Na John Mapepele Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa leo ameweka jiwe la msingi kwenye jengo la utawala la jiji la Arusha na kushuhudia utiaji wa saini mikataba ya mradi wa Stendi Kuu ya Mkoa wa Arusha, Soko la Mrombo na Bustani ya Mapumziko ya Themi vyote vikiwa thamani ya takriban shilingi bilioni 40. Akikagua ujenzi wa jengo la utawala la Halmashauri ya jiji la Arusha lenye sakafu tisa ambalo litakapokamilika litagharimu bilioni 9.8 amemtaka mkandarasi kukamilisha ujenzi kwa wakati ili kuondokana na adha ya sasa ya watumishi kufanyia kazi kutokea kwenye ofisi zilizo katika maeneo tofauti hali inayochelewesha utoaji wa huduma kwa wananchi. "Namshukuru Mheshimiwa Rais kwa kuridhia kutoa fedha za ujenzi wa jengo hili kwa kuwa baada ya kukamilika litakuwa mkombozi kwa watumishi" . Amefafanua Mhe. Mchengerwa Aidha ameuelekeza uongozi wa Mkoa na Jiji la Arusha kuhakikisha jengo hilo linakamilika mara ...
Marato tv - Sauti ya Jamii