Skip to main content

Posts

Showing posts from August 16, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

MV Liemba Returns: Professor Mbarawa Leads First Trials After Major Overall

By Prosper Makene  KIGOMA — The horn of MV Liemba echoed across Lake Tanganyika again over the weekend for the first time in more than eight years, as Minister for Transport Prof. Makame Mbarawa led the first phase of technical  trials of the newly rehabilitated vessel.  The moment marked the beginning of what the government is calling "50 years of new voyages" for the 111-year-old ship that has for generations connected Tanzanian communities to each other and to their neighbors in Burundi, Zambia, and the Democratic Republic of Congo. The TSh 34 billion rehabilitation, fully funded by the government, has transformed the historic vessel while preserving its heritage. With testing now underway, officials say MV Liemba will resume commercial operations on September 1st this year. Minister Mbarawa boarded the ship in Kigoma to witness the start of trials, which he said are being conducted in two phases to ensure the vessel meets both national and international safety standar...

Waziri wa Uchukuzi Ashuhudia Majaribio ya MV Liemba kuashiria miaka 50 ya safari mpya Baada ya Matengenezo Makubwa

Na Prosper Makene  Meli kongwe ya Mv Liemba iliyosimama kazi kwa zaidi ya miaka nane, imeanza rasmi majaribio ya kiufundi baada ya serikali kutumia shilingi bilioni 34 kufanya ukarabati na uwekezaji katika meli hiyo, inayotarajiwa kuanza safari zake September Mosi mwaka huu ikihudumia nchi jirani za Burundi, Zambia na Congo DRC. Akizungumza baada ya kufanya majaribio ya meli hiyo Waziri wa Uchukuzi Makame Mbarawa, alisema majaribio yatafanyika kwa awamu mbili jana ikiwa ni awamu ya kwanza, kabla ya majaribio ya awamu ya mwisho yatakayofanyika kati ya tarehe 19-21 Agosti mwaka huu lengo ikiwa kupima mifumo muhimu kabla ya kuanza kwake. ‘Meli ya Mv Liemba itatumika miaka 50, ikifanyiwa matengenezo ya mara kwa mara itadumu zaidi ya miaka 80, leo tumeangalia ubora wa vifaa vyote na namna itakavyoweza kumudu kipindi cha dharura”, alisema Mbarawa. Alisema meli hiyo imefanyiwa majaribio kwa viwango vya kimataifa, na baada ya hapo atakuja Wakala wa Meli Tanzania (TASAC) ili kujiridhisha ju...

MV LIEMBA RETURN: PROFESSOR MBARAWA LEADS FIRST TRIAL AFTER MAJOR OVERRALL

  By Prosper Makene  KIGOMA — The horn of MV Liemba echoed across Lake Tanganyika again over the weekend for the first time in more than eight years, as Minister for Transport Prof. Makame Mbarawa led the first phase of technical  trials of the newly rehabilitated vessel.  The moment marked the beginning of what the government is calling "50 years of new voyages" for the 111-year-old ship that has for generations connected Tanzanian communities to each other and to their neighbors in Burundi, Zambia, and the Democratic Republic of Congo. The TSh 34 billion rehabilitation, fully funded by the government, has transformed the historic vessel while preserving its heritage. With testing now underway, officials say MV Liemba will resume commercial operations on September 1st this year. Minister Mbarawa boarded the ship in Kigoma to witness the start of trials, which he said are being conducted in two phases to ensure the vessel meets both national and international safety ...

WAZIRI WA UCHUKUZI ASHUHUDIA MAJARIBIO YA MV LIEMBA KUASHURIA MIAKA 50 YA SAFARI MPYA BAADA YA MATENGENEZO MAKUBWA

  Na Prosper Makene  Meli kongwe ya Mv Liemba iliyosimama kazi kwa zaidi ya miaka nane, imeanza rasmi majaribio ya kiufundi baada ya serikali kutumia shilingi bilioni 34 kufanya ukarabati na uwekezaji katika meli hiyo, inayotarajiwa kuanza safari zake September Mosi mwaka huu ikihudumia nchi jirani za Burundi, Zambia na Congo DRC. Akizungumza baada ya kufanya majaribio ya meli hiyo Waziri wa Uchukuzi Makame Mbarawa, alisema majaribio yatafanyika kwa awamu mbili jana ikiwa ni awamu ya kwanza, kabla ya majaribio ya awamu ya mwisho yatakayofanyika kati ya tarehe 19-21 Agosti mwaka huu lengo ikiwa kupima mifumo muhimu kabla ya kuanza kwake. ‘Meli ya Mv Liemba itatumika miaka 50, ikifanyiwa matengenezo ya mara kwa mara itadumu zaidi ya miaka 80, leo tumeangalia ubora wa vifaa vyote na namna itakavyoweza kumudu kipindi cha dharura”, alisema Mbarawa. Alisema meli hiyo imefanyiwa majaribio kwa viwango vya kimataifa, na baada ya hapo atakuja Wakala wa Meli Tanzania (TASAC) ili kujiridh...

SERIKALI YAPONGEZA UBUNIFU WA WANAFUNZI CHUO CHA ST JOSEPH

  Na Mwandishi Wetu SERIKALI imesema itashirikiana na vyuo binafsi kuhakikisha masomo hayo ya sayansi  yanapewa kipaumbele ili wapatikane wahandisi wengi nchini na kuondoa utegemezi wa kutegemea wataalamu wa kigeni. Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mipango na Uwekezaji), Profesa Kitila Mkumbo, wakati akizungumza kwenye wiki ya tafiti na ubunifu ya Chuo cha St Joseph cha jijini Dar es Salaam. Alisema chuo hicho kwa muda mrefu kimekuwa mstari wa mbele kutoa wataalamu wa sayansi na alikitaka kuhakikisha kinaendelea kuchukua nafasi yake ya kuongoza mwa vyuo vinavyotoa wataalamu wengi wa fani ya sayansi hapa nchini. Waziri Mkumbo alisema ametembelea maonesho ya kitaaluma ya wanafunzi wa chuo hicho na kubaini kuwa wanafunzi hao wamemudu kubuni vitu mbalimbali ambavyo vinaweza kuwa na manufaa kwa taifa. “Nimejionea ubunifu mkubwa sana kwa wanafunzi wenu lakini kinachosikitisha ni kuwa ubunifu huo unaishia kuwa wazo tu haufikii mwisho kwa hiyo nawapa c...

MUWASA YATEMBELEA MAENEO YALIYOKOSA HUDUMA YA MAJI.

Na Mwandishi wetu Jovina Massano. Katika kuhakikisha  huduma bora ya maji inaimarika Mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira Musoma (MUWASA) yatembelea maeneo yaliyopata upungufu wa huduma ya  maji sambamba  na kusikiliza kero zinazowakabili wateja wake. Zoezi hilo ni mojawapo ya kudumisha mahusiano na mawasiliano kwa wateja wa MUWASA likiongozwa na timu kutoka Idara ya usambazaji maji na usafi wa mazingira wakiwemo kitengo cha mahusiano. Wateja hao wameshukuru ujio wa wataalam hao huku wakipongeza kurejea kwa huduma ya maji, lakini wameiomba mamlaka hiyo kuongeza jitihada za kuhakikisha huduma hiyo muhimu inapatikana kwa uhakika. Sanjari na hayo wameiomba MUWASA kujitahidi kutoa taarifa mapema ili pale kunapotokea changamoto inayosababisha maji kukatika au kupungua,  wajiandae na kuchukua hatua za dharura wakati wakisubiri huduma kurejea. Vilevile wameiomba Wizara husika kuboresha miundombinu ili iweze kwenda sambamba na  mabadiliko ya uhitaji kwa kuwa wateja...

TRA IMEANZA VIZURI MAKUSANYO JULAI, 2026, WANANCHI TUENDELEZE UAMINIFU ULIPAJI KODI

  NA: DK. REUBENI LUMBAGALA  Katika maisha ya kawaida ya mwanadamu, kuna kuweka malengo ili kufikia mafanikio. Inapotokea malengo yametimia, moyo hujaa furaha kwani mlango wa kufanikiwa unakuwa umefunguka. Haya ndiyo yaliyotokea kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Kwa TRA, mwaka wa fedha 2026/2027 umeanza vizuri. Hii ni kufuatia Mamlaka hiyo kukusanya shilingi trilioni 3.245 kwa mwezi Julai, 2026, ambapo makusanyo hayo ni sawa na asilimia 109 ya lengo la kukusanya trilioni 2.971 kwa mwezi huo. Ni kwamba; mwaka mpya wa fedha huanza Julai 1 ya kila mwaka. Hivyo mwezi wa kwanza wa mwaka mpya wa fedha ni kuanzia Julai 1 hadi 31. Kwa malengo ambayo TRA ilijiwekea, ni kukusanya shilingi trilioni 2.971, lakini lengo hilo limetimia na kuzidi, ambapo zimekusanywa shilingi trilioni 3.245.  Kimsingi, bajeti iliyopitishwa na bunge kwa mwaka wa fedha 2026/2027 ni shilingi trilioni 62.33, ambapo asilimia 74 ya fedha hizo zinategemewa kukusanywa kupitia mapato ya ndani (own sources). ...