▪️Aelekeza shughuli za uchimbaji madini kusimama kipindi hichi cha Masika kama ilivyoelekezwa na NEMC ▪️ Timu ya Wataalam kufanya tathmini kwa kina na kutoa taarifa ya athari ya Mazingira ▪️Akemea wananchi kuharibu mali za mwekezaji ▪️Asisitiza Sheria na kanuni kufuatwa 📍Chunya,Mbeya Waziri wa Madini, *Mh.Anthony Mavunde (Mb)* amesimamisha shughuli za uchimbaji zilizokuwa zikifanywa na kampuni ya G & I Tech Mining Company Ltd kwa kipindi hichi cha masika na pia mpaka pale tathmini ya kitaalam ya mazingira itapokamilika juu ya shughuli za uchimbaji madini kwenye Mto Zila. Ameyasema hayo Jana tarehe 30 Desemba, 2024 katika kijiji cha Ifumbo, Wilayani Chunya alipotembelea eneo la leseni ya mwekezaji ambalo lilivamiwa na wananchi na kusababisha mgogoro mkubwa na uharibifu wa mali za mwekezaji huyo. "Tumetembelea maeneo yote mawili, na sote tumejionea hali halisi ya mazingira. Ni dhamira na maelekezo ya *Mh Rais Dkt. Samia S. Hassan* kuona shughuli zote za kiuchumi hususan za madi...
Marato tv - Sauti ya Jamii