Skip to main content

Posts

Showing posts from September 9, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

MAJALIWA KUFUNGA MKUTANO MAALUM WA VIONGOZI,WATAALAM NA WADAU WA MAZINGIRA

 MAJALIWA KUFUNGA MKUTANO MAALUM WA VIONGOZI, WATAALAM NA WADAU WA MAZINGIRA Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Septemba 10, 2024 anafunga mkutano maalum wa viongozi, wataalam na wadau wa mazingira kuhusu mwelekeo wa mazingira nchini, katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete jijini Dodoma. madhumuni ya Mkutano huo ni kuchambua hali ya mazingira nchini, kubadilishana uzoefu, na kupanga mikakati madhubuti ya kuhifadhi na kusimamia mazingira. Kauli mbiu ya mkutano huo ni “Mazingira Yetu na Tanzania Ijayo” Tuwajibike sasa.

Makamu wa Rais Apongezwa Kwa Jitihada Zake za Uhifadhi wa Mazingira

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akipokea zawadi ya jitihada za uhifadhi wa mazingira kutoka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Ashatu Kijaji (kulia) pamoja na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhandisi Cyprian Luhemeja (kushoto) wakati wa Mkutano Maalum wa Viongozi, Wataalamu na Wadau wa Mazingira kuhusu Mwelekeo wa Mazingira Nchini unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete mkoani Dodoma. Tarehe 09 Septemba 2024.

Wanachama wa Ushirika wa Social Responsibility Women Group Wazindua Mfuko wa Kuweka Akiba na Kukopeshana

  Na Angela Sebastian- Bukoba  Wanachama wa Ushirika wa kuweka na kukopa wa Social  responsibility (SR) women group  uliopo mtaa wa forodhani kata ya Bakoba Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera,wimezindua mfuko wa kuweka na kukopesha wanachama wake ili kusaidiana na kujikwamua kiuchumi. Hayo yameelezwa na mwenyekiti wa chama hicho salaha Karugaba katika risala yao wakati wa uzinduzi wa mfuko huo uliofanyika ndani ya kata hiyo na kuhudhuriwa viongozi mbalimbali wa chama na Serikali akiwemo mbunge wa viti maalum mkoa wa Kagera kupitia  (Ng'os)Neema Lugangira ambaye alikuwa mgeni rasmi. "Mfuko huu utasaidia wanachama kukopa kwa riba ndogo na kujiongezea kipato bila kuhangaika kwenda kukopa kwenye sehemu nyingine za mikopo zenye riba kubwa na za  kuwaumiza  hivyo,lengo la mfuko huu pia nikuhakikisha chama kinajiendesha chenyewe na kufikia malengo ya kuwa taasisi na kutoa ajira kwa vijana"alieleza Karugaba  Amesema walianza kwa kununua hisa moja kwa wiki y...

MAVUNDE AZINDUA NDONDO CUP 2024 KWA KISHINDO

Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini *Mh. Anthony Mavunde* leo amezindua rasmi ya Ndondo Cup Dodoma 2024 ambayo yanaratibiwa na Mbunge Mavunde kwa ushirikiano na Clouds Media Group. Katika Mashindano hayo yanayoshirikisha Timu 32,m Bingwa wa Mashindano atapata Tsh 15,000,000 na Mshindi wa pili Tsh 7,000,000. Aidha Mbunge amezishukuru Kampuni za GSM na ASAS kwa kuwa sehemu ya ufadhili wa mashindano hayo ambayo yamelenga kwa kiasi kikubwa katika kuibua na kuviendeleza vipaji vya vijana wanamichezo. “Ukiacha burudani,katika mashindano haya tumejipanga kuibua vipaji na kuviendeleza kwa kuwa sisi kwetu michezo si burudani tu bali kwetu sisi michezo ni AJIRA”Alisema Mavunde Akizungumza katika mahojiano leo,Mratibu wa Ndondo Cup *Ndg. Yahaya Mohamed “Mkazuzu”* amesema mashindano ya mwaka huu ya Ndondo yanabeba ujumbe juu ya elimu ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa na pia kwa kushirikiana na Watu wa Marekani elimu inatolewa juu ya masuala ya Afya na hasa kujikinga na maambukizi ya UKIMWI.