Skip to main content

Posts

Showing posts from May 9, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Serikali kuimarisha uwezo wa walimu wa michezo

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda, amesema Serikali inaendelea kuweka mikakati  ya kuboresha elimu ya michezo, pamoja na kuinua uwezo wa walimu wa fani hiyo hapa nchini, ili kuhakikisha wanafunzi wanapata maarifa bora kwa maendeleo ya vipaji vyao. Akizungumza  katika hafla ya usiku wa Tuzo kwa  Wanamichezo zilizoandaliwa na Baraza la Michezo la Taifa (BMT)  tarehe 9 Mei, 2026, Mhe.  Makonda amesema, kuna umuhimu wa kuendelea kuwajengea walimu uwezo kupitia programu maalum za mafunzo ili waendane na mahitaji ya sasa.  Ameeleza kuwa, hatua hiyo itasaidia walimu kuelewa vizuri mbinu za ufundishaji pamoja na kuwasaidia wanafunzi kutambua vipaji vyao katika michezo  mapema. "Serikali inalenga kuhakikisha walimu wanaopata nafasi ya kufundisha michezo  katika shule zetu wanakuwa na sifa na uelewa unaotakiwa ili kuongeza ubora wa elimu ya michezo.Tunaendelea kuboresha mazingira bora ya kazi, pamoja na motisha kwa walimu...

Magambo agusa sekta ya elimu Nyamatare, amuunga mkono Rais Dkt Samia kwa kujenga vyumba vitano vya madarasa

MKURUGENZI Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Fortunatus Magambo ameandika historia mpya katika Kata ya Nyamatare baada ya kujitolea kujenga vyumba vitano vya madarasa katika Shule ya Msingi Ring’wani, hatua inayotajwa kuwa mkombozi kwa wanafunzi wa shule hiyo. Bw. Magambo alifikia uamuzi huo baada ya kutembelea shule hiyo mwaka 2024 na kushuhudia hali ya uchakavu wa miundombinu pamoja na upungufu mkubwa wa madarasa uliokuwa ukiathiri mazingira ya kujifunzia kwa wanafunzi. “Nilipofika hapa niliguswa kuona watoto wakisomea katika mazingira magumu kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa. Nimeamua kushiriki kuboresha mazingira haya ili watoto wetu wapate sehemu bora ya kujifunzia,” amesema Bw. Magambo. Tayari kazi ya uchimbaji wa msingi pamoja na hatua za awali za ujenzi wa vyumba hivyo vitano imeanza, huku lengo likiwa ni kuhakikisha mradi huo unakamilika kabla ya Julai 2026 kuisha. Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Nyamatare, Mgaya Maheke amemshukuru Bw. ...

Rais Samia amefanya mageuzi makubwa katika Michezo -Dkt.Mwigulu

WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amechochea kufanyika  kwa mageuzi makubwa katika sekta ya michezo nchini. Amesema hayo leo Jumamosi (Mei 9, 2026) alipomwakilisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,  Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, katika hafla ya utoaji tuzo za michezo za Baraza la Michezo la Taifa  (NSCA), zilizofanyika kwenye ukumbi wa The Super Dom, Masaki jijini Dar es Salaam. Mheshimiwa Dkt. Mwigulu amesema Mheshimiwa Rais Samia amefanya mambo mengi yanayodhihirisha nia yake ya dhati ya kuendeleza michezo nchini. "Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya mageuzi makubwa kwenye michezo, kuanzishwa kwa mfuko wa maendeleo ya michezo ni miongoni mwa mambo makubwa kwenye sekta ya michezo." Amesema Waziri Mkuu Mwigulu. Waziri Mkuu ameongeza kwa kusema kuwa "Goli la mama na knock out ya mama vimeongeza ari kwa wanamichezo na vilabu vyetu vya Tanzania, kama mlivyoona timu zetu zimefanya vizuri...

SGR yatajwa kuchochea utalii na ukuaji wa uchumi

Abiria na wadau wa usafiri wa reli nchini wameeleza namna huduma ya reli ya kisasa ya Standard Gauge Railway (SGR) ilivyokuwa chachu ya maendeleo katika sekta mbalimbali ikiwemo utalii, biashara, usafirishaji wa mizigo, utunzaji wa mazingira pamoja na kuokoa muda kwa wananchi. Maoni hayo yametolewa wakati wa kampeni ya #NusuMudaKoteKote iliyoandaliwa na Shirika la Reli Tanzania (TRC) kwa lengo la kuadhimisha miaka miwili tangu kuanza kwa huduma ya SGR nchini. Wadau hao wamesema ujio wa reli hiyo umeleta mageuzi makubwa katika mfumo wa usafiri wa Tanzania kwa kutoa huduma ya kisasa yenye kasi, usalama na ufanisi mkubwa ukilinganisha na mifumo mingine ya usafiri. Katika kampeni hiyo, TRC imeeleza kuwa #NusuMudaKoteKote inalenga kuhamasisha matumizi ya reli ya kisasa ya SGR pamoja na kuonyesha mafanikio yaliyopatikana tangu kuanza kwa huduma hiyo miaka miwili iliyopita pamoja na kuonesha namna SGR ilivyopunguza muda wa safari, kuongeza ufanisi wa shughuli za wananchi na kuboresha huduma z...

Waziri Chongolo kutangaza bei ya Pamba kesho, Matumaini ya Wakulima Yapanda

WAZIRI wa Kilimo, Daniel Chongolo, anatarajiwa kutangaza bei elekezi ya Serikali kwa zao la pamba kesho Mei 10, 2026, katika uzinduzi rasmi wa msimu wa ununuzi wa pamba wa mwaka 2026/2027 utakaofanyika Kijiji cha Mwamashimba, Wilaya ya Igunga mkoani Tabora. Uzinduzi huo wa Kitaifa unaosimamiwa na Bodi ya Pamba Tanzania (TCB), umeamsha matarajio makubwa kwa maelfu ya wakulima wa zao hilo la kimkakati, huku wengi wakisubiri kwa hamu kusikia bei mpya itakayotoa mwelekeo wa msimu mpya wa kilimo na biashara ya pamba nchini. “Bei ya pamba ndiyo moyo wa mkulima, ikipewa thamani nzuri inaongeza nguvu ya uzalishaji na kuleta matumaini mapya ya maendeleo kwa familia nyingi,” amesema mmoja wa wakulima waliozungumza na waandishi wa habari za pamba na mazingira waliowasili wilayani Igunga. Wakulima hao wameeleza kuwa zao la pamba limeendelea kuwa uti wa mgongo wa uchumi katika maeneo mengi ya uzalishaji, wakiamini kuwa tangazo la Serikali litakuwa chachu ya kuongeza ari ya kilimo, tija na kipato kw...

Rais Samia akimsikiliza kwa makini mmoja wa wafungwa Tanzania

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mfungwa Bw.  Lista Chisoma ambaye amepata ujuzi wa kushona bidhaa mbalimbali za ngozi na vitambaa wakati akiwa gerezani, katika Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania (TCT) Ukonga Jijini Dar es Salaam tarehe 09 Mei, 2026.

Jeshi la Magereza latoa Tuzo kwa Rais Samia

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea Tuzo ya kuwa Kinara wa Dhana ya Urekebishaji wa Wafungwa Magerezani kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Patrobas Paschal Katambi kwenye hafla ya hafla ya kuhitimisha Mafunzo ya Uongozi Ngazi ya Juu Kozi namba 28 na Uongozi Daraja la Pili Kozi namba 48 ya mwaka 2025/2026 katika Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania (TCT) Ukonga Jijini Dar es Salaam tarehe 09 Mei, 2026. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi pamoja na wageni mbalimbali wakati wa kuhitimisha Mafunzo ya Uongozi Ngazi ya Juu Kozi namba 28 na Uongozi Daraja la Pili Kozi namba 48 ya mwaka 2025/2026 katika Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania (TCT) Ukonga Jijini Dar es Salaam tarehe 09 Mei, 2026.

Waziri Ndejembi aweka Jiwe la mwingi mradi wa Benaco-Kyaka

📌 Utawezesha Mkoa wote Kagera kuunganishwa na Gridi ya Taifa 📌 Zaidi ya Bilioni 270 kutumika kutekeleza mradi 📌 Mradi kukamilika ndani ya miezi 24 Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi leo Mei 9, 2026 ameweka jiwe la msingi la mradi wa njia ya kusafirisha umeme wa KV 220 Benaco–Kyaka pamoja na Kituo cha Kupoza Umeme cha Benaco wilayani Ngara, mkoani Kagera. ''Tunatarajia ndani ya miezi 24 Mkoa wa Kagera uwe umeunganishwa katika Gridi ya Taifa na changamoto za umeme ziwe historia,” alisema Mhe. Ndejembi. Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Ngara, Bw. Mathias Kahabi, akimwakilisha Mkuu wa Mkoa amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na Waziri wa Nishati kwa kuendelea kuwekeza katika miradi ya maendeleo ya umeme wilayani humo. Amesema katika Jimbo la Ngara vijiji vyote 75 tayari vimefikiwa na huduma ya umeme, huku vitongoji 219 kati ya vitongoji 389 vikiwa tayari vimeunganishiwa umeme. Akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi huo Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Bw. ...