Skip to main content

Posts

Showing posts from April 9, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Doris Mollel umestahili tuzo ya WHO, umeokoa maisha ya wengi

Na: Dk. Reubeni Lumbagala Nakumbuka mwalimu wangu wa somo la Uraia (Civics) alipokuwa akitufundisha mada (topic) ya "Haki za "Binadamu" (Human Rights) tulipokuwa Kidato cha Kwanza, alituambia mengi kuhusu haki za binadamu.  Miongoni mwa mikazo yake, alituambia hivi: Haki ya kuishi (Right to life) ndiyo haki kubwa kuliko zote maana mtu anapokuwa hai ndipo anakuwa na uwezo wa kupata haki nyingine zote. Nilimwelewa vizuri sana. Kimsingi, uhai ni muhimu katika maisha ya mwanadamu, ndiyo maana inapotokea mtu ameugua, na akawa hana uwezo wa kumudu gharama za matibabu yake, basi familia, ndugu, jamaa na marafiki hushikamana kwa kuchangishana fedha kunusuru uhai wa ndugu yao huyo. Watoto ni kundi ambalo lipo hatarini kukabiliwa na magonjwa mbalimbali. Ni kutokana na msingi huo, serikali inajitahidi sana kutoa chanjo za magonjwa mbalimbali ili kuimarisha na kujenga afya zao ili kuwa na kinga ya kutosha ya kuweza kupambana na magonjwa. Taasisi ya Doris Mollel (DMF) ni wadau muhimu...

Tanzania: CRJE and Asiano Global Sign Tsh48 Billion Deal to Implement Keyne Center Project in Dar

By Prosper Makene  In a major boost to Tanzania's construction sector, CRJE (East Africa) Ltd and Asiano Global Investment Company Limited have signed a whopping Tsh48 billion deal to build a 26-floor project in Dar es Salaam. The project which is expected to be a game-changer in the city's skyline and will be completed in June 2028. The project is part of Tanzania's Vision 2050, which aims to support the government which has identified infrastructure development as a key priority, and projects like this are expected to play a major role in achieving this goal. The 26-floor project will be located in the heart of Dar es Salaam, providing easy access to key business and social amenities. The project will include commercial spaces, residential apartments, and modern amenities, making it a unique blend of business and luxury living. The project is also a part of a larger trend of investment in Tanzania's construction sector. The government has launched several initiatives ...

Tanzania: CRJE na Asiano Global Saini Makubaliano ya Shilingi Bilioni 48 Kutekeleza Mradi wa Kituo cha Keyne jijini Dar

Na Prosper Makene  Katika kuimarisha sekta ya ujenzi nchini Tanzania, CRJE (East Africa) Ltd na Asiano Global Investment Company Limited wamesaini mkataba wa thamani ya shilingi bilioni 48 wa kujenga mradi wa ghorofa 26 jijini Dar es Salaam. Mradi huo unatarajiwa kuleta mabadiliko makubwa katika anga ya jiji na utakamilika Juni 2028. Mradi huu ni sehemu ya Dira ya Tanzania ya 2050, ambayo inalenga kuunga mkono serikali ambayo imetambua maendeleo ya miundombinu kama kipaumbele muhimu, na miradi kama hii inatarajiwa kuchukua jukumu kubwa katika kufikia lengo hili. Mradi huo wa ghorofa 26 utakuwa katikati ya jiji la Dar es Salaam, ukiwapa ufikiaji rahisi wa huduma muhimu za biashara na kijamii. Mradi huo utajumuisha maeneo ya kibiashara, vyumba vya makazi, na huduma za kisasa, na kuufanya kuwa mchanganyiko wa kipekee wa biashara na maisha ya anasa. Mradi huu pia ni sehemu ya mwelekeo mkubwa wa uwekezaji katika sekta ya ujenzi nchini Tanzania. Serikali imezindua mipango kadhaa ya kuvut...

Watendaji Ofisi ya Waziri Mkuu Wakumbushwa Kuimarisha Weledi Kutimiza Dira ya Taifa 2050

Na. MWANDISHI WETU -DODOMA Watendaji wa Ofisi ya Waziri Mkuu wamekumbushwa kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa weledi, ufanisi na kujituma ili kuhakikisha wanachangia kikamilifu katika kufanikisha malengo ya Dira ya Taifa 2050, hususan katika maeneo ya sera, uratibu na usimamizi wa utekelezaji wake. Wito huo umetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Mhe. Prof. Palamagamba J.A. Kabudi, wakati akizungumza na watumishi wa Ofisi hiyo mara baada ya kuwasili rasmi na kupokelewa na uongozi na watumjshi wa Ofisi hiyo katika Jengo la Ngome Jijini Dodoma tarehe 8 Machi, 2026 Prof. Kabudi alisisitiza umuhimu wa ushirikiano na ubunifu miongoni mwa watumishi ili kuongeza ufanisi wa utendaji kazi. “Ni muhimu tushirikishane mawazo na kufanya kazi kwa pamoja ili kumsaidia Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kufanikisha adhima ya maendeleo yenye kuleta ustawi na furaha kwa Watanzania," alisema Prof. Kabudi Aliongezea kuwa upo umuhimu wa kus...

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Afanya Mazungumzo na Balozi wa Qatar Tanzania

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa, Mhe.Dkt.Rhimo Nyansaho, (Mb) tarehe 8 April, 2026 amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Dola ya Qatari Nchini Tanzania, Mheshimiwa Balozi , Fahad Rashid AL-Muraikhi, jijini Dodoma  Balozi Fahad Rashid AL-Muraikhi alimueleza Waziri wa Ulinzi na JKT utayari wa Dola ya Qatari kushirikiana na Tanzania na katika masuala mbalimbali yanayohusiana na Wizara ya Ulinzi na Nchi kwa ujumla . Balozi Fahad Rashid AL-Muraikhi alisema Tanzania na Dola ya Qatari zimekuwa na mahusiano ya muda mrefu ambayo yamekuwa ni chachu ya maendeleo baina ya Nchi hizo mbili , mahusiano hayo yamekuwa yakiongozwa na viongozi wakuu wa Nchi ya Tanzania na Dola ya Qatari ambapo Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan alifanya ziara ya kikazi Nchini Qatari mwaka 2023 . Ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan Nchini humo ni kielelezo Cha utayari wa Tanzania kushirikiana na Dola ya Qatari katika nyanja mbalimbali za kiuchumi , ...

Tutaboresha Bajeti ya Elimu – Waziri Mkuu

_▪️Asema Serikali itaimarisha vitengo vya tathmini na ufuatiliaji kila wizara_ Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Serikali itaendelea kuboresha bajeti ya elimu wakati ikitekeleza mtaala mpya wa elimu ili kuziba mianya ya mahitaji shuleni. “Kwa kuwa tunaenda katika mtaala mpya wa elimu, tutaendelea kuboresha bajeti. Tutaendelea kuboresha bajeti kwa sababu mahitaji yanaongezeka kila wakati katika kumfanya mtoto asome vizuri,” amesema. Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo Bungeni jijini Dodoma, leo (Alhamisi, Aprili 9, 2026) wakati akijibu swali la Mbunge wa Segerea, Agnesta Lambert Kaiza, kwenye kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu ambaye alitaka kujua kauli ya Serikali juu ya kukomesha michango holela inayotozwa shuleni. Dkt. Mwigulu amesema Serikali haina shida na michango ya chakula ambayo imekuwa ikitolewa shuleni lakini akasisitiza kuwa endapo kutatokea michango mingine yoyote, ni lazima ifuate miongozo ya serikali na ipate baraka za Wakuu wa Mikoa husika. Akitoa mfan...

Tanzania: CRJE and Asiano Global Sign Tsh48 Billion Deal to Implement Keyne Center Project in Dar

By Prosper Makene  In a major boost to Tanzania's construction sector, CRJE (East Africa) Ltd and Asiano Global Investment Company Limited have signed a whopping Tsh48 billion deal to build a 26-floor project in Dar es Salaam. The project which is expected to be a game-changer in the city's skyline and will be completed in June 2028. The project is part of Tanzania's Vision 2050, which aims to support the government which has identified infrastructure development as a key priority, and projects like this are expected to play a major role in achieving this goal. The 26-floor project will be located in the heart of Dar es Salaam, providing easy access to key business and social amenities. The project will include commercial spaces, residential apartments, and modern amenities, making it a unique blend of business and luxury living. The project is also a part of a larger trend of investment in Tanzania's construction sector. The government has launched several initiatives ...

Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Akutana na Ujumbe wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola

  Mhe. Lazarus Chakwera, Rais wa Zamani wa Malawi na Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola, Mhe. Shirley Ayorkor Botchwey amekutana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo jijini Dar Es Salaam Aprili 09, 2026. Mkutano huo ulilenga kumkaribisha nchini na pia ni ishara ya kuanza ratiba yake ya kukutana na wadau mbalimbali ikiwamo kukutana na ujumbe wa Serikali Aprili 09, 2026 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere.

Magonjwa ya moyo yaendelea kuiongoza kwa vifo Duniani-JKCI yatoa tahadhari

TAASISI ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) imebainisha kuwa magonjwa ya moyo yanaendelea kuwa tishio kubwa kwa afya ya binadamu duniani, yakiongoza kwa kusababisha vifo zaidi kuliko magonjwa mengine. Akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dodoma kuhusu Miradi ya Maendeleo na Fursa za Vijana kwa Mwaka 2025/26, Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Dkt. Peter Kisenge, amesema kuwa takwimu zinaonesha hali ya kutia wasiwasi, ambapo kutokana na maradhi hayo yanayoweza kuzuilika kwa kiasi kikubwa iwapo hatua stahiki zitachukuliwa mapema. Amesema kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO), takribani watu milioni 17.9 hufariki dunia kila mwaka kutokana na magonjwa ya moyo, hali inayochangia karibu asilimia 75 ya vifo vinavyotokea katika nchi zenye kipato cha chini na cha kati. Dkt. Kisenge amesisitiza kuwa mabadiliko ya mtindo wa maisha, ikiwa ni pamoja na lishe isiyo bora, ukosefu wa mazoezi, matumizi ya tumbaku pamoja na unywaji wa pombe, ni miongoni mwa sababu kuu zinazochangia onge...