Skip to main content

Posts

Showing posts from June 19, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

WANANCHI MSIHOFU KUTUMIA NISHATI YA UMEME KATIKA VYOMBO VYA USAFIRI -MD TWANGE

 📌Asema TANESCO inajenga vituo vya kuchajia vyombo hivyo nchi nzima 📌Aeleza mpango wa kusambaza majiko sanifu ya umeme takribani Mil 1 📌Awapongeza Wafanyakazi kwa ubunifu na jitihada za kuwahudumia wateja kwa ufanisi. Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Bw. Lazaro Twange, amewaondoa hofu wananchi kuhusu matumizi ya nishati ya umeme katika vyombo vya usafiri, akisema kuwa TANESCO imejipanga kujenga vituo vya kuchajia vyombo hivyo nchi nzima. Mkurugenzi huyo amesema hayo Juni 19, 2026, alipotembelea banda la TANESCO katika Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Chinangali, mkoani Dodoma. Amesema shirika linatambua kuwa mahitaji ya umeme yanaendelea kuongezeka kutokana na kukua kwa shughuli za kiuchumi, hivyo jitihada zinaendelea kufanyika kuhakikisha umeme unawafikia wananchi kwa ubora na uhakika kwa matumizi mbalimbali ya kijamii na kiuchumi. “TANESCO inafanya kazi kubwa ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia. Ai...

RAIS DKT. MWINYI: MFUMO WA SNR UMEFUNGUA UKURASA MPYA WA MAWASILIANO KATI YA SERIKALI NA WANANCHI

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Mfumo wa Sema na Rais Mwinyi (SNR) umechangia kupunguza urasimu, kuimarisha uwajibikaji wa watendaji wa Serikali na kujenga daraja la mawasiliano kati ya wananchi na Serikali yao.  Akizungumza katika mahojiano maalum ya kutathmini miaka mitano ya mfumo huo yaliyofanyika Ikulu, Zanzibar, amesema SNR imewawezesha wananchi kuwasilisha malalamiko na maoni yao moja kwa moja na kupatiwa ufumbuzi kwa haraka na uwazi. Rais Dkt. Mwinyi amesisitiza kuwa mfumo huo unashughulikia changamoto za kijamii na kiutendaji, huku masuala ya kimahakama yakipaswa kufuata taratibu rasmi za kisheria, ikiwemo kukata rufaa pale mwananchi anapokuwa hajaridhishwa na hukumu. Katika kipindi cha miaka mitano, SNR imepokea malalamiko 22,521, ambapo 20,623, sawa na asilimia 91.6, yamepatiwa ufumbuzi. Kwa mwaka 2026, Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) imetunukiwa Tuzo ya Taasisi Bora, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Maf...

WAZIRI WA FEDHA AFUNGUA SEMINA YA TWPG KUHUSU BAJETI YENYE MLENGI WA KIJINSIA

 Waziri wa Fedha, Mhe. Khamis Mussa Omar, akiwa mgeni rasmi, amefungua Semina ya Umoja wa Wabunge Wanawake Tanzania (TWPG) kuhusu Bajeti yenye Mlengo wa Kijinsia iliyofanyika leo, tarehe 19 Juni 2026, katika Ukumbi wa Pius Msekwa, Bungeni jijini Dodoma. Akizungumza katika ufunguzi wa semina hiyo, Mhe. Omar amesema bajeti yenye mlengo wa kijinsia ni nyenzo muhimu katika kuhakikisha kuwa wanawake, watoto na makundi maalum wanapata fursa sawa na kunufaika kikamilifu na utekelezaji wa mipango na matumizi ya rasilimali za umma. Amesema kuwa utekelezaji wa bajeti hizo unachangia kwa kiasi kikubwa kupunguza pengo la kijinsia, kupunguza umaskini na kuharakisha maendeleo ya kiuchumi kwa kuzingatia usawa na ujumuishi. “Bajeti yenye mlengo wa kijinsia inatuwezesha kufanya maamuzi sahihi ya maendeleo kwa kuzingatia mahitaji halisi ya makundi mbalimbali ya kijamii, huku ikihakikisha rasilimali za umma zinatumika kwa ufanisi na kwa usawa,” amesema Mhe. Omar. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa TWPG, ...

DKT. MAHERA AUNGA MKONO BAJETI YA SERIKALI KWA ASILIMIA 100, ATOA USHAURI WA KUHARAKISHA MAENDELEO

 Mbunge wa Jimbo la Butiama, Dkt. Charles Mahera, ameunga mkono kwa asilimia 100 Bajeti Kuu ya Serikali ya mwaka wa fedha 2026/2027, akiieleza kuwa ni bajeti ya maendeleo iliyolenga kukuza uchumi, kuongeza mapato ya ndani, kuimarisha huduma za jamii na kuwezesha makundi mbalimbali ya wananchi kiuchumi. Akichangia Bajeti Kuu ya Serikali leo Bungeni jijini Dodoma, Dkt. Mahera alimpongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uongozi wake, pamoja na Waziri wa Fedha na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji kwa kuwasilisha bajeti aliyoieleza kuwa ya kimkakati na yenye kuzingatia mahitaji ya wananchi. Katika mchango wake, Dkt. Mahera ameipongeza Serikali kwa kuendelea kutenga fedha kwa ajili ya kuwawezesha vijana, wanawake, wazee na wafanyabiashara wadogo maarufu kama machinga, akisema kundi hilo limeendelea kuwa mhimili muhimu wa uchumi wa wananchi.  Ameishauri Serikali kuendelea kuboresha mazingira ya biashara kwa machinga kwa kuwapatia maeneo rasmi ya kufanyia biashara, ...

MABALOZI WA MATAIFA MBALIMBALI WASAFIRI KWA SGR KWENDA DODOMA KUSHIRIKI "GRAND BUNGE BONANZA"

 Mabalozi wa mataifa mbalimbali wanaowakilisha nchi zao nchini Tanzania leo, Juni 19, 2026, wameanza safari kuelekea Jijini Dodoma kwa kutumia Treni ya Kisasa ya Mwendokasi (SGR) kushiriki Grand Bunge Bonanza litakalofanyika Juni 20, 2026 katika Uwanja wa Jamhuri. Bonanza hilo linatarajiwa kuwa jukwaa muhimu la kuimarisha umoja, ushirikiano na uhusiano wa kimataifa kupitia michezo, huku likiwa sehemu ya maandalizi na hamasa kuelekea mashindano ya AFCON 2027, ambayo Tanzania itaandaa kwa ushirikiano na Kenya na Uganda. Mabalozi waliosafiri ni wa nchi za Comoro, Rwanda, Burundi, Ethiopia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Afrika Kusini, Sudan, Zimbabwe, Msumbiji na Angola. Ushiriki wa mabalozi hao unaonesha namna michezo inavyoendelea kuwa chombo muhimu cha kuunganisha mataifa, kuimarisha diplomasia na kujenga mahusiano imara kati ya Tanzania na jumuiya ya kimataifa. Grand Bunge Bonanza linatarajiwa kukutanisha viongozi wa Serikali, wabunge, mabalozi na wadau mbalimbali wa mich...

GHATI CHOMETE ASHIRIKI MKUTANO WA MASPIKA WA JUMUIYA YA MADOLA AFRIKA KUSINI

 Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara, Mhe. Ghati Zephania Chomete, ameendelea kushiriki Mkutano wa 19 wa Maspika wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika unaoendelea jijini Johannesburg, Afrika Kusini, ukiwaleta pamoja viongozi wa mabunge kujadili masuala muhimu yanayogusa maendeleo ya bara la Afrika. Katika siku ya pili ya mkutano huo, Mwakilishi wa Spika wa Bunge la Tanzania, Mhe. Cecilia Paresso, aliwasilisha mada iliyojikita katika nafasi ya Mabunge ya Jumuiya ya Madola katika kuwawezesha vijana wa Afrika kushiriki kikamilifu katika kufanikisha maendeleo endelevu. Akiwasilisha mada hiyo, Mhe. Paresso alisisitiza kuwa mabunge yana wajibu mkubwa wa kutunga sheria, kupitisha sera na kuimarisha mifumo inayowapa vijana mazingira rafiki ya kushiriki katika uchumi jumuishi, uongozi na ubunifu. Alibainisha kuwa zaidi ya asilimia 65 ya wakazi wa Afrika ni vijana wenye umri chini ya miaka 30, jambo linaloifanya rasilimali hiyo kuwa nguvu muhimu katika maendeleo ya bara. Aidha, alie...

MSUVA AUNGA MKONO MPANGO WA MAFUNZO WA JAB KUELEKEA AFCON 2027

  Na Mwandishi Wetu Mchezaji wa Kimataifa wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Simon Msuva, amepongeza mpango wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) wa kuandaa mafunzo maalum kwa Waandishi wa Habari kuelekea Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2027), akisema hatua hiyo itasaidia kuimarisha mchango wa sekta ya habari katika kuitangaza Tanzania, kukuza vipaji vya wanamichezo na kuibua fursa mbalimbali za maendeleo zitakazotokana na mashindano hayo. Msuva ametoa pongezi hizo leo, tarehe 19 Juni 2026, alipotembelea Ofisi za Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari zilizopo Posta Mpya, Mtaa wa Jamhuri jijini Dar es Salaam na kufanya mazungumzo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi hiyo, Wakili Patrick Kipangula. Amesema Waandishi wa Habari wamekuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya michezo nchini kwa kutangaza vipaji vya wanamichezo, kuhamasisha ushiriki wa wananchi katika michezo na kuitangaza Tanzania ndani na nje ya nchi. “Mimi nawaombea waweze kutengeneza ...

UKAGUZI WA MIGODI WAENDELEA KUIMARISHA USALAMA NA UHIFADHI WA MAZINGIRA NCHINI

 📍Dodoma Tume ya Madini imeendelea kuimarisha ukaguzi wa migodi nchini kupitia Kurugenzi ya Ukaguzi wa Migodi na Mazingira kwa lengo la kuhakikisha shughuli za uchimbaji zinafanyika kwa usalama, ufanisi na kwa kuzingatia uhifadhi wa mazingira, hatua inayolenga kuhakikisha rasilimali za madini zinanufaisha kizazi cha sasa na kijacho. Akizungumza Juni 19, 2026, katika Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma, Afisa Mkaguzi wa Migodi wa Tume ya Madini, Rose Mika, amesema ukaguzi wa mara kwa mara unaofanyika katika migodi mikubwa, ya kati na midogo unalenga kuhakikisha shughuli za uchimbaji zinaendeshwa kwa kuzingatia Sheria ya Madini pamoja na Kanuni za Usalama, Afya na Utunzaji wa Mazingira za mwaka 2010. Amesema ukaguzi huo husaidia kubaini mapema changamoto zinazoweza kuhatarisha usalama wa wafanyakazi na wananchi wanaoishi jirani na maeneo ya migodi, hivyo kuwezesha hatua stahiki kuchukuliwa kabla ya kutokea kwa madhara. ...

SERIKALI YAWEKEZA TRILIONI 1.2 KATIKA VIFAA TIBA, YAAJIRI WATUMISHI 5,000 WA AFYA

Na Shaban Juma, Dodoma Naibu Waziri wa Afya, Dkt Florence Samizi amesema Serikali imeendelea kuimarisha upatikanaji wa vifaa tiba na rasilimali watu katika sekta ya afya ili kuongeza ufanisi wa huduma kwa wananchi, hususan watakaonufaika na huduma za Bima ya Afya nchini. Dkt. Samizi ameyasema hayo leo Juni 19, 2026 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali kwa niaba ya Waziri wa Afya Mhe Mohamed Mchengerwa kuhusu mkakati wa Serikali wa kuboresha vifaa tiba na rasilimali watu ili kuongeza ubora wa huduma za afya kwa wananchi, hususan katika maeneo ya vijijini. Amesema katika kipindi cha mwaka 2021 hadi 2026, Serikali imefanya uwekezaji mkubwa wa zaidi ya shilingi trilioni 1.2 kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya afya pamoja na ununuzi wa vifaa na vifaa tiba katika ngazi zote za utoaji huduma kuanzia Hospitali ya Taifa, Hospitali za Rufaa za Kanda na Mikoa, Hospitali za Halmashauri, Vituo vya Afya hadi Zahanati. Dkt. Samizi amesema kupitia uwekezaji huo, zaidi ya asilimia 85 ya vituo v...