Skip to main content

Posts

Showing posts from November 21, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Afanya Mazungumzo na Rais wa Zanzibar

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa ushindi wa kishindo aliyoupata katika Uchaguzi Mkuu, Oktoba 2025. Makamu wa Rais ametoa pongezi hizo wakati akizungumza na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, mazungumzo yaliyofanyika Ikulu Zanzibar. Amesema ushindi huo ni matokeo ya kazi kubwa aliyofanya Dkt. Mwinyi pamoja na Chama Cha Mapinduzi katika kipindi cha miaka mitano iliyopita. Kwa upande wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amempongeza Makamu wa Rais Dkt. Nchimbi, kwa kushika wadhifa huo, na kumuhakikishia kuendelea kufanya kazi kwa karibu na Ofisi ya Makamu wa Rais katika kutafuta ufumbuzi wa masuala mbalimbali ya kimuungano. Makamu wa Rais Dkt. Nchimbi, amefanya mazungumzo na Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi  kwa lengo la...

Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Afanya Mazungumzo na Rais wa Zanzibar

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa ushindi wa kishindo aliyoupata katika Uchaguzi Mkuu, Oktoba 2025. Makamu wa Rais ametoa pongezi hizo wakati akizungumza na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, mazungumzo yaliyofanyika Ikulu Zanzibar. Amesema ushindi huo ni matokeo ya kazi kubwa aliyofanya Dkt. Mwinyi pamoja na Chama Cha Mapinduzi katika kipindi cha miaka mitano iliyopita. Kwa upande wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amempongeza Makamu wa Rais Dkt. Nchimbi, kwa kushika wadhifa huo, na kumuhakikishia kuendelea kufanya kazi kwa karibu na Ofisi ya Makamu wa Rais katika kutafuta ufumbuzi wa masuala mbalimbali ya kimuungano. Makamu wa Rais Dkt. Nchimbi, amefanya mazungumzo na Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi  kwa lengo la kujita...

Dondoo ya Yaliyojiri Wakati wa Mkutano wa Hadhara Wa Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba, Uliofanyika Katika Uwanja wa Bombadia, Singida

▪️Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anawasalimia Wana Singida na anawapongeza kwa kazi kubwa ya ujenzi wa Taifa. ▪️Mradi wa SGR ni wa kimkakati una manufaa kwa Taifa letu, ni uti wa mgongo wa Taifa letu, hapa Singida tutanufaika na mradi huu. ▪️Katika Siku 100 Rais Dkt. Samia ameweka vipaumbele ikiwemo kuanza kwa utaratibu matumizi ya Bima ya Afya kwa wote, anataka jambo hili lianze haraka. ▪️Sisi wasaidizi tutafuatilia kwa karibu ahadi zote za Rais Dkt. Samia, tutafuatilia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi pamoja na kufuatilia miradi yote ya maendeleo ili kuwanufaisha Watanzania, ▪️Watumishi wa Umma wanaowasumbua Watanzania hawatakuwa na nafasi, haiwezekani mwananchi anaenda kwenye ofisi ya umma anatarajia apate ufumbuzi na huduma ila anafika pale anazungushwa, huu siyo uelekeo wa Rais Dkt. Samia anaotaka. ▪️Rais Dkt. Samia ametoa vitendea kazi anataka kuona Watanzania wanahudumiwa kwa ufanisi, Mwananchi akifika  ofisini msikilize, weka kumbukumbu kisha fanyia ka...

Waajiriwa Wapya wa Tume Ya Madini Watakiwa Kuzingatia Maadili, Kuepuka Vishawishi

Dodoma WAAJIRIWA wapya wa Tume ya Madini wametakiwa kufuata kikamilifu miongozo, kanuni na taratibu za utumishi wa umma, sambamba na kudumisha maadili na uadilifu wanapoanza kutekeleza majukumu yao. Wito huo umetolewa leo, Novemba 21, 2025, na Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Ramadhani Lwamo, wakati akifungua mafunzo ya awali kwa watumishi hao yaliyofanyika katika Ukumbi wa Graphite, Makao Makuu ya Tume jijini Dodoma. Akizungumza katika mkutano huo, Mhandisi Lwamo amesisitiza umuhimu wa watumishi hao wapya kujiepusha na vishawishi vinavyoweza kuhatarisha uadilifu wao katika sekta ya madini. “Sekta ya madini ina vishawishi vingi. Mara nyingi wafanyabiashara wanatafuta njia za kupata faida kubwa. Kwenye dhahabu kuna masuala ya ubora na usafi (quality na purity). Msikubali kushawishiwa kwa vijisenti ambavyo vinaweza kuwatia hasara baadaye,” amesema. Ameongeza kuwa Tume haitavumilia aina yoyote ya mwenendo usio wa uadilifu: “Epukeni tamaa za mafanikio ya haraka. Mmefundishwa maa...

Tanzania Yajipanga Kuzalisha Bidhaa Zitokanazo na Madini Nchini

▪️Ni maelekezo ya Mhe.Rais Samia ya uongezaji thamani madini nchini ▪️Waziri Mavunde akagua ujenzi wa kiwanda cha kusindika na kuyeyusha madini ya Nikeli na Shaba ▪️Kiwanda kuanza uzalishaji Februari,2026 ▪️Wachimbaji wadogo wapata soko la uhakika wa kuuza malighafi kiwandani ▪️Mradi kugharimu Bilioni 37 *Dodoma* Tanzania yaendelea kupiga hatua katika Mpango wa ujenzi wa viwanda vya uongezaji thamani madini kutokana na ujenzi wa kiwanda kipya cha usindikaji  na uyeyushaji madini ya Nikeli na Shaba kufikia asilimia 85 ya ujenzi ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa maelekezo ya Mhe.Rais .Dkt.Samia Suluhu Hassan yanayoelekeza kuwa shughuli za uongezaji thamani madini kufanyika ndani ya nchi kabla ya kusafirishwa nje. Hayo yameelezwa leo Novemba 21, 2025 na Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde wakati anakagua kiwanda cha kusindika  na kuyeyusha madini ya Nikeli na Shaba kilichopo eneo la Mayamaya , Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma. Mhe.Mavunde amesema kuwa, kiwanda kitawasha mtambo wake...

Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Aagiza Mkandarasi Kukamatwa na Kuzuia Hati Yake

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, ameelekeza Jeshi la Polisi na Uhamiaji kuhakikisha wanamkamata na kuzuia hati ya kusafiria ya mkandarasi anayejenga mradi wa Kituo cha ukaguzi cha Pamoja kilichopo Muhalala mkoani Singida. Dkt. Mwigulu amesema kuwa mkandarasi huyo aliaminiwa na Serikali kwa kupewa ujenzi wa mradi huo wa kimkakati uliosimama kwa zaidi ya miaka nane tangu mwaka 2016. Mradi huo unaojengwa na kampuni ya Impresa di Costruzioni Ing. E. Mantovani S.p.A ulipaswa kukamilika mwaka 2018. Ametoa agizo hilo leo Ijumaa tarehe 21 Novemba, 2025 wakati alipokagua mradi huo katika ziara yake ya kikazi mkoani Singida ambapo atakagua miradi ya maendeleo pamoja na kuzungumza na wananchi. Mheshimiwa Dkt. Mwigulu amesema kuwa jitihada zimefanyika za kuona mradi huo unaendelea lakini mkandarasi amekuwa akileta ugumu katika utekelezaji “Mkandarasi huyu alitangazwa amefilisika na hawezi kuendelea na mradi na alielekezwa ailipe fidia Tanzania kwasababu ameiche...