Skip to main content

Posts

Showing posts from September 7, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Dk.Nchimbi Ndani ya Sumbawanga Vijijini,Rukwa Kuwahutubia Wananchi

MGOMBEA mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi akiwasili katika Uwanja wa Laela A,Sumbawanga Vijijini  kuwahutubia Wananchi  katika mkutano wa hadhara wa Kampeni  leo Jumatatu Septemba 8,2025. Dk.Nchimbi ameingia Mkoani Rukwa leo kuendelea na mikutano yake ya kampeni ya kutafuta kura za kishindo kwa Chama Cha Mapinduzi ( CCM) kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 29,2025.

Nsekela Amuomba Dkt Nchimbi Kusaidia Kutatua Tatizo la Nida

 Na Angela Sebastian; Kyerwa Mgombea ubunge jimbo la Kyerwa Khalid Mussa Nsekela amemuomba mgombea mwenza wa kiti cha Urais kupitia chama cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi kuwa chama hicho kitakaposhika dola tena kisaidie kutatua changamoto inayowakabili wananchi wa jimbo hilo ya kukosa vitambulisho vya Taifa(NIDA).  Nsekela ametoa ombi hilo baada ya Dk.Nchimbi kumnadi kwa kuwahakikishia wananchi kuwa mgombea huyo anafaa na atawaletea maendeleo kisha kumpatia nafasi ya kusalimia maelfu ya wananchi ambao walifulika katika mkutano wa mgombea mwenza uliofanyika leo katika viwanja vya stend ya mabasi Nkwenda wilayani Kyerwa. Nsekela amewaomba wananchi wa jimbo la Kyerwa itakapofika Oktoba 29 mwaka huu kupiga kura kwa wagombea wa chama cha mapinduzi CCM kupiga kura kwa ajili Rais, wabunge na madiwani. "Nashukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na mama yetu Dk.Samia amefanya na kutekeleza mengi sisi sote ni mashuhuda pia anaendelea kutuahidi mengi ambayo anakw...

Nirc Yaridhishwa na Kasi ya Ujenzi wa Skimu ya Makwale-Kyela

NA MWANDISHI WETU  Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC) kupitia Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji wa Miundombinu, Mhandisi Leopold Runji, imefanya ziara ya ukaguzi wa miradi ikiwemo ujenzi wa skimu ya Umwagiliaji Makwale, iliyopo Kyela mkoani Mbeya. Katika ziara hiyo Mhandisi Runji ameeleza kuridhishwa na kazi inayoendelea na kumtaka Mkandarasi anayetekeleza mradi huo kuongeza nguvu ili kukamilisha mradi kwa wakati.   Mhandisi Runji ameeleza kuwa mradi huo unagharimu kiasi cha shilingi bilioni 20.9 za kitanzania na utekelezaji wake umefikia asilimia 60.3, huku mkandarasi akiwa tayari amelipwa asilimia 50.8 ya malipo yake.  “Mradi huo unahusisha ujenzi wa banio, usafirishaji wa maji kupitia bomba lenye urefu wa kilomita 6.3, pamoja na mifereji mikuu na ya upili yenye zaidi ya kilomita 11. Aidha, kazi zilizokamilika ni pamoja na utandazaji na uungani wa Bomba kwa 5,454m (86.6%), Usakafiaji wa mfereji mkuu kwa kiwango cha zege kwa mita3150(63%) pamoja na Ujenzi wa...