Skip to main content

Posts

Showing posts from January 6, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Tanapa yatoa elimu kuhusu umuhimu wa uhifadhi na utalii kwa umma

 Afisa Uhifadhi Mkuu Catherine Mbena Mkuu wa Idara ya Mawasiliano - TANAPA akitoa elimu ya Uhifadhi na Utalii kwa umma kupitia Kipindi cha JIRANI cha Radio Crown iliyop jijini, Dar es Salaam leo Januari 06, 2025. Mbali na elimu ya Uhifadhi na Utalii pia ameendelea kutoa msisitizo kwa watalii wa ndani na nje kufuata sheria, taratibu na miongozo ya kuwepo ndani ya Hifadhi za Taifa. Wakati huo huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbas akiongea kwa njia ya simu kupitia kipindi hicho amesisitiza kuwa sheria, taratibu na miongozo ya kuwepo ndani ya Hifadhi za Taifa ifuatwe kwani uhifadhi ndio moyo wa utalii. "Uhai wa wanyamapori wetu ni jambo la muhimu sana kwetu sisi sote Afrika. Hawa viumbe-pori pamoja na mazingira-pori wana yoishi si tu ni muhimu kwa sababu ni chanzo cha maajabu na kuvutia bali hivi ni vitu muhimu katika rasilimali zetu za asili na kwa mustakhabali wa maisha yetu na ustawi wetu…..” Hayati Mwl. Julius K. Nyerere 1961 Afisa Uhifadhi Mkuu Cat...

Mbunge Sagini akerwa na Kasi ndogo ya Ujenzi wa Chuo Kikuu Mwl Nyerere

  Mbunge wa Jimbo la Butiama na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe Jumanne Sagini ameonesha kukerwa na kampuni zinazochelewesha ujenzi wa chuo kikuu cha Mwalimu Julius Kambarage Nyerere cha kilimo na Teknolojia kinachojengwa wilayani Butiama mkoani Mara. Kwa sababu hiyo amezitaka Kampuni za Shabdong Hi Speed Dejian Group Co LTD na Comfix and Engineering LTD zinazotekeleza Mradi wa Ujenzi wa majengo ya Hosteli, Cafeteria, Maktaba na Utawala katika Chuo Kikuu cha Mwalimu Julius Kambarage Nyerere cha Kilimo na Teknolojia (MJNUAT) kukamilisha kwa wakati kama Mkataba unavyoelekeza.  Ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa katika Ziara yake ya Kutembelea na kukagua uendelezaji wa Ujenzi wa Chuo hicho katika Kampasi ya Oswald Mang'ombe kijiji cha  Butuguri na Makao Makuu yaliopo BAIC Butiama.

Tanzania Kushirikiana na Italia Kuendeleza Sekta ya Madini

  ▪️Mkutano wa Wafanyabiashara wa Tanzania na Italia kufanyika Mwezi Februari, 2025. ▪️Kampuni za Utengenezaji Vifaa kutoka vya Madini kutoka Italia  kushiriki. ▪️Wachimbaji kunufaika na teknolojia na mitambo rafiki kwa mazingira 📍Dar es Salaam Waziri wa Madini, *Mh. Anthony Mavunde (Mb)* amesena kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na Italia katika kuendeleza sekta ya madini nchini hususani katika teknolojia na mitambo. Ameyasema hayo jana tarehe 06 Januari, 2025 alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Italia nchini Tanzania, *Mh. Giuseppe Coppola* katika ofisi ndogo za Wizara ya Madini Jijini Dar es Salaam. "Rais wetu *Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan* ameifungua nchi yetu kwa kuimarisha mahusiano kimataifa kupitia falsafa yake ya 4R. Sisi wasaidizi wake tutaendelea kuhakikisha tunasimamia maono hayo na kujenga mahusiano zaidi na washirika wetu kwa manufaa ya uchumi na wananchi wa pande zote. Zipo fursa nyingi k...

Wanafunzi 86 St Anne Marie Academy wachaguliwa shule za vipaji maalum

Na Mwandishi Wetu WANAFUNZI 86 kati ya 156 wa shule ya St Anne Marie Academy ya Mbezi Kimara kwa Msuguri jijini Dar es Salaam waliohitimu darasa la saba wamechaguliwa kujiunga na shule za vipaji maalum. Mkuu wa shule hiyo, Komredi Gladius Ndyetabula alisema jana kuwa wanafunzi wote wa shule hiyo waliohitimu darasa la sana 2024 walipata alama A. Alisema wamefurahi kuona zaidi ya asilimia 55 ya wahitimu wa darasa la saba wanachaguliwa kujiunga na shule za vipaji maalum huku akitaja siri ya mafanikio hayo kuwa ni uwekezaji mkubwa uliofanywa na Mkurugenzi wa shule hizo. Ndyetabula alisema Mkurugenzi wa shule hizo, ambaye ni Mbunge wa Bukoba Vijijini (CCM), Dk. Jasson Rweikiza ameweka mazingira mazuri ya shule hiyo zikiwemo maktaba za kisasa zilizosheheni vitabu vya kutosha na mifumo ya ufuatiliaji matokeo ya mitihani ndani ya shule hiyo. Alisema hata kwenye matokeo ya darasa la nne yaliyotangazwa na Baraza la Mitihani NECTA mwishoni mwa wiki, wanafunzi 100 wa shule hiyo kati ya 174 wamep...

Majaliwa: Ubora wa Miradi Uwiane na Thamani ya fedha zinazotolewa

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ametoa wito kwa wasimamizi wa miradi inayotekelezwa na Serikali ikiwemo ya elimu kuhakikisha inakamilika kwa wakati na kwa ubora unaolingana na thamani ya fedha iliyotolewa. Ametoa wito huo leo (Jumatatu Januari 06, 2025) wakati wa ufunguzi wa Skuli ya Sekondari ya Makoba iliyopo Mkoa wa Kaskazini Unguja, Zanzibar. Ufunguzi wa skuli hiyo ni sehemu ya shamrashamra kuelekea maadhimisho ya miaka 61 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar. Amesema kuwa Serikali imeendelea kutenga rasilimali fedha kwa ajili ya maendeleo ya sekta ya elimu ambayo kwa kiasi kikubwa imewezesha kuweka mazingira bora ya upatikanaji wa elimu ikiwemo ujenzi wa miundombinu. Aidha, Mheshimiwa Waziri Mkuu amesema kuwa katika kipindi cha miaka 61 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameendelea kuipa hadhi sekta ya elimu kwa kuhakikisha kunakuwa na ufanisi wa utoaji wa huduma za elimu. “Sina shaka leo hii chini ya Jemedar...

Dkt. Biteko akagua Ujenzi wa Ofisi ya Waziri Mkuu na Jengo la Wizara ya Nishati

*📌 Aagiza ujenzi ukamilishwe haraka* *📌 Majengo yakamilika kwa asilimia 88* *📌 Wakandarasi waomba nyongeza  siku 90* *Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati* Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amefanya ziara katika Mji wa Serikali, Mtumba jijini Dodoma kukagua maendeleo ya ujenzi majengo ya Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu pamoja na Wizara ya Nishati ambayo ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 88.  Akizungumza baada ya kukagua na kupata maelezo ya wataalam na wasimamizi wa majengo hayo, Naibu Waziri Mkuu Biteko amewapongeza wakandarasi kwa hatua iliyofikiwa na kuagiza majengo yakamilishwe kabla ya mwezi Aprili, 2025. “Serikali chini ya Rais Samia imefanya kazi kubwa, tayari imetoa zaidi ya asilimia 90 ya malipo kwa wakandarasi kwa maana ya kwamba ni kiasi kikubwa zaidi ya ukamilifu wa jengo, Najua SUMA JKT mkifanya kazi kwa operesheni mnaweza kukamilisha ujenzi wa jengo hili hata kabla ya muda uliopangwa” amesema Dkt. Biteko...