📍Simiyu Serikali imesema itaendelea kusimamia kwa karibu utekelezaji wa miradi ya Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) inayotekelezwa na kampuni za uchimbaji madini nchini, ili kuhakikisha wananchi wanaoishi jirani na migodi wananufaika moja kwa moja na shughuli za uchimbaji madini. Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Simiyu, Mayigi Makolobela, alisema hayo hivi karibuni alipokagua utekelezaji wa miradi ya CSR inayofanywa na kampuni za uchimbaji madini katika mkoa huo, akibainisha kuwa miradi hiyo imechangia kwa kiasi kikubwa kuboresha huduma za kijamii ikiwemo elimu, afya na miundombinu ya umeme. “Serikali inatambua mchango mkubwa wa sekta ya madini katika kukuza uchumi wa nchi na kuboresha maisha ya wananchi. Ndiyo maana tunasisitiza kampuni zote za uchimbaji, zikiwemo zinazomilikiwa na wachimbaji wadogo, kutekeleza wajibu wao wa kijamii kupitia miradi ya CSR ili jamii inayoishi jirani na migodi inufaike moja kwa moja na rasilimali hizo,” alisema Makolobela. Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kampuni ...
Marato tv - Sauti ya Jamii