Skip to main content

Posts

Showing posts from April 25, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Miaka minne ya Rais Samia Arumeru yapokea shiligi Bilioni 100.6 za maendeleo

   ðŸ“Œ Dkt. Biteko asisitiza Watanzania wasijaribu kuchezea amani 📌 Dkt. Biteko awataka Watanzania kuenzi, kudumisha Muungano  Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema wananchi wa wilayani Arumeru, mkoani Arusha na Watanzania kwa ujumla wana kila sababu ya kumshukuru na kumuombea Rais Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo nchini. Dkt. Biteko amesema hayo leo Aprili 25, 2025 katika mkutano wa hadhara uliofanyika Tengeru Wilaya ya Arumeru, Mkoa wa Arusha ambapo amesema katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Dkt. Samia wilaya ya Arumeru imepokea zaidi ya shilingi bilioni 100 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo. “Arusha DC imepata fedha kiasi cha shilingi bilioni 49.6 na Wilaya ya  Arumeru imepokea zaidi ya shilingi  bilioni 51  kwa ajili ya shughuli na miradi mbalimbali ya maendeleo,” ame...

Kiongozi Chadema ainanga kauli mbiu ya kupinga uchaguzi akisema chama cha harakati kinajiandaa kujiua kisiasa

  Kiongozi mwandamizi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kutokea Tarime, mkoani Mara, Mohania Joseph Peter, amekianga chama hicho, akisema ni cha kiharakati na hakiwezi kufanya siasa. Ndugu Mohania, ambaye amewahi kushika nafasi mbalimbali katika chama hicho ngazi ya mkoa, katika Baraza la Vijana wa Chama hicho (Bavicha), kabla ya kuwa msaidizi katika ofisi ya chama hicho Mkoa wa Mara, amesema chama kinachoendekeza harakati kinajiandaa kufa kisiasa na hakiwezi kuaminiwa kushika dola. Kiongozi huyo amesema hayo, alipopewa nafasi ya kuzungumza kwenye mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, katika Uwanja wa Shamba la Bibi, mjini Tarime, leo Ijumaa tarehe 25 Aprili 2025, ambapo pia alitangaza uamuzi wa kuhama Chadema, akijiunga na CCM. “Nimekuwa Mwenyekiti wa Bavicha Mkoa wa Mara. Nimekuwa Mwenyekiti wa Bavicha Jimbo la Tarime Vijijini. Lakini pia nimekuwa msaidizi wa ofisi ya Chadema mkoa. Kuna sababu...

Shule nyingine mpya ya sekondari yafunguliwa kata ya Mugango Musoma Vijijini

  Na Shomari Binda-Musoma  SHULE nyingine mpya ya sekondari ya Kumbukumbu ya Profesa David Masamba imefunguliwa na kukabidhiwa leo aprili 25,2025 kwa wananchi wa Kijiji cha Kurwaki Kata ya Mugango. Hii inakuwa shule ya pili kufunguliwa kwenye jimbo hilo ndani ya siku 2 huku wananchi wakiishukuru serikali kwa kupata shule hiyo. Akizungumza mara baada ya kuitembelea shule hiyo na kuikagua Mkuu wa Wilaya ya Musoma Juma Chikoka ametoa wito kwa wananchi kuilinda na kuitunza shule hiyo ili watoto waendelee kupata elimu. Amesema jambo lingine ni kuhakikisha wanawapa ushirikiano walimu ili waendelea kufundisha na kuwa na ari ya ufundishaji na kuwataka wanafunzi kusoma kwa bidii. Chikoka amesema wanaendelea kutoa asante na shukrani kwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa kiasi cha shilingi milioni 584 kuunga nguvu za wananchi walioanza kuijenga shule hiyo. Katika ujumbe wake kwa wananchi mkuu huyo wa Wilaya amesisitiza suala la chakula shuleni na hatamvumilia yoyote atakayekwamisha ...

Taifa limepata mafanikio makubwa miaka 61 ya Muungano - Majaliwa

  WAZIRI MKUU,  Kassim Majaliwa amesema Tanzania ni Taifa lililopata mafanikio makubwa katika sekta mbalimbali za maendeleo katika kipindi cha miaka 61 ya Muungano Amesema hayo leo (Ijumaa, Aprili 25, 2025) wakati akizungumza na maelfu ya wakazi wa Wilaya ya Ukerewe Mkoani Mwanza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Getrude Mongela.  Mheshimiwa Majaliwa amefanya ziara ya siku moja katika Wilaya ya Ukerewe ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 61 ya Muungano Amesema kuwa Muungano wa Tanzania Bara na Zanzibar umewezesha kujenga Taifa imara na lisiloyumba “Muungano huu umewezesha kuwa na  Taifa ambalo limepata mafanikio katika miradi mbalimbali ya maendeleo Bara na Visiwani, Muungano huu ni tunu ambayo kila mmoja anapaswa kuilinda, kuienzi na kuisemea popote.” “Kwenu hapa Ukerewe Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan mabilioni mengi ya fedha yameletwa kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo katika sekta eli...

Balozi apiga marufuku wimbo unaochochea chuki dhidi ya wapinzani

  _Una maneno yaliyotumiwa dhidi ya Nduli Idi Amin_ _Asisitiza utaifa ulindwe kwa wivu mkubwa_ KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Emmanuel John Nchimbi amepiga marufuku wimbo unaobeza na kuchochea chuki dhidi ya vyama vya upinzani, akiagiza usitumiwe na wanaCCM popote, kwani wao wanapaswa kuwa mfano wa kuigwa kuhamasisha upendo, umoja na mshikamano nchini. Balozi Nchimbi alichukua hatua hiyo alipokuwa akihutubia umati mkubwa wa maelfu ya wananchi wa Mji wa Shirati, wilayani Rorya, kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Obwele, leo Ijumaa tarehe 25 Aprili 2025, akiwa katika siku ya nne ya ziara yake ya kikazi mkoani Mara. Kabla ya kutoa kauli hiyo, kwanza Balozi Nchimbi aliwakumbusha wananchi waliokuwa wakimsikiliza wimbo maarufu uliokuwa unatumiwa na wanajeshi wa Tanzania kwenye Vita vya Kagera, wakati wa kumtoa na kumpiga Nduli Idi Amin Dada, aliyekuwa Rais wa Uganda, baada ya kuvamia mipaka ya Tanzania. “Mnaukumbuka ule wimbo ulikuwa unaimbwa wakati ...

Serikali Kuendelea Kuwekeza Katika Sekta Ya Afya - Dkt. Biteko

📌 Dkt. Biteko atambelea Hospitali ya Wilaya ya Meru Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Serikali imeahidi kuendelea kuboresha huduma za Afya nchini katika ngazi zote ili kuboresha huduma za Afya kwa Watanzania. Hayo yamesemwa Aprili, 25, 2025 na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko akiwa ziarani Mkoani Arusha ambapo amesema kuwa lengo la uwekezaji katika sekta ya afya ni kusigeza huduma za afya kwa wananchi." Serikali inayoongozwa na Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea na uwekezaji mkubwa unaofanya kwa kujenga hospitali, vituo vya afya na zahanati katika maeneo mbalimbali nchini. Akizungumza baada kutembelea Hospitali ya Wilaya ya Meru, iliyopo Wilaya ya Arumeru, Mkoa wa Arusha, Mhe. Dkt. Biteko amesema lengo la uwekezaji katika sekta ya afya ni kuboresha afya za Watanzania. “ Kama mnavyofahamu afya ndio mtaji wa wananchi na Serikali itaendelea kuboresha huduma za afya kwa kujenga hospitali mpya na kufanyia ukarabati zilizopo,” a...