Skip to main content

Posts

Showing posts from November 11, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Ulinzi wa Msitu wa Mgori Kuimarika

TFS kuongeza askari, vifaa na kujenga kituo cha walinzi Pohama Na Mwandishi Wetu, Singida Ulinzi wa Msitu wa Hifadhi wa Mgori mkoani Singida unatarajiwa kuimarika baada ya Kamishna wa Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Profesa Dos Santos Silayo, kutangaza mpango wa kuongeza askari, kupeleka vifaa vya kisasa vya ulinzi na kuanzisha ujenzi wa Ranger Post katika kijiji cha Pohama. Profesa Silayo alitoa ahadi hiyo leo Jumanne, Novemba 11, 2025,  wakati wa kikao maalum cha Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Singida, kilichofanyika katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Mhe. Godwin Gondwe, kwa lengo la kujadili mikakati ya kuimarisha ulinzi na uhifadhi wa Msitu wa Mgori. Msitu huo, ambao ni miongoni mwa hifadhi muhimu nchini, umekuwa ukikabiliwa na changamoto za uchomaji moto, ukataji miti holela na uvamizi unaoathiri juhudi za Serikali katika kulinda rasilimali za misitu. Akizungumza katika kikao hicho, Mhe. Gondwe alisisitiza umuhimu wa uhifadhi shirikishi, akipendek...

VERONICA MGETA AHIMIZA MSHIKAMANO WA KITAIFA

Alieyekua mgombea ubunge wa jimbo la Ilemela Veronica Calist Mgeta katika hutuba yake mbele ya wandishi wa habari amesema kufuatia uungwaji mkono alioupata wakati wa uchaguzi mkuu oktoba 29 Jimbo la Ilemela ni dhahiri kuwa anadeni kubwa kwa wanachi. “Imani yangu kwa wapiga kura ni kubwa namna mlivyojitokeza hakika ungwaji mkono huu sikua nautegemea hivi mmenipa heshima kubwa maishani mwangu najiona mwenye deni sina cha kuwalipa ila mungu pekee ndie anaweza kuwatosheleza alisema mgeta” Mgeta amesema kampeni zilizofanyika kata 19 za jimbo la ilemela zimeshuhudiwa   na wananchi  waliojitokeza kwa wingi katika mikutano yetu ya kampeni ili kutusikiliza sera mikakati ya kuwaleta maendeleo wananchi endapo CHAUMMA ingeshinda . Veronica alisema shukrani pekee hazitoshi ila ataendelea kushirikiana na wananchi wa jimbo hilo katika kuyafikia maendeleo endelevu na kujenga uchumi wa jamii ya wana Ilemela wote kwa kuzingatia misingi ya utu na uzalendo. Aidha Veronica Mgeta amesema Uch...