Skip to main content

Posts

Showing posts from April 21, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

MNEC Manguzo aendelea Kuigusa Jamii

  BUSWELU ILEMELA 🗓️ 21/4/2025 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa (MNEC)Ndugu Leonard  Mahenda Maarufu Kwa Jina la Manguzo ameendelea kuigusa Jamii Kwa kutoa Viti Mwendo (Wheel Chair)  30 Kwa watoto wenye Ulemavu. Viti hivyo vimetolewa kwa watoto wanaolelewa katika Kituo cha Kulelea watoto yatima cha Watoto wa Africa Orphanage kilichopo Busenga, Buswelu Ilemela Mwanza Tanzania. Akisoma Risala Mkurugenzi Wa Taasisi ya Inuka Angaza  Eva Samara  amesema Lengo Lao ni kuhakikisha Wanapata Viti Mwendo 100 kila Mwaka. Mahende ambaye pia ni Mkurugenzi Wa QWIHAYA INTERPRISES na MNEC Taifa amekuwa akiigusa Sana Sana Jamii ya watu wenye ulemavu  Kwa Kutoa Viti Mwendo 30 (Wheel Chair) na kufanya Jumla ya Viti Mwendo 36 kwenye Kituo hicho Akijibu Risala ya Mkurugenzi Wa Kituo cha Inuka Uangaze MNEC Manguzo  amesema Kitendo cha kutoa Viti Mwendo 30 ni ishara ya kufufuka na Yesu Kristu kama agizo la Upendo lilitolewa na Bwana yetu Yesu Kristu. Ai...

Mchungaji Dkt. GetrudeLwakatare aendelea kukumbukwa

....Alisaidia mahabusu 150 kuachiwa huru ........Alisomesha maelfu kutoka kaya maskini  Na  Mwandishi Wetu KANISA la Mlima wa Moto la Mikocheni jijini Dar es Salaam, limeendelea kuenzi kazi nzuri zilizokuwa zikifanywa na mwasisi wake Hayati Askofu Dk. Getrude Rwakatare ikiwemo kuombea amani ya nchi na viongozi wake. Hayo yalisemwa jana Jumapili na Askofu wa Kanisa hilo, Rose Mgeta wakati wa tamasha la kuadhimisha miaka mitano tangu mwasisi wa Kanisa hilo Dk Getrude Rwakatare afariki dunia. Alisema kila mwaka wamekuwa wakifanya tamasha kubwa kama hilo kuenzi kazi za mwasisi wake ikiwemo kuliombea taifa na viongozi wake. “Kanisa hili ni maono ya Askofu wetu mwanzilishi hayati Askofu Dk. Getrude Rwakatare na tumekuwa tukiyaendeleza maono yake mwaka hadi mwaka na makanisa yote ya Mlima wa Moto wamekuwa wakifanya maombi haya kila mwaka,” alisema Alisema kanisa hilo litaendelea kuombea taifa liendelee kuwa na amani na kuondokana na majanga kama ukame, mafuriko na matatizo mbalimbali...

Kambi ya madaktari bingwa, Tanzania yatibu maelfu Comoro

…JKCI, Global Medicare wawasilisha ripoti serikalini Na Mwandishi Wetu KAMBI ya matibabu iliyofanywa na madaktari bingwa wa Tanzania nchini Comoro imekuwa ya mafanikio makubwa kwani wananchi zaidi ya 2,270 waliokuwa na changamoto za kiafya walipata tiba. Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Dk Peter Kisenge wakati wa kukabidhi ripoti ya kambi hiyo kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Dk  Seif Shekilage. Ripoti ya kambi hiyo iliyofanyika Novemba mwaka jana iliwasilishwa sanjari na andiko la pendekezo la maandalizi ya ziara ya ujumbe wa sekta ya afya kutoka Comoro nchini Tanzania Iliyowasilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Global Medicare, Abdulmalik Mollel. Madaktari hao bingwa walitoka Taasisi ya Mifupa (MOI), Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), JKCI, Hospitali ya Benjamin Mkapa Dodoma na Taasisi ya Saratani Ocean Road. Alisema  kati ya wagonjwa 2,270 waliopatiwa matibabu 221 walipewa rufaa kuja kuti...

Mbunge Ghati Chomete Aahidi Kuendelea Kuiomba Fedha Serikali Kutekeleza Miradi

Na Shomari Binda-GMTV-Butiama  MBUNGE  wa viti maalum mkoa wa Mara Ghati Chomete amssema ataendelea kuusemea mkoa wa Mara na kuomba fedha serikalini kwa ajili ya utekelezaji wa miradi. Kauli hiyo ameitoa leo aprili 21,2025 Kata ya Bwiregi wilayani Butiama alipokuwa akiwasilisha utekelezaji wa ilani ya mwaka 2020/2025 kwenye Kata hiyo. Amesema katika kipindi cha utekelezaji wa ilanj ya kipindi hicho Kata hiyo imepokea zaidi ya bilioni 2 ambazo zimetekeleza miradi mbalimbali. Ghati amesema miradi iliyotekelezwa ni pamoja ya elimu,afya,maji na miundomninu ikiwa kufungua barabara. Mbunge huyo amesema kamwe hawezi kuwa bubu kwa kuongea kwaajili ya mkoa wa Mara katika utekelezaji wa miradi. Amesema licha ya kuongea kwa kipindi alichokaa bungeni amejua njia za kupita kutafuta fedha za utekelezaji wa miradi. " Nduhu zangu wana Bwiregi tuendelea kuishukuru serikali chini ya Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa namna anavuotupatia fedha mkoa wa Mara kwaajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali. ...