Mfanyabiashara Maarufu Nchini, Otieno Olunga Igogo, ameeleza namna alivyoguswa kufuatia kifo cha shemeji yake, Dkt. Alex Seka Odemba, aliyefariki dunia katika Jimbo la Michigan nchini Marekani siku chache zilizopita. Akizungumza kuhusu tukio hilo, Mzee Igogo amesema kuwa familia imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo hicho, akieleza kuwa marehemu alikuwa nguzo muhimu ya familia, mtu mwenye busara, upendo na aliyekuwa mstari wa mbele kuimarisha mshikamano wa ndugu na jamaa. Aidha, Igogo ameeleza kuwa hakuna aliyedhani kuwa Dkt. Odemba angefariki katika kipindi ambacho alikuwa akijiandaa kufunga maisha yake nchini Marekani na kurejea Tanzania kuanza makazi mapya ambapo amesema siku moja kabla ya safari yake, marehemu alianza kujisikia vibaya kutokana na homa ya ghafla na kukimbizwa hospitalini, ambapo baadaye alifariki dunia. Pia, Ameongeza kuwa taarifa za msiba huo ziliishtua familia na marafiki waliokuwa wakiamini kuwa wangempokea Tanzania ndani ya muda mfupi. Badal...
Marato tv - Sauti ya Jamii