Skip to main content

Posts

Showing posts from September 2, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

HII HAPA MIKOA 14 NCHINI ITAKAYOKUMBANA NA EL NIÑO

 WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Prof. Palamagamba Kabudi, ameitaka mikoa 13 iliyopewa tahadhari kujiandaa mapema kukabiliana na madhara yanayoweza kusababishwa na mvua za El Niño. Akizungumza kuhusu utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Dharura wa Kukabiliana na Madhara ya El Niño, Prof. Kabudi amesema mikoa hiyo inapaswa kuhakikisha maandalizi yanafanyika kwa wakati ili kupunguza madhara kwa wananchi na mali zao. Mikoa iliyotajwa ni Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu,Morogoro, Kigoma, Tanga, Pwani, Ruvuma, Mara, Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Dar es Salaam. Prof. Kabudi pia amesisitiza umuhimu wa wananchi kupata na kuzingatia taarifa za tahadhari zinazotolewa na mamlaka husika, huku akivitaka vyombo vya habari kuendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu umuhimu wa maandalizi na hatua za kuchukua. Amesema Serikali, kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, inaendelea kuratibu maandalizi kwa kushirikisha serikali za mikoa, serikali za mitaa na jamii ili kuhak...

SERIKALI YAFAFANUA SHILINGI BILIONI 730 ZA MPANGO WA KUKABILI EL-NIÑO

 SERIKALI imefafanua kuwa makadirio ya Shilingi bilioni 730 yanayotajwa katika Mpango wa Taifa wa Dharura wa Kukabiliana na Madhara ya El-Niño si fedha zilizotengwa na Serikali kwa matumizi ya moja kwa moja, bali ni makadirio ya rasilimali zinazohitajika kutekeleza mpango huo kwa kushirikisha Serikali, taasisi, sekta binafsi, mashirika ya kitaifa na kimataifa pamoja na wadau wengine.  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Prof. Palamagamba Kabudi, amesema mpango huo umeandaliwa kufuatia utabiri wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) wa Agosti 18, 2026, uliotabiri uwepo wa El-Niño yenye nguvu inayoweza kusababisha mvua kubwa, mafuriko, maporomoko ya ardhi, magonjwa ya mlipuko kwa binadamu na wanyama pamoja na madhara kwa miundombinu, makazi na shughuli za kiuchumi.  Amesema mpango huo umeandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikisha Wizara, Idara na Taasisi za Serikali, Mikoa na Halmashauri, mashirika ya kitaifa na kimataifa, ...