Skip to main content

Posts

Showing posts from November 26, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Msama Atoa Wito Kwa Wazazi, Viongozi wa Dini Kuwalinda Vijana Dhidi ya Vurugu

MKURUGENZI wa Msama Promotion, Alex Msama, ameetoa wito kwa wazazi nchini kukaa karibu na watoto wao na kuwashauri kuepuka ushawishi wa kujiingiza kwenye vitendo vya vurugu na misukumo isiyo na tija. Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Msama alisema wazazi wana jukumu kubwa la kuhakikisha vijana wanalelewa katika misingi ya maadili na uzalendo, kwa kuwa wao ndio wamewazaa na kuwalea. “Mimi kama mzazi niseme kuwa watoto ni wetu, tumewazaa na kuwalea. Tuna uwezo wa kukaa nao, kuzungumza nao na kuwaonya. Tusikubali waingie kwenye mkumbo wa kufanya vurugu,” amesema Msama. Amesisitiza kuwa hakuna mtu mwenye mapenzi ya dhati kwa Tanzania zaidi ya Watanzania wenyewe, hivyo ni muhimu kuepuka kufuata mkumbo usio na manufaa kwa taifa. “Amani tuliyonayo ni ya muhimu sana. Tumeachiwa na waasisi wetu, wazazi na mababu zetu. Tunapaswa kuilinda kwa nguvu zetu zote,” ameongeza. Msama aliwahimiza pia viongozi wa dini kuendelea kuzungumza na waumini pamoja na vijana kuhusu umuhi...

Wananchi Mikoa ya Iringa na Dodoma Kuwa na Umeme wa Uhakika-Mhe. Makamba.

📌Atembelea mradi wa kituo cha kuzalisha umeme cha Mtera 📌Awaasa wananchi kutunza mazingira ili kulinda vyanzo vya maji. 📌Zaidi ya Bilioni Kumi zimetumika kutekeleza miradi hii. Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Salome Makamba leo Novemba 26, 2025 ametembelea na kukagua mradi wa kuzalisha umeme kwa njia ya maji la Bwala la Mtera liliopo mpakani kati ya Iringa na Dodoma, ambapo amesema kuwa wananchi wa mikoa ya Dodoma na Iringa sasa kuwa na umeme wa uhakika. Mhe. Makamba amesema Mitambo ya kufua umeme imeboreshwa kwa kiasi kikubwa sana na mitambo hii inauwezo wa kuzalisha umeme mpaka ifikapo msimu ujao wa mvua na hii ni habari njema kwa wananchi wa wilaya ya Mpwapwa,Chamwino na Isimani . “ Kimsingi mitambo hii mara baada ya kuboreshwa inatuhakikishia kuwa umeme unapatikana wa kutosha hivyo kwa ujumla mikoa ya Dodoma na Iringa itakuwa na umeme  wa uhakika".Alisema Mhe. Makamba Aidha Mhe Makamba aliongeza kuwa juhudi hizi za Serikali lazima tumshukuru Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa...

Mbunge Mavunde Azindua Soko Dogo la Wafanyabiashara wa Mtaa wa Nzasa-dodoma Jiji

Mbunge wa Jimbo la Mtumba Mh. Anthony Mavunde leo asubuhi amefungua rasmi soko la wafanyabiashara wadogo la Mnyambugwe kwenye Mtaa wa Nzasa,kata ya Chihanga. Soko hilo ambalo limejengea kwa ufadhili wa shirika la VSO linatarajiwa kuwa na wafanyabiashara zaidi ya 100 ambao awali walikuwa wanafanya biashara zao katika maeneo ya wazi na hivyo kuathiriwa na mvua na jua. Akizungumza katika ufunguzi huo,Mbunge Mavundw amewashukuru wadau wa maendeleo VSO kwa ujenzi wa soko hilo la kisasa na kueleza kuwa ni mkakati wake kuhakikisha mitaa ya Jimbo la Mtumba inapata masoko ya aina hiyo ili kusaidia kuchochea uchumi wa maeneo hayo. Mbunge Mavunde pia ameishukuru serikali chini ya uongozi wa Mh Rais Dkt. Samia S. Hassan kwa mikopo isiyo na riba kwa wafanyabiashara hao ambayo imesaidia kuwaongezea mitaji ya kufanya biashara. Mbunge Mavunde pia ameahidi kuwapatia meza wafanyabiashara hao za kuwekea bidhaa zao ili zitunzwe katika hali ya usafi. Meneja Mradi wa VSO Ndg. Fortunatus Nyundo amesema shiri...

Dkt. Mwigulu Awaonya Wavunjifu wa Sheria

WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba amevitaka vyombo vinavyosimamia usalama barabarani vitekeleze sheria hizo bila upendeleo kwani tabia ya kuogopana na kuoneana aibu imechangia baadhi ya watu kukwepa wajibu wakati wengine wakibebeshwa mzigo wa sheria.  “Yeyote atakayevunja sheria akamatwe na hatua zichukuliwe kwa usawa. Huyu mmoja anavunja sheria anakamatwa, analipa. Huyu mwingine anavunja mbele yake anaachwa. Kama una haraka, toka mapema zaidi si kufidia kwa kuvunja sheria.” Ametoa kauli hiyo leo (Jumatano, Novemba 26, 2025) wakati akifungua Maadhimisho ya Kimataifa ya Wiki ya Usafiri Endelevu Ardhini katika ukumbi wa Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam. Amesema kuwa haitakuwa uungwana kuona baadhi ya watu wakilipa adhabu papo hapo wanapokosea ilhali wengine wakiachwa kupita bila kuchukuliwa hatua. Amewaonya baadhi ya viongozi na madereva wa Serikali ambao wanaelewa sheria vizuri lakini bado wanazikiuka kwa makusudi. “Ni muhimu kuwasaidia watumiaji wa vyombo vya usafiri kama...

Utafiti Wa Uanzishwaji Mgodi Mkubwa Wa Dhahabu Waanza Wilayani Hanang

▪️Waziri Mavunde aipongeza Kampuni kwa kukidhi masharti ya Leseni ya Utafiti ▪️Asimamia kwa vitendo lengo la kuongeza eneo la utafiti kutoka 16% hadi 50% ifikapo 2030* ▪️Ni utekelezaji wa maelekezo ya Mhe. Rais Samia ▪️Wananchi kunufaika kiuchumi na kijamii mradi ukianza kutekelezwa 📍 Manyara Waziri wa Madini, *Mhe. Anthony Mavunde (Mb)*, ametembelea na kushuhudia utekelezaji wa utafiti wa kina wa madini kwa kutumia teknolojia ya ndege nyuki (drone) katika Kata ya Basotu, Wilaya Hanang, mkoani Manyara. Utafiti huo wa jiofizikia unalenga kubainisha maeneo yenye hifadhi ya madini utakaopelekea kuanzishwa kwa mgodi mkubwa wa dhahabu wilayani humo. Ziara hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, *Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan* aliyoyatoa wakati akihutubia Bunge Oktoba 13, 2025 ambapo alitaja utafiti wa madini kama kipaumbele kwa mwaka 2025 - 2030 utakaopelekea kufikia angalau asilimia 50 ya utafiti wa kina wa madini nchini ifikapo mwaka 2...

CBE kuwa mhimili utekelezaji vipaumbele Wizara ya wizara ya Viwanda

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga  amekipongeza  Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), kwa kazi kubwa ya kuwaandaa vijana kujitegemea kwenye masuala ya biashara. Alitoa pongezi hizo alipotembelea chuo hicho jana kwaajili ya kujitambulisha katika mwendelezo wa ziara zake katika taasisi zilizo chini ya wizara yake. Alikipongeza chuo hicho kwa kusimamia vizuri ujenzi wa miundombinu ikiwemo ujenzi wa jengo la metrolojia ambalo ujenzi wake wa awamu ya kwanza umefikia asilimia 80 ya ujenzi wake Alisema miradi yote ya chuo iendelee kutekelezwa kwa weledi na ufanisi mkubwa na kuhakikisha inakamilika ndani ya muda wa mkataba uliosainiwa ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza. “Kwa kuwa miradi hii ni kwaajili ya kuongeza ufanisi basi sisi tunapenda ikamilike kwa haraka ili yale ambayo tunategemea yatatimia baada ya miradi hiyo basi yatimie, nimeona video nzuri ya CBE na nimesikiliza maelezo ya uongozi wa chuo nasisi tunamipango yetu kama Dira ya 2050 tunataka...

Wanunuzi wa Madini Wajipanga kwa Mnada Mkubwa Arusha

Arusha Wanunuzi wa madini kutoka maeneo mbalimbali nchini wameendelea kujitokeza katika Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC) jijini Arusha, wakikagua na kuhakiki ubora wa madini yatakayouzwa katika Mnada wa Tatu wa Madini ya Vito unaotarajiwa kufanyika tarehe 27 Novemba 2025. Ukaguzi huo ni hatua muhimu inayolenga kuhakikisha uwazi, ushindani na ongezeko la thamani ya madini nchini, kwa kuwa madini yote yatakayopatikana kwenye mnada huo wa kidigitali lazima yakidhi viwango na thamani halisi ya soko. Mnada huo umeendelea kuvutia wanunuzi wengi wa ndani, jambo linalopanua fursa za kibiashara na kuimarisha mchango wa sekta ya madini katika ukuaji wa uchumi wa taifa.  Aidha, unafungua milango kwa wachimbaji na wauzaji kuongeza wigo wa soko kupitia mfumo wa kisasa na salama wa uuzaji. Hatua hizi ni sehemu ya jitihada za Serikali kupitia Tume ya Madini kwa kushirikiana na Soko la Bidhaa Tanzania (TMX), kuhakikisha mifumo ya usimamizi na mauzo ya madini inakuwa ya kisasa na yenye tija kwa w...