Skip to main content

Posts

Showing posts from February 2, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Wahandisi wa Umwagiliaji Nchini Watakiwa Kuimarisha Usimamizi wa Miradi

_Apongeza NIRC kwa kuimarisha uwezo kupitia mafunzo ya Usimamizi wa Mikataba, Sheria, Ununuzi na Utafiti wa Miamba_ 📍 NIRC – Iringa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Bw. Gerald Mweli, amewataka Wahandisi wa Umwagiliaji nchini kuachana na kufanya kazi kwa mazoea na badala yake kutumia mbinu bunifu na uzoefu wa kitaalamu katika kusimamia miradi ya umwagiliaji, ili kuhakikisha miradi hiyo inaleta tija kwa Taifa. Akifungua mafunzo ya usimamizi wa mikataba, sheria za ununuzi na utafiti wa miamba katika mabwawa mkoani Iringa, Bw. Mweli aliwataka wahandisi kufuta dhana ya kukariri kwa kuwa usimamizi wa wakandarasi unahitaji mbinu za ziada na kubadilishana uzoefu miongoni mwa wataalamu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji na wadau wengine. “Utatuzi wa changamoto za miradi haujawahi kuandikwa wote kwenye makaratasi. Mara nyingine unakutana na mkandarasi mbishi, hapo ndipo unahitaji kuzungumza na mhandisi mwenzako aliyejua jinsi ya kumdhibiti. Msikae kama mnaogopana, kaeni pamoja mbadilishane mbinu z...

Hospitali ya Kairuki Yawachunguza Afya Bure Wananch 500

....Ni sehemu ya kumbukizi ya miaka 27 ya kifo cha Profesa Hubert Kairuki  Na Mwandishi Wetu ZAIDI ya wananchi 500 wamepatiwa huduma ya uchunguzi wa maradhi mbalimbali na ushauri wa bure katika siku ya kwanza ya kambi hiyo katika hospitali ya Kairuki iliyoko Mikocheni jijini Dar es Salaam. Naibu Mkurugenzi wa hospitali hiyo, Dk Muganyizi Kairuki amesema leo kuwa  wameamua kutoa huduma hizo bure kama sehemu ya kumuenzi mwasisi wa hospitali hiyo, Hayati Profesa Hubert Kairuki aliyefariki miaka 27 iliyopita. Alisema huduma hiyo ya uchunguzi inafanyika katika hospitali hiyo na kituo chao cha matibabu kilichoko katika Kituo cha Mabasi cha Magufuli Mbezi jijini Dar es Salaam. Dk Muganyizi alitaja baadhi ya huduma zinazotolewa kwenye kambi hiyo kuwa ni pamoja na uchunguzi wa uvimbe katika tezi dume, uzimbe katika kizazi, uvimbe kwenye uvimbe kwenye matiti. Alisema katika siku ya kwanza pekee idadi ya waliojitokeza imekuwa kubwa kupita kawaida lakini walifanikiwa kuwafanyia uchunguzi ...

Mradi wa majiko banifu watambulishwa Geita

📌 *Majiko banifu 11,022 kusambazwa na kuuzwa kwa bei ya ruzuku mkoani Geita*  📌 *Wilaya tano (5) kunufaika na mradi*  📍 *Geita*  Serikali ya Geita kupitia Kaimu katibu tawala wa mkoa wa Geita ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya Mipango na Uratibu, Ndugu Deodatus Kayango leo Februari 02, 2026 imepokea mradi wa mradi na utafuta wa majiko banifu kwa bei ya ruzuku. Sauti wakati wa utoaji wa taarifa ya mradi, Mhandisi Mwandamizi kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Deusdedit Malulu amesema, Serikali kupitia REA imekuja na mpango wa kutafuta na matumizi ya majiko banifu kwa bei ya ruzuku ambao unatumia ufanisi za kiafya na mazingira zitokanazo na matumizi ya nishati salama ya kupikia. Aidha, kuuza na kuuza wa majiko haya banifu ni ya kutekeleza mkakati wa kitaifa wa sehemu ya matumizi safi ya watu wengi zaidi mpaka ifikapo 2034 zaidi ya asilimia themanini 80% ya watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia. Halikadhalika, katika eneo hilo Wakala wa Nishati Vijijini unat...