Skip to main content

Posts

Showing posts from September 19, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

SISTER YOHANA AWASOGEZEA HUDUMA BODABODA MTAKUJA, AWAKABIDHI BANDA LA KUJIKINGA NA MVUA

 Kutokana na utabiri wa mvua kubwa zinazotarajiwa kunyesha nchini katika kipindi hiki cha mvua za El Niño, Diwani wa Viti Maalum wa Manispaa ya Musoma,Mh Sister Yohana, amewakabidhi waendesha bodaboda wa Kata ya Mwisenge eneo la Mtakuja banda maalum la kujikinga na mvua na jua wanapokuwa wakisubiri abiria. Banda hilo limejengwa katika viwanja vya Shule ya Msingi Mtakuja, Manispaa ya Musoma, ikiwa ni hatua ya kuwawezesha vijana hao kuendelea na shughuli zao za usafirishaji bila kuathiriwa na hali ya hewa, hususan wakati wa mvua. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa banda hilo, Sister Yohana amesema ameamua kutekeleza ujenzi huo kwa kutambua umuhimu wa kuwaunga mkono vijana wanaotegemea shughuli za bodaboda kujipatia kipato na kuendesha maisha yao. “Mimi kama Diwani wa Viti Maalum nimeamua kuwajengea kivuli vijana wa bodaboda wa Mtakuja, ambao ni majirani kabisa na nyumbani kwangu. Nimefanya hivi kwa kutambua juhudi za Serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan katika kuwajali na kuwawe...

AFISA ELIMU WILAYA YA BAGAMOYO AIMWAGIA SIFA SIFA SHULE YA MSINGI TWIBHOKI MKOA WA PWANI

 Afisa Elimu Msingi wa Wilaya ya Bagamoyo, Joseph Bureta, ameipongeza shule ya msingi na awali ya Twibhoki kwa kuendelea kufaulisha vyema wanafunzi katika masomo ya sayansi  Bureta amesema hayo leo Septemba 19, 2026 katika mahafali ya nne ya wanafunzi 14 wa Shule ya Msingi na Awali ya Twibhoki, iliyopo Bagamoyo mkoani Pwani, ambapo amewataka wahitimu kutumia ipasavyo elimu waliyoipata na kujiepusha na marafiki wenye tabia zinazoweza kukatisha ndoto zao za kielimu. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Shule hiyo, Issa Juma Kiango, amewataka wazazi wa wahitimu hao kuwa mabalozi wazuri wa shule kwa kuthamini elimu bora waliyoipata watoto wao na kuendeleza ushirikiano na uongozi wa shule. Naye Mkuu wa Shule ya Twibhoki, Peter Chacha, amempongeza Mkurugenzi wa shule hiyo, Grace Warioba, kwa kuendelea kutoa mchango katika maendeleo ya shule hiyo, huku akiwataka wahitimu kuwa wavumilivu na kukabiliana kwa ujasiri na changamoto mbalimbali zinazoweza kujitokeza katika safari yao y...

MAKAMU WA RAIS AZITAKA TAASISI ZA MUUNGANO KUIMARISHA USHIRIKIANO, HUDUMA KWA WANANCHI

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius John Ndejembi, amezitaka Taasisi za Muungano kuimarisha ushirikiano, kubaini na kutumia fursa zilizopo pamoja na kushiriki kwa pamoja katika shughuli mbalimbali ndani na nje ya nchi kwa lengo la kuongeza tija na kuleta manufaa zaidi kwa Watanzania.   Makamu wa Rais ametoa wito huo leo, Septemba 19, 2026 wakati akifungua kikao cha Wakuu wa Taasisi za Muungano kilichofanyika katika Ukumbi wa Golden Tulip, Zanzibar, na kuhudhuriwa na wakuu wa Taasisi 39 za Muungano.   Makamu wa Rais amewataka viongozi wa taasisi hizo kuelewa kwa kina wajibu wao katika kuwahudumia wananchi na kufanya kazi kwa mtazamo mmoja wa kujenga “nyumba moja”, huku maslahi ya Watanzania yakiwekwa mbele.   Amesema matarajio ya wananchi ni kuona Muungano na taasisi zake zikitoa matokeo yanayogusa maisha yao moja kwa moja, hususan katika kuboresha hali ya uchumi, afya, elimu na maeneo mengine muhimu ya kijamii.   Amezihimiza taasi...

WANAOTENGENEZA MAGARI YA SERIKALI TANGA WATAKIWA KUFATA SHERIA.

 Na Mwanamkuu Mwandoro, Tanga. Wamiliki wa gereji zenye vibali vya kutengeneza magari ya serikali mkoani Tanga wametakiwa kuacha mara moja tabia ya kupokea magari hayo ya serikali na kuyafanyia Matengenezo bila kuwa na kibali Cha gari husika kutoka TEMESA. Agizo hilo limetolewa na meneja wa TEMESA mkoa wa Tanga Mhandisi Jamal Waziri kufuatia baadhi ya wamiliki wa gereji kufanya kazi kinyume na taratibu zilizopo. Aidha Mhandisi Jamal ameainisha gereji hizo kuwa ni LAL GROUP OF CAMPANY, TOYOTA, na ADAMS MOTOR na kusema kuwa hizo ndizo zenye vibali/ithibati ya kutengeneza magari ya serikali kwa mkoa wa Tanga lakini hawapaswi kutengeneza mpaka kuwa na kibali cha gari husika. "Yaani kuwa na kibali kutoka TEMESA haimaanishi kwamba wanaruhusiwa kupokea kila gari,isipokuwa ni gari litakalofika kwao liwe na kibali sasa cha matengenezo husika,sasa baadhi yao wamekuwa wakikaidi na kufanya wanavyotaka wao ila hii itawagharimu kwani hata hicho kibali tutamfutia kabisa kwani kufanya matengene...

TRA TANGA YASISITIZA ULIPAJI KODI KWA WAKATI.

Na Mwanamkuu Mwandoro, Tanga. Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Tanga imeendelea kuwaomba wafanyabiashara kulipa kodi Kwa hiyari na Kwa wakati ili kujiepusha na adhabu zitokanazo na kuchelewa kulipa Kodi ikiwemo faini. Rai hiyo imetolewa na meneja wa TRA mkoa Castro John alipokuwa akizungumza na waandshi wa habari ofisini kwake kufuatia ongezeko la makusanyo ya Kodi tangu walipoadhimisha miaka 30 ya kuanzishwa Kwa mamlaka hiyo ambapo ndani ya miezi miwili wameweza kukusanya kiasi zaidi ya lengo. "TRA mwaka huu tumesherehekea miaka 30 niwashukuru sana walipa Kodi wa mkoa wa Tanga muitikio umekuwa mkubwa kwenye miezi miwili kutoka mwezi July hadi August 2026 tume fanya vizuri tulipangiwa kukusanywa shilingi Billion 75.7 lakini tumevuka lengo na kukusanya Billion 104.9 sawa na asilimia 139" Castro pia amevipongeza vyama vya wafanyabiashara kama Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania (JWT),TNCC,TWCC wamekuwa na mchango mkubwa sana katika kuhakikisha TRA wanafanya vizuri...

GREEN ACRES YAELEZA UMUHIMU WA KUFUNDISHA AKILI MNEMBA

 Na Mwandishi Wetu Mkururugenzi wa shule ya Green Acres ya Mbezi Beach Salasala jijini Dar es Salaam, Jackline Rushaigo, amewataka wazazi kutenga muda wa kukaa na watoto wao kuwafundisha maadili na stadi za maisha. Alitoa wito huo leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza kwenye mahafali ya darasa la saba na shule ya awali ambapo wanafunzi 60 walihitimu elimu ya msingi, Jackline alisema Shule hiyo inatambua umuhimu wa kuzingatia teknolojia za kisasa katika ufundishaji. Alisema wazazi wananafasi kubwa kwenye malezi ya watoto hivyo ni busara kuwa na muda mwingi wa kukaa na watoto na kuwafundisha mambo mbalimbali muhimu zikiwemo stadi za maisha. Aidha, aliwataka wahitimu wa darasa la saba kuendelea kuwa na nidhamu, bidii na kujituma katika masomo wanapoingia katika hatua nyingine ya elimu. Alisema mafanikio ya mwanafunzi hayawezi kutenganishwa na ushirikiano wa karibu kati ya shule, walimu, wazazi na walezi. Alieleza kuwa juhudi za pamoja ni muhimu katika kuhakikisha watoto wanapata...

JESHI LA MAGEREZA LAJIPANGA KUFANYA VIZURI BAMMATA 2026

 Na Ssgt Mawazo Mtondo - MWANZA. Mkuu wa Ofisi ya Michezo na Utamaduni Jeshi la Magereza, Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP) Solomon Mwambingu, leo 19 Septemba, 2026, ameeleza maandalizi na mikakati ya Jeshi la Magereza kuelekea Mashindano ya Baraza la Michezo ya Majeshi Tanzania (BAMMATA) 2026. ACP Mwambingu ameyasema hayo wakati akizungumza na vyombo vya habari katika Ukumbi wa Mikutano wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT), jijini Mwanza, ambapo amesema Jeshi la Magereza limejiandaa vyema katika michezo mbalimbali kuelekea mashindano hayo yanayotarajiwa kufanyika kuanzia Septemba 21 hadi Oktoba 5, 2026, katika Viwanja mbalimbali, jijini Mwanza. Amesema kama sehemu ya maandalizi, Jeshi la Magereza lilifanya Mashindano ya CGP CUP jijini Dar es Salaam mwezi Agosti 2026, kwa lengo la kuziandaa timu na kuhakikisha zinafikia kiwango kizuri cha ushindani kuelekea BAMMATA. “Jeshi la Magereza limejiandaa vyema katika michezo mbalimbali. Tunaendelea kuibua na kukuza vipaji, ambapo...