Skip to main content

Posts

Showing posts from November 18, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Tarura Yaboresha Miundombinu Kukabiliana Na Athari Za Mabadiliko Ya Tabianchi

   Belem, Brazil Serikali kupitia Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) inaendelea kuimarisha usimamizi wa mazingira kwa kujenga miundombinu thabiti ikiwemo madaraja ili kukabiliana na athari za mafuriko yanayotokana na mabadiliko ya tabianchi. Hayo yameelezwa na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu–TAMISEMI (Miundombinu), Mhandisi Rogatus Mativila katika Mkutano wa 30 wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP 30) unaoendelea jijini Belem, Brazil. Mhandisi Mativila amesema Mpango wa ‘SCALE’ (Scaling up Locally Led Climate Actions) unaoanza kutekelezwa kupitia fedha za mkopo nafuu kutoka Benki ya Dunia ni muhimu katika utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwa kuwa unahusisha jamii husika katika maeneo yao ili  kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.  Ameeleza kuwa mpango huo unatarajiwa kuwafikia watu takribani milioni 6.6 katika mamlaka 65 za Serikali za Mitaa zikiwemo 54 kutoka Tanzania Bara na 11 kutoka ...

National Institute of Transport joins hands with UDART to provide training opportunities for BRT bus drivers

By Prosper Makene The National Institute of Transport (NIT), in collaboration with the Dar Rapid Transit (UDART), has announced a special training opportunity for BRT bus drivers.  The training aims to equip drivers with advanced skills to operate BRT buses efficiently and safely, providing better services to passengers and enhancing road safety. The 10-day training program will run from November 24 to December 5, 2025, with a training fee of Tsh 150,000. Eligible candidates must possess a valid driving license class C, be between 25-50 years old, and have at least 3 years of driving experience. The primary objective of this training is to produce skilled drivers who can operate BRT buses effectively and safely while providing excellent customer service. This opportunity is ideal for those seeking to acquire modern bus driving skills and improve their employment prospects in Tanzania's transport sector. Successful trainees will be equipped to work on the BRT project and access empl...

NIT yashirikiana na UDART kutoa mafunzo kwa Madereva wa Mabasi ya mwendokasi

Na Prosper Makene Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kwa kushirikiana na Kampuni ya Mabasi Yaendayo Haraka (UDART) kimetangaza fursa ya mafunzo maalum kwa madereva wa mabasi ya Mwendo Kasi (BRT).  Mafunzo haya yanalenga kuwandaa madereva wenye ujuzi wa hali ya juu wa kuendesha mabasi ya BRT, ili kutoa huduma bora kwa abiria na kuimarisha usalama barabarani. Mafunzo haya ni ya siku kumi, kuanzia tarehe 24 Novemba hadi 5 Desemba 2025, na ada ya mafunzo imetangwa kuwa shilingi za Kitanzania 150,000. Madereva wanaotakiwa ni wale wenye sifa za msingi kama vile wenye leseni ya udereva Class C, umri wa kati ya miaka 25-50, na uzoefu wa miaka mitatu ya udereva. Lengo kuu la mafunzo haya ni kuandaa madereva ambao watakuwa na uwezo wa kuendesha mabasi ya BRT kwa ufanisi na usalama, huku wakitoa huduma bora kwa abiria. Mafunzo haya ni fursa muhimu kwa wale wanaotaka kujipatia ujuzi wa kuendesha mabasi ya kisasa na kuboresha nafasi zao za ajira katika sekta ya usafiri nchini Tanzania. Watak...

Watu 200 wafanyiwa uchunguzi wa kisukari bure hospitali ya Shifaa

Na Mwandishi Wetu ZAIDI ya watu 200 wamenufaika na uchunguzi wa kisukari bure uliofanywa na hospitali ya Shifaa ya Kinondoni jijijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya kisukari duniani Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Dk Emmanuel Maganga wakati akizungumza kuhusu uchunguzi wa maradhi ya kisukari yaliyofanywa bila malipo hospitalini hapo. Alisema ugonjwa wa kisukari usipotibiwa vizuri unaweza kusababisha matatizo ya figo, macho misuli  na watu wengine kupata vidonda visivyopona na kusababisha kukatwa baadhi ya viungo kuokoa uhai wao. Alisema kumekuwa na ongezeko kubwa la wagonjwa wanaosafisha figo Dialysis hali ambayo inasababishwa na wagonjwa wa kisukari  kushindwa kupata huduma sahihi na za kibingwa kwa wakati. “Haya yote ndiyo yamesababisha hospitali ya Shifaa kufungua kitengo ambacho matibabu yote yanayohusiana na kisukari yatapatikana sehemu moja kama lishe mazoezi, macho, na  ushauri wa kupunguza uzito ul...