Skip to main content

Posts

Showing posts from February 3, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Iringa fursa za madini zipo njooni – Mhandisi Milandu

 *Iringa fursa za madini zipo njooni – Mhandisi Milandu* *Yakaribia 60% ya lengo ukusanyaji maduhuli kwa mwaka 2024/2025* *Yaita wawekezaji wakubwa kuwekeza Sekta ya Madini* MAKUSANYO  ya maduhuli ya Serikali kupitia Sekta ya Madini katika Mkoa wa Iringa yatokanayo na mrahaba, tozo na ada mbalimbali kwa mwaka wa fedha  2024/2025 yamefikia shilingi  milioni 698.05 ikiwa ni asilimia 58.2 ya lengo walilowekewa. Akizungumza katika mahojiano maalum, Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Iringa, Mhandisi AbdulRahman Milandu amesema Mkoa wa Iringa umewekewa lengo la kukusanya Shilingi Bilioni 1.2. “Mwaka huu wa fedha mpaka sasa  tunakaribia  asilimia 60, tumekusanya shilingi milioni 698.05 zaidi ya nusu ya lengo, hii inaonyesha fursa zipo,” amesema na kuongeza, Aidha, Mhandisi Milandu ametoa wito kwa wawekezaji wote nchini kuchangamkia fursa za uwekezaji zilizopo katika Sekta ya Madini mkoani Iringa ambapo mkoa huo umebarikiwa kuwa na madini ya aina mbalimbali ikiwemo dha...

Tshisekedi na Kagame Kukutana Dar-es-salaam Kujadili Mgogoro wa Mashariki Mwa Drc

Kongamano la dharura la pamoja baina ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), la kujadili hali ya usalama Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo limeratibiwa kufanyika Jumamosi wiki hii Jijini Dar es Salaam, Nchini Tanzania. Hii inafuatia makubaliano kati ya mwenyekiti wa SADC ambaye pia ni Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa na mwenyekiti wa EAC, Rais William Ruto wa Kenya. Kulingana na taarifa hiyo, Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania, amekubali kuandaa kongamano hilo huku Marais Felix Tshisekedi wa Jamhuri ya Demokrasia ya Congo (DRC) na Paul Kagame wa Rwanda, wakithibitisha Ushiriki wao.  Vile vile, Rais Ruto amethibitisha kuwa amejadiliana na Marais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini, Yoweri Museveni wa Uganda, na Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia, huku wote wakitoa Uthibitisho wa Kuhudhuria kongamano hilo la dharura. Chanzo;KBC

Mbunge Mathayo azungumzia Mafanikio Utekelezaji wa ilani ya Ccm Jimbo la Musoma Mjini Mbele ya Wasira

Na Shomari Binda-Musoma  MBUNGE wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo amezungumzia utekelezaji wa ilank ya uchaguzi ya CCM mbele ya Makamu Mwenyekiti wa chama hicho taifa Stephine Wasira. Akizungumza kwenye ukumbi wa mikutano wa chama hicho zilizopo kẁenye ofisi za mkoa ikiwa ni muendelezo wa ziara ya makamu huyo wa chama amesema utekelezaji wa miradi ya maendeleo umetekelezwa ipasavyo. Amesema kwenye sekta ya elimu ilani imetekelezwa ikiwa ni pamoja na kujengwa kwa shule mpya na kupelekea kila mtoto anayetakiwa kwenda shule anapata nafasi hiyo. Mathayo amesema elimu ndio suala la msingi na kwa jimbo la Musoma mjini hawana deni na Rais Dkt.Ssmia Suluhu Hassan bali yeye ndio anawadai kumpa kura za kishindo kwenye uchaguzi sa mwaka 2025. Amesema licha ya utekelezwaji wa ilani suala la kiuchumi kwa wananchi bado ni changamoto kutokana na viwanda kufa na kumuomba Makamu Mwenyekiti kusaidia eneo hilo.  " Tunakupongeza Makamu Mwenyekiti kwa kuchaguliwa kwenye nafasi hiyo na tuna...

Mbunge Mathayo Azungumzia Mafanikio Utekelezaji wa Ilani ya Ccm Jimbo La Musoma Mjini Mbele ya Wasira

Na Shomari Binda-Musoma  MBUNGE wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo amezungumzia utekelezaji wa ilank ya uchaguzi ya CCM mbele ya Makamu Mwenyekiti wa chama hicho taifa Stephine Wasira. Akizungumza kwenye ukumbi wa mikutano wa chama hicho zilizopo kẁenye ofisi za mkoa ikiwa ni muendelezo wa ziara ya makamu huyo wa chama amesema utekelezaji wa miradi ya maendeleo umetekelezwa ipasavyo. Amesema kwenye sekta ya elimu ilani imetekelezwa ikiwa ni pamoja na kujengwa kwa shule mpya na kupelekea kila mtoto anayetakiwa kwenda shule anapata nafasi hiyo. Mathayo amesema elimu ndio suala la msingi na kwa jimbo la Musoma mjini hawana deni na Rais Dkt.Ssmia Suluhu Hassan bali yeye ndio anawadai kumpa kura za kishindo kwenye uchaguzi sa mwaka 2025. Amesema licha ya utekelezwaji wa ilani suala la kiuchumi kwa wananchi bado ni changamoto kutokana na viwanda kufa na kumuomba Makamu Mwenyekiti kusaidia eneo hilo.  " Tunakupongeza Makamu Mwenyekiti kwa kuchaguliwa kwenye nafasi hiyo na tuna...

Wasira atembelea Kaburi la Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere Kijijini Butiama

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndg. Stephen Wassira ametembelea kaburi la Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Butiama, leo Februari 3, 2025 akiwa ziarani mkoani Mara ambapo pia amezungumza na wazee wa Butiama.