*Na MASHAKA MHANDO, Tanga* RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amepokea kwa majonzi makubwa kifo cha nguli wa muziki wa dansi nchini, Hayati Stephen Hiza (80), aliyetunga na kuimba wimbo wa kitaifa wa uzalendo, *"Tanzania Nchi ya Furaha."* Hayati Mzee Hiza amehifadhiwa leo, Februari 18, 2026, katika nyumba yake ya milele eneo la Mwanzange, jijini Tanga. Akiwa na historia iliyotukuka, Mzee Hiza atakumbukwa kwa utunzi wake uliotikisa Radio Tanzania (RTD) mwaka 1967 akiwa na bendi kongwe ya *Atomic Jazz ya Tanga*, akizalisha vibao vilivyodumu vizazi na vizazi kama *"Leo Nakupasulia"*, *"Hamida Wangu"*, na *"Sitamani Kitu"*. *Alama ya Mwaka 1967 na Uzalendo* Wimbo uliompa heshima ya kipekee na kumfanya atambulike kama "Mzalendo Namba Moja" wa sanaa ni *"Tanzania Nchi ya Furaha"*. Wimbo huu, uliotungwa miaka sita tu baada ya Uhuru, umekuwa utambulisho wa amani na furaha ya Watanzania, jambo ambal...