Skip to main content

Posts

Showing posts from October 8, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Dkt Samia Aomba Kura Kwa Wananchi wa Lamadi Mkoani Simiyu

 Mgombea nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM na Mwenyekiti wa Chama cha Mapindzii CCM Taifa Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Wananchi, Wanachana na Wapenzi wa CCM wa Lamadi (Busega) katika muendelezo wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu kwa Chama hicho Mkoani Simiyu tarehe 09 Octoba 2025.

Dkt Nchimbi Awasili Nyamwage 'rufiji' | Kusaka Ushindi Wa Dkt Samia

Mgombea mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania kupitia CCM, Balozi Dkt Emmanuel John Nchimbi akiwasili Uwanja wa Soko la Tasaf, katika kata ya Nyamwage, Wilaya ya Rufiji mkoa wa Pwani, kwa ajili ya Kuendelea na Mikutano ya Kampeni za Urais Kuelekea Uchaguzi mkuu utakaofanyika Jumatano ya  Oktoba 29 mwaka huu. Mkoa wa Pwani unakuwa wa 21 kwa mgombea mwenza huyo wa Dkt Samia Suluhu Hassan, wakipeperusha Bendera ya Chama cha Mapinduzi (CCM). Akiwa Nyamwage Dkt Nchimbi atanadi ilani ya Uchaguzi ya CCM na sera zinazolenga kuwaletea maendeleo Wananchi wote. Dkt  Nchimbi atamwombea kura za urais, Dkt Samia Suluhu Hassan, wabunge na madiwani wa CCM. Mgombea mwenza, Dkt Nchimbi atafanya mikutano Jimbo la Rufiji, Jimbo la Kibiti na Jimbo la Mkuranga.

Miradi ya Kusambaza Umeme Vitongojini Kukamilika Ifikapo 2030

*📌Huduma ya umeme kwenye vitongoji yafikia asilimia 58* *📌Majiko banifu 200,000 kuuzwa kwa ruzuku  ya 80% hadi 85% Tanzania bara* *📌Mitungi ya gesi 452,455 ya kilo 6 kuuzwa kwa ruzuku ya 50%* *📌Mifumo 20,000 ya umeme jua kufungwa kwa wakazi maeneo ya visiwani* *📌Serikali kupitia REA kutoa mikopo ujenzi wa vituo vidogo vya mafuta* *📌Watumishi REA waipamba wiki ya huduma kwa wateja* 📍Dodoma Serikali imeeleza mafanikio makubwa ya utekelezaji  wa miradi ya kusambaza umeme maeneo ya vijijini  na pembezoni mwa miji ambapo Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini  (REA) imefanikiwa kufikisha huduma ya umeme kwenye vijiji vyote 12,318 sawa na asilimia 100 na miradi ya umeme kwenye vitongoji inatarajiwa kukamilika ifikapo mwaka 2030. Mafanikio ya miradi ya umeme Vijijini  yamebainishwa leo Oktoba 8, 2025 na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Umeme Vijijini Mha. Jones Olotu wakati akizungumza na Waandishi wa Habari w...

Maelfu ya Wananchi wa Pemba Wajitokeza Kumsikiliza Dkt Nchimbi

 Mgombea Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel Nchimbi, ameendelea na ziara yake ya kampeni visiwani Zanzibar ambapo leo Oktoba 8, 2025, amewasili katika Uwanja wa Ndege wa Pemba. Mara baada ya kuwasili, Dkt. Nchimbi alilakiwa kwa shamrashamra na mamia ya wananchi, viongozi wa chama na jumuiya mbalimbali za CCM waliojitokeza kumpokea kwa hamasa kubwa. Katika siku ya leo, Dkt. Nchimbi anatarajiwa kuanza mikutano yake ya hadhara katika Mkoa wa Kaskazini Pemba, eneo la Kinyasi – Wete, kabla ya kuelekea Mkoa wa Kusini Unguja, ambako atahitimisha kwa mkutano mkubwa wa kampeni katika Jimbo la Chwaka. Ziara hiyo ni sehemu ya mwendelezo wa mikutano ya kampeni ya CCM kusaka ushindi wa kishindo kwa Dkt. Samia Suluhu Hassan (Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania), pamoja na wabunge na madiwani kote nchini.