Skip to main content

Posts

Showing posts from January 24, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Rais Samia Ameimarisha Uchumi Geita Kupitia Ujenzi wa Barabara ya Kasamwa-Gamashi - Prof. Shemdoe

Na OWM - TAMISEMI, Geita Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu -TAMISEMI Mhe. Prof. Riziki Shemdoe amemshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuidhinisha Shilingi 1,035,047,200/= za ujenzi wa dharura wa barabara ya Kasamwa- Gamashi yenye urefu wa kilomita 18, iliyoimarisha shughuli za kiuchumi kupitia Sekta ya Usafiri na Usafirishaji kati ya Wilaya ya Nyang’hwale na Makao Makuu ya Mkoa wa Geita. Prof. Shemdoe amesema barabara hiyo ina umuhimu kiuchumi kwa wananchi wa Nyang’hwale na Geita ambao wanategemea shughuli za kilimo na  ufugaji, hivyo uzalishaji unaofanyika Nyang’hwale ulikuwa hauwezi kufika makao makuu ya mkoa kutokana na changamoto iliyokuwepo ya ubovu wa miundombinu ya barabara ya  Kasamwa- Gamashi. “Ujenzi wa barabara hii ni muhimu sana kiuchumi, hivyo tunapaswa kumshukuru Mhe. Rais kwa kuidhinisha fedha zilizowezesha barabara kujengwa ili kuendeleza shughuli za wananchi kiuchumi,” amesisitiza Prof. Shemdoe. Sanjari na hilo, Prof. Shemdoe amempongeza Mshauri...

Kikwete Atembelea Familia ya Edward Lowassa

Nimefanya ziara ya kutembea familia za viongozi wastaafu siku ya leo. Ziara imekuwa na mafanikio makubwa. Serikali ya Awamu ya Sita imeendelea kuwa karibu na familia hizi kwa mujibu wa Sheria inayosimamia viongozi hawa. Katika ziara hii leo, nimepata nafasi ya kutembelea familia ya Hayati Dr. Omar Ally Juma, Dr. salim Ahmed Salim na Hayati Edward Lowasa.

Mzee Edwin Mtei Aagwa Arusha, Serikali Kuenzi Mchango Wake Kitaifa

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika ibada ya kumuaga aliyekuwa Gavana wa kwanza wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Mzee Edwin Mtei, akimtaja kuwa kiongozi mahiri, mzalendo na nguzo muhimu katika historia ya uchumi na demokrasia ya Tanzania. Akizungumza katika ibada hiyo ya mazishi iliyofanyika nyumbani kwa marehemu Tengeru, Dkt. Nchemba alisema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anatambua mchango mkubwa wa marehemu kwa Taifa na Serikali mara zote itaenzi  mchango wake mkubwa katika uchumi na demokrasia nchini. Waziri Mkuu alisema Mzee Mtei alikuwa miongoni mwa Watanzania wachache waliobahatika kuhudumu katika nyadhifa zote kuu za sekta ya fedha, ikiwemo kuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Waziri wa Fedha na mwakilishi wa Tanzania katika taasisi za fedha za kimataifa, mchango uliompa heshima ya kipekee kitaifa na kimataifa. Alisema katika maisha yake ya utumishi wa u...

Kawaida Amwaga Pongezi Kwa Rais Samia

Mwenyekiti wa UVCCM na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Ndugu Mohammed Ali Kawaida amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kuendelea kuleta maendeleo hususani ahadi alizotoa katika kampeni za Uchaguzi Mkuu katika siku 100 za kwanza za uongozi wake. Ndugu Kawaida akizungumza na maelfu ya wanafunzi wa Vyuo vya Kati na Vyuo Vikuu mkoani Dodoma leo tarehe 24 Januari 2026 katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete. Ametaja baadhi ya yaliyotekelezwa ikiwemo Bima ya Afya kwa wote na ajira kwa vijana zikiwemo za udaktari.

Mzee Edwin Mtei Aagwa Arusha, Serikali Kuenzi Mchango Wake Kitaifa

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika ibada ya kumuaga aliyekuwa Gavana wa kwanza wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Mzee Edwin Mtei, akimtaja kuwa kiongozi mahiri, mzalendo na nguzo muhimu katika historia ya uchumi na demokrasia ya Tanzania. Akizungumza katika ibada hiyo ya mazishi iliyofanyika nyumbani kwa marehemu Tengeru, Dkt. Nchemba alisema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anatambua mchango mkubwa wa marehemu kwa Taifa na Serikali mara zote itaenzi  mchango wake mkubwa katika uchumi na demokrasia nchini. Waziri Mkuu alisema Mzee Mtei alikuwa miongoni mwa Watanzania wachache waliobahatika kuhudumu katika nyadhifa zote kuu za sekta ya fedha, ikiwemo kuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Waziri wa Fedha na mwakilishi wa Tanzania katika taasisi za fedha za kimataifa, mchango uliompa heshima ya kipekee kitaifa na kimataifa. Alisema katika maisha yake ya utumishi wa u...

BMG Media Yajivunia Mafanikio ya Miaka 12

Waandishi wa habari nchini wameaswa kutumia fursa ya ulimwengu wa kidijitali ikiwemo mitandao ya kijamii kujiajiri ili kupunguza tatizo la ajira nchini. Wito huo umetolewa na mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa mwanza Edwin Soko wakati akikabidhi Tuzo Mkurugenzi wa Bmg media George Binagi. Tuzo hiyo imetolewa na Mtandao wa Youtoube baada ya chombo hicho cha habari za mtandaoni kufikisha idadi ya wachangiaji laki moja. Soko amewaasa waandishi wa habari kuachana na kasumba ya kutaka kuajiriwa na badala yake wajiajiri kwenye ulimwengu wa kidijitali ambako kuna fursa nyingi zitakazoweza kuwakwamua kiuchumi.  ‘’Tunapozungumzia Bmg tunazungumzia uchumi wa kidijitali,uchumi wa kidijitali kwa wale ambao mnaona ugumu kidogo ndio huu sasa,tutumie fursa hii kujiajiri na kutengeneza nafasi za ajira,zamani tulikuwa tunasema kama mjini pagumu shika Jembe ukalime,lakini siku hizi mabadiliko ya tabia nchi hata ukirudi kijijini mazao yatanyauka kutokana na ukame’’alisema Soko na kuo...