Skip to main content

Posts

Showing posts from November 22, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Tanzania na Uganda Kuendelea Kuimarisha Ushirikiano

  🚨Ni katika  kuendeleza Sekta za Mafuta na Gesi.  🚨Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi wafikia asilimia 47.  Na Lubango Mleka, Dar es Salaam.  NCHI za Tanzania na Uganda zitaendelea kushirikiana katika uendelezaji wa miradi mbalimbali ya Nishati ikiwemo Sekta ya Mafuta na Gesi ambapo Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi umefikia asilima 47. Hayo yamesemwa leo Novemba 22, 2024 jijini Dar es Salaam na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati,  Dkt. James Mataragio wakati akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya kushiriki Jukwaa la Kibiashara kati ya Tanzania na Uganda. "Tunaangalia ni kwa jinsi gani Sekta hii ya Mafuta na Gesi inaweza ikachangia katika maendeleo ya Nchi hizi mbili, tumekuwa na mijadala mbalimbali inayolenga kuiendeleza sekta hii ya mafuta na gesi." Amesema Dkt. Mataragio.  Ameongeza kuwa, mjadala mkubwa katika jukwaa hilo ni kuangalia namna gani nchi za Tanzania na Uganda zinaweza kushirikiana katika sekta za mafuta na gesi. Mataragio amesema kuwa...

Wilaya Misungwi yaweka Mikakati ya Kukabiliana na tatizo la Lishe Mashuleni

Maafisa Watendaji wa Kata wilayani Misungwi Mkoani Mwanza wametakiwa kuhamasisha Kilimo Cha Mazao ya Chakula na mbogamboga katika Mashamba ya Shule za Msingi na Sekondari ili kukabiliana na kupunguza tatizo la Lishe Mashuleni. Mkuu wa wilaya hiyo Johari Samizi amesema kuwa hatua hiyo itawezesha wanafunzi kupata Chakula Cha kutosha shuleni na hivyo kuondoa Tatizo la utoro na hatimaye kuinua kiwango cha ufaulu.  Samizi ametoa agizo hilo Novemba 22,2024 Wakati wa kikao Cha Kamati ya Lishe ya Halmashauri ya Misungwi mapema.  Kikao hicho kimejadili Hali ya Maendeleo ya Lishe kwa Wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari  Akiwasilisha Taarifa ya Maendeleo na utekelezaji wa Mkataba wa Lishe katika Halmashauri ya Misungwi Afisa Lishe Bi. Lucy ameeleza kwamba Juhudi zinaendelea kuboreshwa ili kuhakikisha suala la Lishe kwa Wanafunzi linapatiwa kipaumbele Lucy amebainisha hivi sasa Shule nyingi zinaendelea kutoa Chakula angalau mara moja kwa mlo mmoja kwa siku kupitia Makubaliano y...

Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Zanzibar: NIT watoa mafunzo kwa madereva, makondakta

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kimetumia Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani visiwani Zanzibar kutoa mafunzo kwa madereva na makondakta wa mabasi ya abiria juu ya usalama barabarani, wakisema kuwaelimisha madereva na makondakta kuhusu kanuni za usalama barabarani na maadili mema ni muhimu sana katika jitihada za kupunguza ajali za barabarani nchini. Hayo yamebainishwa na wataalamu kutoka Chuo cha Taifa cha Usafirishaji ambapo waliongea katika semina kuhusu ‘Kanuni za Usalama Barabarani’ kwa madereva na makondakta wa vyombo vya usafiri wa umma katika kuadhimisha ‘Wiki ya Usalama Barabarani mwaka huu iliyoanza Novemba 12 hadi 23, mwaka huu. Bw Godlisten Msumanje, Mkuu wa Kituo cha Umaahili cha Usalama barabarani cha Kikanda wa NIT amewataka madereva na makondakta nchini, kwenda mara kwa mara kupata mafunzo ili kuwa ‘madereva wa kutegemewa'.  “NIT iliamua kushirikiana na Mamlaka ya Usalama Barabarani Zanzibar (ZARSTA) kuwakumbusha mad...

Wana Mbogwe Msisahau njia kuelekea Mafanikio-Dkt. Biteko

  *📌Awaomba kuchagua viongozi wenye maono* *📌Atahadharisha dhidi ya viongozi wenye kuhubiri chuki na mgawanyiko* *📌Wagombea waomba kuchaguliwa ifikapo Novemba 27* Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM, ambaye pia ni Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe.Dkt. Doto Biteko amewataka wananchi wasisahau safari iliyowafikisha katika nchi ya amani na maendeleo. Dkt. Biteko amesema hayo Novemba 22, 2024 katika wakati akizungumza kwenye mkutano wa Kampeni za Serikali za Mitaa zilizofanyika katika Kata ya Lulembela, Wilaya ya Mbogwe, Geita. Amewataka kujitokeza kuwachagua viongozi wenye maono na mwelekeo wa kuwaunganisha kuanzia ngazi ya shina hadi Taifa.  “ Tunachagua viongozi wenye uelewa wa matatizo na kujua namna ya kutatua matatizo ya wananchi” amesema Dkt. Biteko. Wanambogwe mna haki ya kuchagua  Chama chenye Sera zinazotekelezeka ambacho ni Chama Cha Mapinduzi na kuachana na wale wenye porojo na maneno maneno,  kwa kuwa watu wangependa kupata maendeleo...

Tunakutakia kila la kheri kaka yetu Edwin Soko

 " Tunamtakia heri kaka yetu, kiongozi wetu na mpambanaji wetu wa tasnia ya habari Edwin Soko kuelekea ndoa yake takatifu inayotaraji kufungwa Novemba 23, 2024" wadau wa Habaria

Mhe. Sangu Awaomba Wananchi Jimbo la Kwela Kuwachagua Viongozi wa CCM

Na Hamida Ramadhan - Rukwa. NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kwela Mh. Deus Sangu ametoa wito kwa Wananchi kuendelea kumuunga mkono Rais, Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuwachagua Viongozi wa Serikali za Mitaa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).  Mhe. Sangu ametoa kauli hiyo leo kwa nyakati tofauti wakati akifanya Mikutano ya Kimkakati ya kumuunga mkono Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ya kuwachagua Viongozi katika Kata ya Mfinga, Kalumbaleza, Mwadui na Muze zilizopo katika Jimbo la Kwela, Mkoani Rukwa. Amesema CCM ina kila sababu ya kushinda kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa jinsi ilivyo jipambanua kushughulikia kero zinazowakabili Wananchi wa Jimbo hilo.  Ameendele kusema kuwa, Wananchi wa Jimbo hilo wana kila sababu ya kuwapigia kura Viongozi wa Serikali za Mitaa waliogombea kupitia chama hicho ikiwa ni ishara ya shukrani kutokana na mabilioni ya fedha ambayo Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anayo...

Hope for Girls and Women Tanzania Yawataka Wazazi na Walezi Kuendelea Kuwalinda Watoto

  Fresha Kinasa-Mara.  WAZAZI na walezi  wametakiwa kuendelea kuweka misingi bora ya elimu kwa Watoto na kuwalinda dhidi ya vitendo vya Ukatili wa Kijinsia ili wasome na kufikia ndoto zao.   Hayo yamesemwa Novemba 22, 2024 na Mkurugenzi wa Shirika  lisilo la Kiserikali la  Hope for Girls and Women in Tanzania (HGWT) linalojishughulisha na kutetea haki za Wanawake na Watoto Mkoa wa Mara  Rhobi Samwelly wakati akizungumza   katika mahafali ya sita kwa  wahitimu wa Elimu  ya  Awali ya pili  katika  Shule ya Msingi St. John Bosco iliyopo Mjini Musoma Mkoa wa Mara. Akisoma hotuba yake Rhobi amesema,    ili Watoto wafike mbali kielimu Wazazi na walezi wanalojukumu la kuhakikisha wanaimarisha misingi bora kwa  watoto wao kuanzia nyumbani ikiwemo kuhakikisha wanakuwa na nidhamu ya kupenda kusoma, kufuatilia maendeleo yao kitaaluma,  na kushirikiana na Walimu wao kwa  ukaribu.   Aidha, m...

Rais Samia Atoa Shilingi Bilioni 24 Kutekeleza Miradi ya Maendeleo Namtumbo

Na Mwandishi Wetu-Ruvuma.  Mbunge wa Vijana Mkoa wa Ruvuma (CCM) ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga amempongeza Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa zaidi ya shilingi bilioni 24 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma. Kauli hiyo ameitoa Novemba 21, 2024 wakati wa uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wilaya ya Namtumbo, mkoa wa Ruvuma ambao unalenga kupata Viongozi wa ngazi za Mitaa, Vijiji na Vitongoji hapa nchini. "Serikali kupitia kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kutoa fedha ili kufanikisha utekelezaji wa shughuli za maendeleo ikiwemo ujenzi wa shule ya Wasichana, miradi ya kusambaza umeme kwenye Vijiji na Vitongoji, Elimu, Afya, Kilimo, Maji, Ujenzi wa Kituo cha Polisi na Mahakama katika wilaya hii ya Namtumbo, " Ameeleza Mhe. Kapinga.  Katika Sekta ya Umeme amesema kuwa, Vijiji zaidi ya 12,000 Tanzania Bara vimepata umeme...

Zaidi ya billioni 10 kugharamia Ujenzi wa Skimu ya Umwagiliaji Masimba,Wakulima elfu 24 Mkoani Singida Kunufaika na Skimu hiyo

📍 *NIRC Singida.*  Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba  ambaye ni mbunge wa  Iramba Magharibi ameipongeza Wizara ya Kilimo kwa kuendelea kuboresha sekta ya kilimo nchini kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji  kwani hatua zinazochukuliwa zitaboresha maisha ya Watanzania hasa wakulima. Dkt.Mwigulu amesema kuwa Waziri wa Kilimo Hussein Bashe anaitendea haki sekta ya kilimo na hakuna miujiza katika uchumi zaidi ya mapinduzi yanayofanywa sekta hiyo  inayogusa watu wengi kupitia Umwagiliaji.  Dkt. Mwigulu ametoa kauli hiyo wakati wa hafla ya kukabidhi eneo la mradi wa ujenzi skimu ya umwagiliaji Masimba  kwa mkandarasi iliyopo kata ya Urughu wilaya ya Iramba mkoani Singida. Amesema serikali kupitia Wizara ya Kilimo inatekeleza dira ya Rais kwa kuwahakikishia Watanzania kuwa na kilimo cha kisasa na kufanya mapinduzi ya kilimo kupitia sekta ya kilimo cha umwagiliaji. Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Iramba Magaharibi Mhe. Suleiman Mwenda amesema ni kilio cha...