Na Mashaka Mhando, Muheza SERIKALI imetangaza mkakati wa kuhakikisha fursa za mikopo na zabuni za manunuzi ya umma zinawafikia vijana katika maeneo yote ya nchi ili kuwajengea uwezo wa kiuchumi na kupunguza ukosefu wa ajira. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Maendeleo ya Vijana), Joel Nanauka, ametoa kauli hiyo jana wilayani Muheza wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii ilipotembelea na kukagua shughuli za Kikundi cha Vijana cha ‘Mali Hai’. Nanauka ameiagiza Halmashauri ya Wilaya ya Muheza kuhakikisha inatenga asilimia 30 ya manunuzi ya umma kwa ajili ya vijana, ikiwa ni pamoja na kuwapatia zabuni za ujenzi kikundi hicho ambacho kimeonesha uaminifu kwa kurejesha mkopo wa Shilingi Milioni 20. “Wizara itahakikisha vijana wanafikiwa kila kona ya nchi ili wanufaike na fursa hizi. Niwaombe vijana kutumia vyema Shilingi Bilioni 200 zilizotolewa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya uwezeshaji wananchi,” amesema Nanauka. Pia Waziri Nanauka amewa...
Marato tv - Sauti ya Jamii