuheshimu mchango wa Tanzania katika ukombozi na ustawi wa amani na usalama nchini Msumbiji. Vilevile, tarehe 26 Septemba 2024, Jenerali Mkunda alikutana na mwenyeji wake, Admiral Joaquim Rivas Mangrasse, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Msumbiji na kuzungumza masuala mbalimbali ya Ushirikiano kati ya JWTZ na Jeshi la Ulinzi la Msumbiji (FADM) ambapo Viongozi hao walikubaliana na kusisitiza juu ya haja ya kuendelea kushirikiana kwa ukaribu kwa ma...

Waziri mkuu anadi sababu 10 za kuwekeza Tanzania

Ni katika jopo la wafanyabiashara mahiri wa Marekani Waziri Kassim Majaliwa ametoa sababu 10 zinazoweza kumfaya mfanyabiashara yeyote kutoka Marekani avutiwe kuwekeza nchini. Amezitaja sababu hizo kuwa ni mahusiano imara, sera thabiti za kiuchumi, mazingira ya amani na uthabiti, nafasi ya kijiografia ya nchi, uwepo wa masoko makubwa, uwepo wa nguvu kazi ya vijana na miundombinu ya kidijitali. Nyingine ni miundombinu ya kisasa ya mawasiliano, uchumi mpana na utawala bora na mfumo wa kodi wa haki. Akifungua jukwaa la biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Marekani lililofanyika jana jana (Septemba 26, 2024) katika makao makuu ya ofisi za CITI, jijini New York, Marekani, Waziri Mkuu aliwaeleza wafanyabiashara hao kwamba Tanzania ni mahali sahihi pa kuwekeza mitaji yao na pana mvuto ambao hakuna mwekezaji anaweza kuukwepa. Akielezea kuhusu uimara wa mahusiano, Waziri Mkuu alisema uhusiano wa muda mrefu baina ya nchi hizo mbili ambao umedumu kwa zaidi ya nusu karne, unathibitisha mazingi...

Mikopo ya kausha damu yaiumiza kichwa serikali

  Wanawake wilayani misungwi mkoani mwanza wametakiwa kuacha kukopa fedha kwenye taasisi zisizo rasmi ili kuepuka kuingia kwenye migogoro wakati wa kurejesha mikopo hiyo. Akizindua Jukwaa la uwezeshaji wa wanawake kiuchumi,Mkuu wa wilaya hiyo Johari Samizi amesema kuwa mikopo inayotolewa na Taasisi zisizo rasmi imekuwa ikiwaumiza wananchi  kutokana na riba kubwa inayowekwa na wakopeshaji ambao hawazingatii taratibu za mikopo. “Kuna Taasisi rasmi za fedha,tuache kwenda kukopa mikopo kausha damu,kuna mikopo ina majina mpaka unaogopa,yaani ukisikia mkopo mpaka apetitle ya kula inaisha,kuna mkopo unaitwa ngumu kumeza,Jina lenyewe linahataraisha usalama wako,mkopo kausha damu,damu ikikauka kuna uhai”alisema Samizi na kuongeza kuwa “Mama zangu nawaomba sana,Mikopo hii inasambaratisha familia,ndoa zimevunjika na kuharibika kwa mahusiano,familia zinasambaratika kisa mkopo kausha damu,ndo maana nawaambia kopeni kwenye taasisi rasmi za kifedha,mkishindwa taasisi rasmi dirisha likifungul...