Skip to main content

Posts

Showing posts from June 13, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Madawa mgeni rasmi maadhimisho ya miaka 21 ya Tahliso

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Juni 14, 2025 ni mgeni rasmi katika maadhimisho ya miaka 21 ya Jumuiya ya Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu, yanayofanyika katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma

Balozi Matinyi awasilisha Hati ya utambulisho kwa Mfalme wa Sweden

  Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mhe. Mobhare Matinyi, amewasilisha rasmi Hati za Utambulisho kwa Mfalme Carl XVI Gustaf, katika hafla maalum iliyofanyika tarehe 12 Juni, 2025, katika Kasri la Mfalme wa Sweden, jijini Stockholm.  Baada ya mazungumzo mafupi kwenye Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufalme wa Uswidi, Mhe. Balozi Matinyi alisindikizwa kwa gwaride rasmi kuelekea kwenye Kasri la Kifalme na kuwasilisha hati hizo kwa Mfalme Carl XVI Gustaf, ikiwa ni ishara rasmi ya kuanza kazi yake kama mwakilishi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Sweden. Katika mazungumzo yao mafupi, Mhe. Balozi Matinyi alimfikishia Mfalme Carl XVI Gustaf salamu za Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwake yeye binafsi pamoja na serikali na watu wa Uswidi. Mhe. Balozi Matinyi alimwelezea pia Mfalme Carl XVI Gustaf dhamira ya Tanzania ya kuendeleza na kuimarisha uhusiano mzuri wa kidiplomasia uliopo baina ya nchi hizi mbili na nia ya kukuza ushirikiano kati...

Kampuni yaandaa maonyesho ya watoto kuonyesha vipaji vyao

  Na Mwandishi Wetu KAMPUNI ya Maestro Africa Solutions Ltd, kwa kushirikiana na Peak Performance Company Ltd na Rehoboth Organization na The Ark Africa wameandaa Maonyesho Maalum ya Baby Market yatakayofanyika tarehe 28 mwezi huu katika Viwanja vya Sayansi, Kijitonyama, jijini Dar es Salaam Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Maestro Africa Solution, Amaris Mwako wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uzinduzi wa kampeni ya icare watoto kuhamasisha jamii kuwajali watoto. Amesema tukio hilo maalum limeandaliwa kwa lengo la kuwa One Stop Center kwa kila kitu kinachomhusu mtoto, kuanzia bidhaa, huduma hadi taarifa muhimu kutoka kwa Kampuni zinazohudumia watoto, Taasisi zinazojihusisha na ustawi wa mtoto na Shule za awali na msingi. Amesema tukio hilo linawalenga watoa huduma za afya na lishe kwa watoto, vifaa vya watoto, mavazi, michezo, elimu na zaidi! “Maonyesho Haya Yana Tofauti Gani? Haya siyo maonyesho ya kawaida tu. Ni jukwaa la watoto kuonyesha v...

Waziri Mkuu atembelea kituo cha malezi ya watoto Sanganigwa, Kigoma

  WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Juni 13, 2025 ametembelea kituo cha kulea watoto wenye uhitaji cha Sanganigwa kilichopo mjini Kigoma, kinachosimamiwa na Kanisa Katoliki jimbo la Kigoma. Akizungumza na watoto na walezi wa kituo hicho, Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inatambua mchango wa madhehebu ya dini katika kuwalea kimwili na kiroho watoto wenye mahitaji maalum nchini. “Kwa niaba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ninalishukuru kanisa katoliki jimbo la Kigoma, mtu mmoja mmoja na taasisi mbalimbali ambazo zimekuwa msaada mkubwa kwa Serikali katika kuwalea watoto wetu, hakika mnafanya jambo kubwa na lakumpenda Mungu na wanadamu” Akisoma taarifa ya kituo hicho kwa Waziri Mkuu, Mkurugenzi wa Kituo hicho Keneth Hageze amesema kuwa kilianzishwa mwaka 1995 na mpaka sasa kimehudumia watoto 1309. Mheshimiwa Majaliwa alitoa Mchele, Maharage, Mafuta, Sukari pamoja na Taulo za kike.

Jumanne Munema Atanganza nia Kugombea Ubunge Mbele ya Mbunge Mathayo

Na Shomari Binda-Musoma  KADA wa Chama cha Mapinduzi ( CCM) Jumanne Munema ametangaza nia ya kugombea ubunge jimbo la Musoma mjini mbele ya mbunge Vedastus Mathayo. Nia hiyo ameitangaza leo juni 13 2025 kwenye kikao kilichofanyika kwenye Kata ya Mwisenge wakati mbunge huyo akiwashukuru wana CCM kwa kumpa ushirikiano kwa kipindi cha uongozi wake unaokŵenda kumalizika. Akizungumza kwenye kikao hicho amesema yapo mambo mazuri yaliyofanywa na mbunge huyo ambayo yanastahiki kupongezwa. Munema amesema chama hakizuii mwanachama kugombea muda wa uchaguzi ukifika lakini pale yanapofanywa mazuri na mtangulizi hakuna budi kupongeza. Amesema ameamua kutia nia ya kugombea ubunge ili kuendelea kusaidiana kuleta maendeleo ndani ya jimbo la Musoma mjini. " Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni mbunge wetu Vedastus Mathayo yapo mazuri ambayo ameyafanya. " Musoma ile ya zamani sio Musoma hii ya leo yapo Mambo yamefanyika na kila mwana CCM anapaswa kutembea kifua mbele",amesema. Munema ...

Majaliwa: Tutaendelea Kuwalinda Na Kuwapatia Fursa Stahiki Watu Wenye Ulemavu

_▪️Asema hadi kufikia Machi, 2025 shilingi bilioni 5.48 zimetolewa kwa vikundi 891 vya Watu Wenye Ulemavu Nchini._ _▪️Azindua Programu janja ya usajili ya wenye ualbino ‘Albino Mobile App’._ _▪️Awataka Watanzania kutowaficha watoto wenye ulemavu._ _▪️Asisitiza kununuliwa kwa vifaa saidizi kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum wakiwemo wenye ualbino_   WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inawathamini Watu wenye Ulemavu wakiwemo wenye ualbino na wakati wote itahakikisha inawalinda na kuwapatia fursa stahiki katika ujenzi wa Taifa. Amesema katika kuendelea kutekeleza mpango wa uwezeshaji wananchi kiuchumi kwa kutumia mikopo inayotokana na mapato ya ndani ya Halmashauri, hadi kufikia Machi, 2025 tayari shilingi bilioni 5.48 zimetolewa kwa vikundi 891 vya Watu Wenye Ulemavu nchini. Amesema kuwa Serikali itaendelea kuchukua hatua mahsusi za kuimarisha ustawi na utoaji huduma kwa watu wenye ualbino ikiw...

Dc Chikoka Apokea Maaada wa Mabati Kutoka Nyansaho Foundation

Na Shomari Binda-Musoma  TAASISI ya maendeleo ya Nyansaho Foundation imetoa msaada wa mabati 130 ya rangi yenye kiasi cha zaidi shilingi milioni 7 ili kusaidia kuezeka shule ya sekondari Rukuba. Msaada huo umekuja kutoka taasisi hiyo kupitia wito wa mbunge wa jimbo la Musoma Vijijini Profesa Sospeter Muhongo kuomba wadau mbalimbali kushiriki maendeleo ya elimu kwenye jimbo hilo. Akipokea msaada huo Mkuu wa Wilaya ya Musoma Juma Chikoka ameishukuru taasisi hiyo kwa kutambua umuhimu wa elimu na kuamua kusaidia. Amesema zipo taasisi nyingi lakini Nyansaho Foundation imekuwa mfano wa kuigwa katika kusaidia na kutoa misaada kwa jamii ikiwemo ya kielimu. Chikoka amesema shule hiyo itakapokamilika kwa asilimia mia moja itasaidia wanafunzi kupata elimu na kutovuka maji kwenda kupata elimu nchi kavu. Mkuu huyo wa Wilaya amemshukuru mkurugenzi wa taasisi hiyo Dkt.Rhimo Nyansaho kwa msaada huo ambao kupitia wanafunzi kusoma inakuwa ni baraka kwa mkurugenzi huyo. " Hili ni jambo la baraka lil...

Ajali 5 za ndege mbaya zaidi kuwahi kutokea duniani

Simanzi nzito imetanda nchini India kufuatia ajali mbaya ya ndege ya Air India, iliyokuwa ikielekea London na kubeba watu 242, iliyoanguka Alhamisi, Juni 12, muda mfupi baada ya kuruka kutoka Uwanja wa Ndege wa Ahmedabad, magharibi mwa India. Maafa haya yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 200, na taarifa za awali zikibainisha kuwa miili 204 imepatikana. Kiasi cha waliokuwa ndani ya ndege na waliokuwa chini wakati waanguko ulipotokea bado hakijafahamika, huku uchunguzi ukiendelea kubaini ukubwa kamili wa janga hili. Ndege hiyo ilianguka kwenye makazi yaliyotumiwa na madaktari, na simulizi ya mwanamke mmoja anasema mwanaye alivyonusurika baada ya kuruka kutoka dirishani ghorofa ya pili, baada ya ndege hiyo kuangukia makazi. Katika ndege hiyo walikuwepo raia 169 wa India, Waingereza 53, Wareno saba na Mkanada mmoja. Ajali hii ya kushtua inaongeza kwenye orodha ndefu ya matukio mabaya katika historia ya usafiri wa anga, ikikumbusha ulimwengu juu ya hatari zilizopo licha ya maendeleo makub...