Skip to main content

Posts

Showing posts from December 29, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri Mkuu Akagua Soko Na Kituo Cha Mabasi Bunju B

Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba akizungumza na baadhi ya wafanyabiashara wa soko la Bunju B, Jijini Dar es Salaam, alipofanya ziara na kukagua maendeleo ya ujenzi wa soko hilo pamoja na ujenzi wa Kituo cha Mabasi, leo Desemba 29, 2025.

Anthony Mtaka ni Level Nyingine

  Watanzania wenye Fikra, Strategy, na Vision ya kuivusha nchi level nyingine, wapo, ila mfumo wa nchi, Umekaa kibinafsi mno. Anthony Mtaka ni mfano wa Kiongozi mzalendo na mwenye nia, Fikra na strategies za kuiendeleza nchi, Hili wazo la kujengea uwezo watanzania, likifanyiwa kazi, at National level lazima tutoboe,  Kuna watu wengi wenye mawazo mazuri tu kama Jenerali Mstaafu Venance Mabeyo⁩, kwamba mito yetu imetufaidishaje kama nchi zaidi ya kuneemesha nchi za wenzetu huko sudani ?  Trump anasema, America first" Alipokuwa anapeleka majeshi Ukrain, alisain deal na Rais wa Ukrain kuifaidisha Marekani kwenye swala la madini, mifano mingine ni Congo. Swali la kujiuliza, wanajeshi wetu wanapokwenda kufanya peace keeping, nchi yetu inafaidikaje, Mtaka anahoji, kama nchi imekusaidia kwenye peace keeping, Unapopata miradi yako kwa nini uwape wachina? Badala ya watanzania[ Kufa kufaana]....

Dkt. Mwigulu Akagua Hali ya Uzalishaji na Usambazaji wa Maji Ruvu Chini

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Desemba 29, 2025 amekagua hali za uzalishaji na usambazaji wa maji eneo la Ruvu Chini, mkoani Pwani. Akizungumza baada ya ukaguzi huo, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu amesema kuwa ili kukabiliana na changamoto ya upungufu wa maji unaotokana na Mabadiliko ya tabia ya nchi, Serikali ilianza utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maji katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita. “Mipango hii ya ujenzi wa miradi inayolenga kukabiliana na changamoto ya upungufu wa maji ilianza muda mrefu, Serikali iliona na ilianza kutafuta majawabu ya hali hii miaka mitatu iliyopita kwa kujenga miradi mikubwa itakayotoa matokeo chanya”.