Skip to main content

Posts

Showing posts from April 21, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete Kutoa Mafunzo ya Uongozi Nchini Marekani

 Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, yuko Boston, Marekani ambapo anashiriki kutoa mafunzo kwa Mawaziri wakiwemo wa Fedha na wa Mipango kutoka nchi mbalimbali zinazoendelea kupitia Mpango wa Uongozi wa Ngazi ya Mawaziri wa Harvard “Harvard Ministerial Leadership Program” inayoendeshwa na Chuo Kikuu cha Harvard.  Mheshimiwa Rais Mstaafu ni mmoja wa Viongozi Wakuu wa Kitaifa Wastaafu wanaoshiriki kutoa mafunzo hayo. Pamoja na Viongozi Wakuu wa Kitaifa Wastaafu, wengine wanaoshiriki kutoa mafunzo hayo ni pamoja na Wakuu wa Taasisi za Kimataifa, Mashirika Binafsi na Wabobezi katika masuala ya sera, uchumi na maendeleo kutoka sehemu mbalimbali duniani. Kutoka Tanzania, mafunzo hayo yamehudhuriwa na Mhe. Khamis Mussa Omar, Waziri wa Fedha; Mhe. Prof. Kitila Alexander Mkumbo, Waziri Ofisi ya Rais - Mipango na Uwekezaji; na Mhe. Juma Malik Akil, Waziri wa Fedha na Mipango wa Zanzibar.

Veterinarians: Africa’s First Line of Defence for Public Health

By Dr Samuel Kahariri What comes to mind when you think about public health threats? Perhaps you picture hospital wards, busy emergency rooms, or doctors treating patients. However, most diseases that threaten human health do not begin in hospitals, they often start quietly in animals with first warning signs often seen on farms, in livestock markets, abattoirs or in communities where humans and animals interact closely everyday. Yet, in African countries, the professionals best positioned to detect these threats early– the veterinarians remain underutilized in the design and implementation of our public health systems. As the world marks World Veterinary Day, under the theme "Veterinarians: Guardians of Food and Health," we are reminded of the critical role veterinarians play not only in animal health but also in protecting our health, our food, and national resilience. In Africa, this role is important as millions of families depend on livestock for food, and income. Veteri...

Katibu Mkuu Ccm, Ujumbe Mtandao wa Viongozi Wanawake Afrika Wafanya Mazungumzo

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndg. Asha-Rose Migiro, leo tarehe 21 Aprili 2026 amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa Mtandao wa Viongozi Wanawake wa Afrika (African Women Leaders Network - AWLN), ulioongozwa na Marais wastaafu wa Jamhuri ya Liberia, Mhe. Ellen Johnson Sirleaf, na Jamhuri ya Shirikisho la Kidemokrasia ya Ethiopia, Mhe. Sahle-Work Zewde, jijini Dar es Salaam. Mazungumzo hayo yalijikita katika hali ya kisiasa nchini pamoja na matukio ya wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, yakihusisha pia umuhimu wa kudumisha amani, utulivu na mshikamano wa kitaifa. Ujumbe huo upo nchini Tanzania kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kufanya mashauriano na viongozi mbalimbali wa kitaifa kuhusu maendeleo ya kisiasa na juhudi zinazoendelea za kuimarisha demokrasia na utawala bora, ikiwa ni sehemu ya mchango wa wanawake viongozi wa Afrika katika kulinda amani na utulivu barani.

Makamu wa Rais Ashiriki Ibada ya Kumuaga Marehemu Askofu Mfumbusa

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amesema Taifa litaukumbuka mchango mkubwa aliyoutoa marehemu Askofu Bernadin Mfumbusa, enzi za uhai wake ikiwemo kuwa kiungo muhimu wa kuunganisha Kanisa Katoliki na Madhehebu mbalimbali pamoja na Dini zingine. Makamu wa Rais amesema hayo mara baada ya kushiriki Ibada ya kumuaga na kumuombea Askofu wa Jimbo Katoliki Kondoa, marehemu Askofu Bernadin Francis Mfumbusa, iliyofanyika Katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Paulo wa Msalaba, Jimbo Kuu Katoliki Dodoma. Amesema Marehemu Askofu Mfumbusa alijitolea katika kuunganisha dini na madhehebu ili zifanye kazi kwa kuheshimiana, kushirikiana na kupendana. Ameongeza kwamba Taifa litakumbuka mchango wake katika kuhamasisha elimu pamoja na kufanya kazi kubwa ya kuhamasisha na kusimamia ujenzi na uendelezaji wa huduma za Afya katika Wilaya ya Kondoa na Taifa kwa ujumla. Makamu wa Rais amesema Marehemu Askofu Mfumbusa ametoa mchango katika sekta ya Mawasiliano na H...

Tume ya Uchunguzi Kuwasilisha Ripoti Yake April 23

Tume ya Uchunguzi ya matukio ya Oktoba 29 inatarajiwa kuwasilisha ripoti yake tarehe 23 mwezi huu (Alhamisi) kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan. Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Othman Chande, wakati akizungumza na waandishi wa habari leo katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam. Tume hiyo imesema ripoti hiyo itakuwa msingi muhimu wa kutoa mwelekeo kuhusu matukio hayo.