Skip to main content

Posts

Showing posts from February 5, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Wabunge wamchagua Dkt Mahera kuwa Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Bunge

Waliochaguliwa TUME YA UTUMISHI WA BUNGE 1. Dkt. Dotto Mashaka Biteko 2. ⁠Charles Mahela 3. ⁠Dkt. Catherine Walioshinda PAP - BARA 1. Lulu Mwacha - 290 2. ⁠Mariam Mungula - 280 3. ⁠Joshua Nassari - 280 Walioshinda SADC PF- BARA 1. Prof Ndalichako 2. ⁠Lutengano Mwalwiba - 270 3. ⁠Mwanahamisi Munkunda - 290 Waliochaguliwa IPU - BARA 1. Pindi Chana - 283 2. ⁠Fatma Rembo - 276 3. ⁠Elibariki Kingu - 285 4. ⁠Asha Ferouz - 267 5. ⁠Rashid Shangazi - 290 6. ⁠Kiza Mayeye - 251 Waliochaguliwa JUKWAA LA NCHI ZA MAZIWA MAKUU - BARA 1. Slvia Sigula - 286 2. ⁠Ezra Chiwelesa - 285 3. ⁠Cosmas Bulala - 255 4. ⁠Bakari Shingo - 242 NB: Kuna waheshimiwa vigogo wamepata zile kura zetu za wajumbe (namba ndogo)

Wassira arejesha matumaini kwa wanaccm mkoa wa Mara

MARA Makamu Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi CCM mzee Steven Masato Wassira ameongoza harambee kubwa ya kuchangia fedha kwa ajili ujenzi na ukarabati ofisi za CCM wilayani Bunda baada ya zilizokuwepo kuteketezwa na moto katika machafuko ya Oktoba 29 mwaka 2025. Katika harambee hiyo ambayo imeongozwa na mzee Wassira imeshirikisha viongozi mbalimbali wa mkoa wa Mara na kufanyika chuo cha ualimu Bunda ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya kuzawali kwa chama hicho. Akizungumza katika sherehe za maadhimisho ya kumbukizi ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo February 5,2026, Makamu Mwenyekiti huyo amesema lengo la kujengwa Kwa ofisi ya chama Chama Cha mapinduzi wilaya ya Bunda ni Kwa ajili ya kuskiliza kero za wananchi na kuzitatua. Kiasi cha shilling Millioni Mia nne arobaini kimechangwa katika harambee hiyo ambapo kiasi kinachotakiwa ili.kumaliza ujenzi wa Ofisi hizo ni shillingi Million mia saba. "Siwezi kukarabati nyumba yangu wakati wilaya ya bunda haina ofisi ya chama Cha ma...

Dkt. Mwigulu Amkabidhi Nanauka Hundi ya Sh. Bilioni 200

_Ni utekelezaji wa ahadi za Rais Dkt. Samia ndani ya siku 100 tangu achaguliwe_ WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba amekabidhi hundi ya shilingi bilioni 200 kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Maendeleo ya Vijana, Joel Nanauka ikiwa ni utekelezaji wa vitendo wa ahadi ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyoitoa wakati wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, ya kutenga na kutoa mitaji kwa ajili ya kuwawezesha vijana na wanawake. Pia, Waziri Mkuu amesema uwezeshaji wananchi kiuchumi ni mhimili wa kukuza uzalishaji, biashara, uwekezaji na ustawi wa maisha ya wananchi, hasa vijana na wanawake ambapo amezitaka wizara, taasisi na mamlaka za kisekta zinazoendelea kutekeleza mpango huo kuhakikisha fedha hizo zinawafikia walengwa wote na program zilizokusudiwa na kutoa tija tarajiwa.   “Utoaji wa Hundi ya Shilingi Bilioni 200 unaonesha kwa vitendo kwamba Serikali ya Awamu ya Sita inatekeleza ahadi zake kwa vitendo, si kwa maneno. Tukio hili linaweka msingi mpya wa kuimarisha ushiriki...

Rais Samia Atekeleza Ahadi Yake ya Bilioni 200 Kwa Ajili ya Mitaji Kwa Vijana na Wanawake

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba akimkabidhi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Maendeleo ya Vijana Mhe. Joel Nanauka, hundi ya shilingi bilioni 200 ambazo ni ahadi ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya mitaji ya kuwawezesha vijana na wanawake, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Februari 05, 2026. kulia  ni kutoka kwa Waziri wa Fedha Balozi Khamis Mussa Omar na kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) William Lukuvi.   Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba akipokea kutoka kwa Waziri wa Fedha Balozi Khamis Mussa Omar hundi ya shilingi bilioni 200 ambazo ni ahadi ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya mitaji ya kuwawezesha vijana na wanawake, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Februari 05, 2026.