KONGO: Kamanda wa Brigedi ya kujibu ya mashambulizi (FIB) inayohudumu chini ya Mwamvuli wa Umoja wa Mataifa (MONUSCO) nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Brigedia Jenerali Alexandar Masangura amewatembelea Walinda amani wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) wa Kikundi Cha Utayari (TANZQRF-05) kilichokalia eneo la Kiteule cha Mambasa kilichopo katika Jimbo la Ituri, Mashariki mwa nchi hiyo tarehe 25 Julai 2026. Lengo la ziara hiyo ni kujionea mazingira halisi ya kiutendaji wakati Kikundi hicho kikiendelea kutekeleza jukumu la ulinzi wa amani. Brigedia Jenerali Masangura amewapongeza walinda amani hao kwa namna wanavyotekeleza majukumu kwa weledi licha ya kuwa na changamoto kadhaa za kimazingira. Brigedia Jenerali Masangula wa Tanzania anaongoza Brigedi hiyo inayoundwa na vikundi kutoka nchi za Tanzania, Malawi, Kenya na Nepal ambavyo vinaendelea kuwajibika Mashariki ya Kongo kwa kulinda raia dhidi ya mashambulizi kutoka kwa makundi ya watu wenye silaha.
Marato tv - Sauti ya Jamii