Skip to main content

Posts

Showing posts from May 26, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Milioni 70 Zaokolewa na Takukuru Mara yakiwemo Malipo ya Makaburi Hewa

Na Shomari Binda-Musoma  TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ( TAKUKURU) wa Mara imefanikiwa kuokoa kiasi jumla ya shilingi milioni 70,212,800.00 yakiwemo malipo ya makaburi hewa. Hayo yamesemwa leo mei 27,2025 na Mkuu wa taasisi hiyo Muhamed Shariff alipokuwa akitoa taarifa ya utendaji kazi kwa kipindi cha miezi 3 ya januari hadi machi 2025 kwa Waandishi wa Habari. Amesema katika zoezi la uhamishaji wa makaburi kwa wananchi wanaopisha upanuzi wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti Kata ya Nyatwali Wilaya ya Bunda kiasi cha milioni 49,200,,200 kimeokolewa. Mkuu huyo wa TAKUKURU amesema fedhà hizo iliyokuwa ilipwe kama kifuta machozi kwa wanufaika wa makaburi hewa 123 ambapo kila kaburi lllipaswa kulipwa shilingi 400,000. Amesema walifanikiwa jambo hilo baada ya kufanya uchambuzi wa mchakato mzima uliotumika kuhalalisha ulipaji fidia za makaburi yaliyopswa kuhamishwa. Amedai kuwa uchambuzi ulibaini katika hatua ya uthaminishaji makaburi hayo yalithaminishwa kwa namna yalivyotambulish...

Majaliwa: Serikali itaendeleza Mikakati ya Kuwaunganisha Wafanyabiashara

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali itaendelea na mikakati ya kuwaunganisha wafanyabiashara wa Tanzania na wa Mataifa mbalimbali duniani ikiwemo Japan ili kuwawezesha kunufaika na fursa mbalimbali zilizopo katika mataifa hayo. Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Serikali imekuwa ikifanya hivyo kwa kushiriki katika makongamano mbalimbali ya kimataifa ambayo yamekuwa yakiwakutanisha wafanyabiashara na wawekezaji ili kuongeza tija kubwa kwenye masuala ya biashara na uwekezaji. Amesema hayo leo (Jumatatu, Mei 26, 2025) alipofungua kongamano la Biashara, Uwekezaji na Utalii lililowakutanisha wafanyabiashara wa Tanzania na wafanyabiashara na wawekezaji wa Japan katika ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya Westin, Osaka, Japan ikiwa ni sehemu ya  ushiriki wa Tanzania katika maonersho ya World Expo Osaka 2025. “Tumewaeleza wafanyabaishara na wawekezaji hawa wa Japan fursa ambazo zipo nchini, hii ni mara ya tatu tunakutana na wafanyabara na wawekezaji kutoka Japan, tayari tumeanza kuo...

Zaidi ya Sh. Bilioni 28 Kujenga Kituo Cha Upandikizaji Figo Tanzania

_▪️Ni kikubwa katika Ukanda wa Jangwa la Sahala_ _▪️Pia itatumika katika kutoa mafunzo kwa madaktari bingwa_   WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ameshuhudia utiaji saini wa hati ya makubaliano ya ujenzi wa kituo kikubwa cha kupandikiza figo pamoja na utoaji mafunzo kwa madaktari bingwa ambacho kitakuwa ni kikubwa katika ukanda wa Jangwa la Sahara. Kituo hicho ambacho kitajengwa kwenye Hospitali ya Kanda ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma ni ushirikiano kati ya Shirika la Tiba la TOKUSHUKAI, Hospitali ya Benjamin Mkapa na Chuo Kikuu cha Dodoma na kinatarajia kugharimu zaidi ya shilingi bilioni 28 ikiwa ni msaada usiokuwa na masharti yoyote. Utiaji saini huo umefanyika jana (Jumatatu, Mei 26, 2025) wakati kongamano la Biashara, Uwekezaji na Utalii lililowakutanisha wafanyabiashara wa Tanzania na wafanyabiashara na wawekezaji wa Japan katika ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya Westin, Osaka, Japan, ikiwa ni sehemu ya  ushiriki wa Tanzania katika maonersho ya World Expo Osaka 2025. Kongamano ...

Majaliwa: Serikali itaendeleza Mikakati ya Kuwaunganisha Wafanyabiashara

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali itaendelea na mikakati ya kuwaunganisha wafanyabiashara wa Tanzania na wa Mataifa mbalimbali duniani ikiwemo Japan ili kuwawezesha kunufaika na fursa mbalimbali zilizopo katika mataifa hayo. Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Serikali imekuwa ikifanya hivyo kwa kushiriki katika makongamano mbalimbali ya kimataifa ambayo yamekuwa yakiwakutanisha wafanyabiashara na wawekezaji ili kuongeza tija kubwa kwenye masuala ya biashara na uwekezaji. Amesema hayo leo (Jumatatu, Mei 26, 2025) alipofungua kongamano la Biashara, Uwekezaji na Utalii lililowakutanisha wafanyabiashara wa Tanzania na wafanyabiashara na wawekezaji wa Japan katika ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya Westin, Osaka, Japan ikiwa ni sehemu ya  ushiriki wa Tanzania katika maonersho ya World Expo Osaka 2025. “Tumewaeleza wafanyabaishara na wawekezaji hawa wa Japan fursa ambazo zipo nchini, hii ni mara ya tatu tunakutana na wafanyabara na wawekezaji kutoka Japan, tayari tumeanza kuo...

Wagonjwa Kituo Cha Afya Kisorya Wamshukuru Mbunge Ghati Chomete

Na Shomari Binda-Bunda WAGONJWA wanaohudumiwa kwenye kituo cha afya Kisorya kilichopo jimbo la Mwibara wilayani Bunda wamemshukuru mbunge Ghati Chomete kuwafikia na kuwafariji. Licha ya kuwafariji ametoa msaada wa mashuka kwaajili wodi za kituo hicho zitazoweza kusaidia wagonjwa watakaolazwa kwaajili ya matibabu. Msaada huo ameutoa leo mei 26,2025 alipofika kituoni hapo akiambatana na viongozi mbalimbali wakiwemo wa Jumuiya ya Wanawake wa CCM Wilaya ya Bunda. Wakizungumza hospitalini hapo wagonjwa waliofika kupata matibabu na wale waliolazwa wamemshukuru mbunge huyo kwa moyo wake wa upendo. Wamesema ni viongozi wachache wanaoguswa na kuwa na moyo wa kuifikia jamii kwa lengo la kusaidia na kutoa faraja. Mmoja wa wagonjwa waliokuwa hospitalini hapo aliyejitambulisha kwa jina la Mariam Suleiman mkazi wa Kisorya amesema yupo jirani na kituo hicho cha afya na hajawahi kuona kiongozi yoyote aliyekitembelea na kutuo msaada. Amesema moyo alionao mbunge huyo ni wa pekee na anastahili kupewa shu...

Rais Samia Aongoza Kikao Cha Kamati Kuu Ya Ccm,Wasira Akiwepo

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiongoza Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa iliyoketi jijini Dodoma, leo Jumatatu tarehe 26, Mei 2025.