Na Mwandishi wetu - Msumbiji TANZANIA inaandaa Mpango wa Kitaifa wa Hatua za Mapema za kujiandaa, kukabiliana na ukame kwa maeneo yanayokabiliwa na janga hilo kwa kushirikiana na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), ikiwa ni jitihada za kupunguza athari za janga hilo nchini. Hatua hiyo inaonesha dhamira ya serikali kuachana na utaratibu wa kusubiri madhara yatokee ndipo ichukue hatua, na badala yake kuelekea katika usimamizi wa hatari unaozingatia maandalizi na tahadhari za mapema. Hayo yameelewa na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu Dkt. Jim Yonazi, katika ziara ya kubadilishana uzoefu kati ya Tanzania na Msumbiji kuhusu hatua za mapema kabla ya majanga unaoendelea kwa siku tano kuanzia tarehe 25 hadi 29 Mei, 2026 Mjini Maputo Msumbiji. Alisema ukame una madhara makubwa katika kilimo, mifugo, rasilimali za maji, usalama wa chakula, maisha ya wananchi, maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa ujumla. “Kwa sasa Tanzania inaendelea kuandaa Mpango ...
Marato tv - Sauti ya Jamii