Skip to main content

Posts

Showing posts from October 10, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

MKAKATI WA MAZINGIRA WAWEKWA MAENEO YENYE UCHAFU KUPEWA KINYAGO CHA FISI MANISPAA YA MUSOMA.

 Na Mwandishi wetu Jovina Massano Musoma. Manispaa ya Musoma mkoani Mara yaweka mkakati kukabiliana na uchafu wa mazingira maeneo yaliyo machafu kukabidhiwa kinyago cha fisi. Utaratibu huo umewekwa na Ofisi ya mkuu wa Wilaya kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkurugenzi wa halmashauri hiyo wakiwemo viongozi wa Kata. October 7,2026 utoaji wa tuzo za usafi na vinyago vya fisi vimetolewa kwa makundi mbalimbali kutoka kata, mitaa na shule. Uondoshaji taka huu unafanyika katika kata zote 16 zilizopo katika Manispaa hiyo kwenye barabara, Kaya,maduka,masoko,stendi za mabasi, taasisi viwanja vya michezo na maeneo ya wazi. Katika hafla hiyo ya utoaji tuzo hizo zimehudhuriwa na mkuu wa Wilaya ya Musoma Juma Chikoka ambapo amesema zoezi hilo litakuwa endelevu na litakuwa linafanyika kila mwezi ili kuhakikisha mazingira yanakuwa safi na kuweka usalama wa afya za wananchi. "Usafi unapaswa kuwa miongoni mwa vipaumbele na kila mmoja anatakiwa kuwajibika kuweka mazingira safi kuanzia mashuleni,majumba...

ABIRIA WAPONGEZA MSAKO WA KUSHTUKIZA KUTHIBITI AJALI BARABARANI

Abiria wanaosafiri kati ya Mikoa ya Mwanza, Geita, Kigoma na Kagera wamelipongeza Jeshi la Polisi Mikoa ya Mwanza na Geita kwa operesheni kabambe ya kushtukiza iliyolenga mabasi ya abiria na magari mengine ya usafirishaji, wakisema hatua hiyo inalinda maisha yao na kurejesha nidhamu barabarani. ​Pongezi hizo zimetolewa kufuatia operesheni ya pamoja iliyofanyika Oktoba 9 na kuongozwa na Wakuu wa Vikosi vya Usalama Barabarani wa mikoa hiyo miwili, ambapo zaidi ya magari 100 yalikaguliwa, ikiwa ni pamoja na mabasi 38 ya abiria. ​Wakizungumza wakati wa operesheni hiyo, baadhi ya abiria walieleza kuwa hatua hizo za kushtukiza zinapaswa kufanyika mara kwa mara ili kudhibiti ajali za barabarani ambazo zinaweza kuzuiliwa kwa kuongeza usimamizi. ​"Tunamshukuru sana Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani na askari wake. Dereva anapojua kuna ukaguzi wa kushtukiza anakuwa makini sana. Hatua hii inalinda roho zetu kwa sababu ajali nyingi zimekuwa zikitokea kwa uzembe wa madereva wanaolewa na ku...

S2KIZZY MBIONI KUACHIA ALBAMU YA VIRUS

  S2kizzy Atangaza Albamu Mpya Inayokwenda kwa Jina la "Virus" Producer na msanii nguli wa muziki wa Bongo Fleva, S2kizzy, ametangaza ujio wa albamu yake mpya inayokwenda kwa jina la Virus  S2KIZZY Leo oktoba 9,2026, amesema mbele ya waandishi wa Habari kuwa anatarajia kutoa Album mpya inayotajwa kuwa na mabadiliko makubwa, mtindo mpya, na sauti ya kipekee itakayowashangaza na kuwafurahisha mashabiki. Amesema Sifa Kuu za Albamu ya Virus  Mabadiliko na Ubunifu na vionjo kedekede ambavyo havijawai kutokea kwenye Tasinia ya mziki wa Bongo freva Amesema albamu hii ina sauti ya tofauti na ni fenomena, ikileta mabadiliko, muonekano mpya (artwork/front view), na mwelekeo wa kipekee kwenye muziki.  Ameongeza kuwa Ushirikiano yaani (Collabs za Kipekee): Albamu hiyo inajumuisha ngoma kali za kolabo, ambapo kwa mara ya kwanza ngoma yake na msanii Nandy imepatikana kupitia albamu hii, mbali na kolabo nyingine nyingi zenye mshangao.  S2KIZZY amewataka mashabiki kujiandaa k...