Skip to main content

Posts

Showing posts from May 25, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Viongozi wa Tanzania waungana maonesho ya Dunia nchini Japan

  Na Jovina Massano  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Mhandisi Hamad Masauni ameungana na ujumbe wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, katika ziara yao nchini Japan kushiriki Maonesho ya Dunia ya EXPO 2025 yanayofanyika Osaka, Japan. Mei 25, 2025, ikiwa ni Siku ya Taifa la Tanzania (Tanzania National Day) katika maonesho hayo, ujumbe wa Tanzania umeendelea kuonyesha utajiri wa nchi katika sekta mbalimbali zikiwemo utalii, uwekezaji, teknolojia na utamaduni. Ushiriki huu wa maonesho haya makubwa duniani unalenga kuitangaza nchi kimataifa, kuvutia wawekezaji na kuimarisha ushirikiano wa kimataifa hususan katika sekta za maendeleo endelevu na mazingira. Tanzania ni miongoni mwa mataifa yanayoshiriki kikamilifu katika EXPO 2025, ikiwa ni sehemu ya juhudi za serikali ya awamu ya sita katika kukuza diplomasia ya uchumi na kulinda mazingira. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. ...

Ndege za ATCL zazidi kupasua anga ruti za kimataifa

  KAMPUNI ya Ndege ya (ATCL), imeendelea kutanua wigo wa safari zake na sasa iko katika mchakato wa kutafuta vibali vya kuanza safari za kutua mji wa Lagos Nigeria, Accra Ghana, Ivory Coast na Dakar Senegal. Hayo yalisemwa jana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Mhandisi Peter Ulanga, wakati akizungumzia mafanikio ya shirika hilo ndani ya miaka minne ya Rais Samia Suluhu Hassan. Alisema hivi kari walianzisha safari za moja kwa moja kati ya Dar es Salaam na mji wa Kinshansa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), hatua inayolenga kupanua mtandao wake wa safari barani Afrika. Ndege za kampuni hiyo pia zinafanya safarai zake mji wa Lubumbashi DRC na kwa sasa ndege hizo zinafanya safari kwenye vituo 14 ndani ya nchi, vituo 10 Afrika na vitatu nje ya Afrika Ulanga alisema wakifanikisha mpango wa ruti hizo mpya ATCL itakuwa ni moja ya kampuni za ndege zinazounganisha Afrika Magharibi, Afrika Mashariki, Kusini mwa Afrika . Alisema Novemba mwaka jana walirudisha safari ya ...

Mbunge Ummy Mwalimu alivyoleta tabasamu kwa bodaboda Tanga kupitia leseni za udereva

Na: Dk. Reubeni Lumbagala, Tanga Usalama wa maisha ya binadamu ni jambo la msingi sana, na ndiyo maana unapaswa kulindwa kwa gharama zote. Katika suala la usalama barabani ambalo ni muhimu katika kuhakikisha raia wanakuwa salama dhidi ya ajali na majanga mengine yanayoweza kutokea barabarani, suala la madereva wenye sifa stahiki kwa maana ya kuhudhuria mafunzo ya udereva katika vyuo mbalimbali linasisitizwa sana. Kimsingi, ni kosa kisheria kwa dereva wa pikipiki au gari kuendesha chombo cha moto barabarani bila kuwa na leseni ya udereva. Hii inasisitiza watu kuhudhuria kwanza mafunzo ya udereva, kuhitimu na kupata leseni, ndipo waingie barabarani kuendesha vyombo vya moto. Lakini sheria hii inakiukwa na baadhi ya madereva kukosa leseni zinazotambulika. Wanachofanya baadhi yao ni kujifunza kuendesha vyombo vya moto mitaani na kuingia barabarani, jambo linaloongeza ajali na kusababisha ulemavu na vifo kwa watumiaji wa barabara. Madereva waliopo chini ya mwamvuli wa Umoja wa Wamiliki na W...

Wawekezaji Sekta ya Madini Wakaribishwa Mtwara

📍*Mtwara* Wawekezaji katika Sekta ya Madini wamekaribishwa kuwekezwa katika mkoa wa Mtwara kutokana na uwepo wa madini ya aina mbalimbali yakiwemo madini mkakati yanayotumika kwenye shughuli za viwanda. Hayo yamesemwa na  Mhandisi wa Migodi Mwandamizi, Michael Mtatiro alipokuwa akizungumza kwa niaba ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa huo, Winnifrida Mrema kupitia mahojiano maalum na wanahabari wanaoandaa kipindi maalum cha kuangazia mafanikio katika Sekta ya Madini. “Yapo madini  mbalimbali yakiwemo yanayotokana na mchanga wa bahari (Heavy mineral sands) yanayohusisha madini ya *Rutile, Titanium, Ilminite na Zircon*” amesema Mtatiro. Akielezea hali ya makusanyo katika mkoa huo, Mhandisi Mtatiro amesema kuwa, Mkoa wa Mtwara ulipangiwa kukusanya Shilingi Bilioni 9.18 kwa mwaka wa fedha 2024/2025, na kuongeza kuwa hadi sasa wamefanikiwa kukusanya Shilingi Bilioni 7.14 sawa na asilimia 75 ya lengo lililopangwa. “Tuna imani mpaka mwisho wa mwezi wa sita tutakuwa tumefikia lengo la asil...

Waziri Mkuu Anadi Vivutio Vya Utalii, Uwekezaji

  _▪️Ni katika siku ya Tanzania kwenye maonesho ya Osaka World EXPO 2025_ _▪️Asema mauazo ya bidhaa za Tanzania Japan yafikia sh bilioni 37_ _▪️Asisitiza Tanzania ni mahali salama kwa uwekezaji_   WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema ushirikiano wa Tanzania na Japan umezidi kukua katika nyanja za kiuchumi, kisiasa na kidiplomasia umezidi kuimarika siku hadi siku, ambapo mauzo ya biashara kati ya nchi hizo yameongezeka kutoka dola za Marekani bilioni saba mwaka 2023 hadi bilioni 37 kwa mwaka 2024. Mheshimiwa Majaliwa ameyasema hayo leo (Jumapili, Mei 25, 2025) alipomwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa maadhimisho ya Siku ya Tanzania kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Osaka (World Expo Osaka 2025) yanayoendelea nchini Japan. Amesema Wajapan wanapenda sana bidhaa kutoka Tanzania zikiwemo za kilimo kama chai, kahawa, ufuta, tumbaku, tingatinga, vinyago, katani, viungo kama karafuu pamoja na madini mbalimbali yanayopatikana nchini. Waziri Mkuu ametumia fursa h...