Skip to main content

Posts

Showing posts from October 25, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

JESHI LA MAGEREZA TANZANIA, USHELISHELI ZASAINI HATI YA MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO

 Ssgt Mawazo Mtondo na Wdrs Irine Nkana – DODOMA. Mkuu wa Jeshi la Magereza, CGP Jeremiah Yoram Katungu, leo Oktoba 23, 2026, amepokea ujumbe wa Maafisa wa Magereza kutoka nchini Ushelisheli, ukiongozwa na Kamishna wa Magereza wa nchi hiyo, CP Antoine Denousse, katika Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Msalato jijini Dodoma. Akizungumza mara baada ya kupokea ujumbe huo, CGP Katungu amepongeza ushirikiano wa kindugu na wa muda mrefu uliopo kati ya Jeshi la Magereza Tanzania na Idara ya Magereza ya Ushelisheli, akieleza kuwa ushirikiano huo umekuwa na mchango katika kubadilishana uzoefu na kuimarisha utendaji wa taasisi hizo. Amebainisha kuwa ushirikiano huo umetoa fursa kwa Maafisa wa Magereza kutoka Tanzania kufanya kazi katika Magereza ya Ushelisheli, hatua inayochangia kubadilishana ujuzi na kuboresha mfumo wa uendeshaji wa magereza nchini humo. Kwa upande wake, Kamishna wa Magereza wa Ushelisheli, CP Antoine Denousse, amesema ziara hiyo inalenga kuendeleza na kuimarisha ...

KAMATI YA BUNGE YALIPONGEZA SUMAJKT KWA UBUNIFU WA UZALISHAJI

 Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU), ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Mheshimiwa Najma Murtaza Giga (Mb), imetembelea Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Mgulani, jijini Dar es Salaam, na kupongeza ubunifu wake katika uzalishaji. Ziara hiyo iliyofanyika Oktoba 23, 2026, ilihusisha Kiwanda cha SUMAJKT Bottling Company Limited, kinachozalisha maji ya Uhuru Pick, pamoja na Kiwanda cha Ushonaji cha SUMAJKT Garments Co. Ltd, vyote vilivyopo Mgulani. Kamati hiyo ilipokelewa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mheshimiwa Dkt. Rhimo Nyansaho (Mb), aliyeongoza ujumbe wa viongozi waandamizi wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa. Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa JKT, Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT, Brigedia Jenerali Petro Ngata, ameishukuru Kamati kwa ziara hiyo na kusisitiza kuwa shirika litaendelea kuimarisha uzalishaji wa bidhaa za ushonaji na maji ya Uhuru Pick. Akihitimisha ziara hiyo, Mwenyekiti wa Kamati, Mhesh...

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MAMBO YA NJE, ULINZI NA USALAMA YATEMBELEA TATC–NYUMBU

Kamati ya Kudumu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU), tarehe 24 Oktoba , 2026, imefanya ziara ya kikazi katika Shirika la Tanzania Automotive Technology Centre (TATC–Nyumbu), lililopo Kibaha, mkoani Pwani, kwa lengo la kufahamu utekelezaji wa majukumu ya shirika hilo, mafanikio yaliyofikiwa pamoja na changamoto zinazolikabili. TATC–Nyumbu ni shirika la kimkakati lililo chini ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, linalojishughulisha na utafiti, uhaulishaji wa teknolojia, uundaji wa vipuri vya magari na utengenezaji wa mitambo. Shirika hilo lina mchango muhimu katika kukuza uwezo wa ndani wa kiteknolojia na kuendeleza sekta ya viwanda nchini. Kamati hiyo iliongozwa na Makamu Mwenyekiti wake, Mheshimiwa Paschal Inyasi (Mb), na kupokelewa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mheshimiwa Dkt. Rhimo Nyansaho. Viongozi wengine waliohudhuria mapokezi hayo ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Faraji...